Nyumbani » 15/11/2013 Entries posted on “Novemba 15th, 2013”

Urejeshaji wa wakimbizi wa Burundi walioko Uganda wamulikwa

Kusikiliza / Wakimbizi wa Burundi walioko Uganda

Burundi,Ugandana Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR wamefikia makubaliano ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Burundi waliochukua hifadhi  nchiniUganda. Hii ni baada ya kikao cha pande hizo tatu kilichofanyika hivi karibuni mjini Bujumbura Burundi.Uganda imewapa hifadhi zaidi ya wakimbizi elfu 10 kutoka Burundi, sehemu kubwa walikimbia machafuko ya mwaka wa 1993. Shughuli hiyo [...]

15/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Huu ni ushindi kwa Afrika, haturudi nyuma -Balozi Macharia

Kusikiliza / Macharia Kamau

Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa balozi Macharia Kamau amesema kile kinachoonekana kama kushindwa kwa ombi la Umoja wa Afrika kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya yaliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC ni ushindi mkubwa kwa Afrika. [...]

15/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNECE yataka hatua kuchukukuliwa ulimwengu unapoadhimisha siku ya choo duniani

Kusikiliza / world_toilet_day

Huku watu watu bilioni sita kati ya watu bilioni saba duniani kwa sasa wakiwa wanamiliki simu za mkononi ni watu bilioni 4.5 tu walio na choo, watu bilioni 2.5 wakiwa hana choo za kisasa huku watu wengine bilioni moja wakiwa hawa choo kabisa kwa mjibu wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya [...]

15/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Suala la kuahirisha kesi ya viongozi wa Kenya ICC halijaenda kombo: Balozi Macharia

Kusikiliza / Balazi Macharia Kamau

Mwakilishi wa kudumu wa KenyaKwenye Umoja wa Mataifa Balozi Macharia Kamau akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi tu baada ya Baraza la Usalama kukataa rasimu ya azimio la kuahirisha hadi wakati muafaka kesi zinazokabili viongozi waandamizi wa Kenyakwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague. Balozi Kamau amesema kilichojiri kwenye upigaji kura [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yawasaidia wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu kutoka Ulaya:

Kusikiliza / iom logo

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Ufaransa limezindua mradi wa kuwarejesha katika maisha ya kawaida wahanga 130 wa usafirishaji haramu wa binadamu ambao wameamua wanataka kurejea kwa hiyari katika nchi walizotoka barani Afrika, Asia na Amerika ya Kusini wakitoka katika nchi za muungano wa Ulaya. Mradi huo wa pamoja walioouita CARE una lengo la [...]

15/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuwalinda wakimbizi wa ndani Sudan Kusini kupewe kipaumbele:Beyani

Kusikiliza / Chaloka Beyani

Hatua za kibinadamu, kujumuishwa katika katiba, maendeleo na hatua za kuleta amani ni viungo muhimu kwa suluhu ya wakimbizi wa ndani na wale wanaorejea nyumbani. Hayo yamesemwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani ambaye ameongeza kuwa maendeleo na amani haviwezi kupatikana wakati maelfu ya [...]

15/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO na washirika wake wameanza kuwafikia wanaohitaji msaada katika visiwa vingi Ufilipino:

Kusikiliza / typhoon_philippines_20131113

Shirika la afya duniani WHO linafanya kazi kwa karibu na serikali ya Ufilipino na wadau wengine wa kimataifa kuwafikia manusura wa kimbunga Haiyan ambao wanahitaji huduma za afya. Hali halisi ya athari za kimbunga hicho inaanza kubainika sasa huku maeneo mengi yakihitaji msaada. Takribani majimbo saba yameathirika na kimbunga hicho ambayo ni Samar, Leyte, Cebu, [...]

15/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yalaani ubaguzi dhidi ya waziri wa sheria wa Ufaransa:

Kusikiliza / Waziri Christiane Taubira

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira. Kwa mujibu wa ofisi hiyo mashambulizi hayo ya wiki chache zilizopita yanajumuisha habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la kila wiki lililotoka Jumatano likiambatanisha picha yake na kichwa cha habari "hila [...]

15/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa mafuta waathiri jitihada za utoaji misaada Ufilipino:UM

Kusikiliza / typhoon-haiyan3

Nchini Ufilipino ambako wakati mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiendelea na jitihada za kutoa misaada kwenye maeneo yaliyokumbwa na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino uhaba mkubwa wa mafuta umekwamisha jitihada za kuwafikia mamilioni ya watu walioathiriwa na kimbunga hicho. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa hata [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakataa ombi la Kenya la kutaka kesi ziahirishwe

Kusikiliza / Baraza la usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo baada ya kupokea ombi kutoka Umoja wa Afrika la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya iliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC imepiga kura na kupinga ombi hilo. Flora Nducha na ripoti kamili.  (Ripoti ya Flora)  Ijumaa asubuhi wajumbe wa Baraza la [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wanaojaribu kuingia Ulaya wakataliwa na kurejeshwa walikotoka:UNHCR

Kusikiliza / Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema linatiwa hofu na hatua ya baadhi ya nchi za muungano wa Ulaya kuweka vikwazo vya kuingia au kuwarejesha kwa nguvu watu wanaoomba hifadhi wakiwemo wale waliokimbia machafuko nchini Syria. Kwa mujibu wa shirika hilo Bulgaria mwishoni mwa wiki iliwakatalia kuingia wakimbizi 100 na kuweka polisi [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA yakamilisha uchunguzi Australia

Kusikiliza / IAEA LOGO

Timu ya wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu nguvu za atomiki IAEA leo limekamilisha tathimini ya usalama nchini Australia namna taifa hilo linavyochukua hatua za usalama kuhusiana na matumizi ya nukilia. Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wamekuwa nchini humo kwa muda wa wiki mbili ambako pa moja na kufanya ukaguzi wa mitambo [...]

15/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Misaada ya UNHCR kwa waathirika wa kimbunga Philippine yaanza kuwasili

Kusikiliza / philippines12nov

Kumekuwa na ongezeko kubwa la misaada kwa waathirika wa kimbunga Haiyan kilichowakumba raia wa Ufilipino baada ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kusambaza misaada kadhaa kwa njia ya ndege. Ndege mbili za shirika hilo zimekuwa zikidondosha misaada eneo Cebu ambalo limeaathiriwa zaidi na juhudi za kuyafikia maeneo mengine ikiwemo mji wa [...]

15/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni Wakati wa kutoa mchango wa kweli kukabiliana na tabia nchi: Mtaalam wa UM

Kusikiliza / HRC 21

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu na mshikamamo wa pamoja duniani Virginia Dandan, amezitaka nchi kutoa michango ya kweli ili kukabiliana na tatizo la tabia nchi.  George Njogopa na taarifa kamili (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Wito wa Bi Dandan umekuja katika wakati ambapo wataalamu wa majadiliano ya mapatano kutoka mataifa [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Heko Afrika kwa kuchukua hatua kulinda albino: Ofisi ya Haki za binadamu

Kusikiliza / Albinos_Senegal_IRIN-Helen-Blakesley

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imepongeza hatua ya Tume ya Afrika ya kuridhia azimio la kwanza la ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi barani humo au Albino huku ikisema kilichobakia sasa ni utekelezaji na elimu kwa umma juu ya haki za msingi za kundi hilo. Msemaji wa Ofis hiyo Rupert [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031