Nyumbani » 19/11/2013 Entries posted on “Novemba 19th, 2013”

Baraza la Usalama lalaani vikali shambulizi la bomu Lebanon

Kusikiliza / Rais wa Baraza la Usalama Balozi Liu Jieyi wa Uchina

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamelaani vikali shambulio la bomu lililotekelezwa dhidi ya ubalozi wa Iran mjini Beirut, Lebanon, ambalo limewaua watu wapatao 23 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 140 karibu na ubalozi huo. Kundi moja linajihusisha na kundi la kigaidi la Al-Qaeda limedai kutekeleza shambulizi hilo. Wanachama wa Baraza la [...]

19/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa vyoo wahatarisha afya za wananchi nchini Kenya

Kusikiliza / MKURU KWA NJENGA

Dunia ikiadhimisha siku ya choo duniani leo Nov 19, 2013 baadhi ya nyumba bado hazina vyoo. Takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 kote duniani hawana vyoo hatua inayoweza kusababisha matatizo ya afya kwao. Mwandishi wetu Jasson Nyakundi anamulika hali ilivyo nchini Kenya ambapo anazungumza na Samwel Waweru akiwa Mukuru Kwa njenga anayemiliki choo cha [...]

19/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulizi huko Lebanon

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu vikali shambulio la kigaidi lililotokea leo karibu na ubalozi wa Iran uliopo mji mkuu wa Lebanon, Beirut na kusababisha vifo vya raia 23 akiwemo mwanadiplomasia mmoja wa Iran na majeruhi zaidi ya mia moja. Ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za waliokufa pamoja na serikali [...]

19/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Afrika hatarini kuingia kwenye gharama kubwa –UNEP

Kusikiliza / Gharama ni kubwa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi:UNEP

 Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP imesema kuwa gharama ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika itaongezeka kwa kiasi kikubwa iwapo hatua mahsusi hazitachukuliwa hivi sasa. Yakadiriwa kwamba Afrika inaweza ikaingia gharama ya dola Bilioni 350 kila mwaka ifikapo mwaka 2070 iwapo wakati huu itashindwa kutekeleza mipango [...]

19/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya watu wahama mapigano nchini Syria na kuingia nchini Lebanon

Kusikiliza / Wasyria wanokimbia kuelekea Lebanon (UNHCR)

Takriban watu 6000 wamekimbia makwao eneo la Qarah  nchini Syria  ambapo wamevuka mpaka na kuingia mashariki mwa Lebanon. Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yamekuwa nchini Lebanon tangu juma lililopita yakifanya kazi na wizara inayohusika na masuala ya kijamii kukabiliana na hali hii. Kuhama huku kumetokana na  kuongezeka kwa ghasia eneo la Qarah na vijiji [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji zaidi ya milioni tano wanaishi Italy: IOM

Kusikiliza / Wahamiaji wanaotumia boti kusafiri hadi Italia

Ripoti ya kuhusu uhamiaji iliyozinduliwa na ofisi ya taifa ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Italia na taasisi ifahamikayo kwa jina la IDOS inaonyesha kuwa nchi hiyo ina wahamiaji zaidi ya milioni tano ambayo ni asilimia 7.4 ya idadi ya watu. Ripoti hiyo kadhalika inabainisha kuwa wahamiaji nchini Italia wanachangia asilimia 12 ya pato la [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OHCRM yatilia shaka baada ya kuzuka upya machafuko Libya

Kusikiliza / Ofisi ya haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani na kuelezea masikitiko yake kutokana na kujirudia upya machafuko nchini Libya ambayo yamesababisha zaidi ya watu 40 kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa tangu yaliyozuka ijumaa iliyopita. Grace Kaneiya na maelezo kamili  (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Kumekuwa na ongezeko kubwa la umwagaji damu katika mji [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi waendelea na kuhama wakitafuta misaada nchini Ufilipino

Kusikiliza / Waathirika wa Kimbunga Haiyan wahama kutafuta misaada

Maelfu ya  watu walionusurika kimbunga Haiyan kutoka maeneo ya Tacloban nchini Ufilipino wameripotiwa kuhama makwao wakitafuta wenzao na misaada kwenye maeneo yaliyo karibu na pia ya mabli kama Cebu naManilakwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. UNHCR inasema kuwa muda mfupi baada ya kimbunga kuikumba Ufilipino watu walianza kuondoka kwa [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa COP19 wafunguliwa, viongozi watakiwa kufikiria kwa mapana zaidi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akihutubia mkutano wa COP19 huko Warsaw, Poland

Mkutano wa ngazi ya juu wa mabadiliko ya tabia nchi, umefunguliwa rasmi huko Poland ambapo Umoja wa Mataifa umetaka viongozi kutokuwa wabinafsi katika fikra za mabadiliko ya tabianchi, huku shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa likitoa ripoti inayosema kuwa gharama za kukabili mabadiliko ya tabianchi Afrika itaongezeka iwapo hatua hazitachukuliwa. Assumpta Massoi na ripoti [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya choo duniani:UM

Kusikiliza / Choo

Leo ni siku ya choo duniani inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa huku kukitolewa wito wa kuboresha mazingira na kuzingatia usafi wa vyoo vyenyewe. George Njogopa na taarifa zaidi (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Siku hii ya choo duniani inakumbusha ulimwengu kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 duniani kote wanakabiliwa na matatizo yanayoambatana na ukosefu wa vyoo [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaendelea kuratibu misaada ya madawa Ufilipino:

Kusikiliza / Hospitali ya muda Ufilipino

Ikiwa ni zaidi ya siku kumi tangu kuzuka kwa kimbunga Haiyan nchini Ufilipino, shirika la afya duniani WHO linaendelea kuleta wataalamu wa kitabibu kutoka sehemu mbalimbali wanaokwenda Ufilipino . Hivi sasa kwa mujibu wa shirika hilo wanajikita zaidi kwa majeruhi na wale walioathirika kisaikolojia na kimbunga hicho huku wakitilia maanani mahitaji ya muda mrefu ya [...]

19/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Familia nyingi Tacloban zimepoteza kila kitu:UNICEF.

Kusikiliza / Waathirika wa kimbunga Haiyan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema uharibifu uliosababishwa na kimbunga Haiyan mjini Tacloban na voinga vyake ni mkubwa saana. Linasema familia nyingi zimepoteza kila kitu na msaada ndio unaanza kuwafikia huku serikali na mashirika ya makanisa yakiendelea kuwasaidia. Kwa mujibu wa UNICEF msaada wa haraka unahitajika ili kuzuia kusambaa kwa magonjwa [...]

19/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Filamu ya Mary na Martha yatanabaisha athari za malaria

Kusikiliza / Mbu wasabibishao Malaria

Mpango wa kimataifa wa kudhibiti malaria,The Roll Back Malaria umeshirikiana na Richard Curtis ambaye ametengeneza filamu iitwayo Mary and Martha inayojikita katika kutanabaisha mkasa wa gonjwa la malaria. Mada kuu ya filamu hiyo ni safari ya mama hao wawili mmoja toka Marekani na mwingine uingereza na kila mmoja wao ameathirika na malaria na maisha yao [...]

19/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 13 wameathirika na kimbunga Haiyan:OCHA

Kusikiliza / Waathirika wa kimbunga Haiyan

Idara ya ustawi wa jamii na maendeleo ya Ufilipino inakadiria kwamba watu milioni 13 wameathirika na kimbunga Haiyan na wengine milioni 4 wametawanywa , limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. OCHA imeongeza kwamba watu zaidi ya 392,000 wanaishi katika vituo vya muda 1,587 ambavyo vingi [...]

19/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031