Nyumbani » 14/11/2013 Entries posted on “Novemba 14th, 2013”

Baraza la Usalama lataka udhibiti wa vikosi vya FDLR

Kusikiliza / Kikosi cha MONUSCO kikiwa kwenye doria huko DR Congo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia taarifa ya Rais wa baraza hilo ambayo pamoja na mambo mengine inakaribisha kumalizika kwa uhasama kati ya serikali ya DR Congo na waasi wa M23 na kusema kutaka hitimisho la haraka la mazungumzo ya Kampala yanayotoa fursa ya kupokonywa silaha waasi na kuwajibika kwa waliokiuka haki za [...]

14/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban asifu hatua za maendeleo Latvia

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelipongeza taifa la Latvia kwa kuendeleza haki za binadamu, kuwapa wanawake nguvu na kuendeleza usawa wa jinsia. Bwana Ban amesema hayo katika mkutano na waandishi habari wakati wa ziara yake nchini humo, akiongeza kuwa taifa hilo huchangia mara kwa mara kwa ajenda ya kimataifa ya amani, [...]

14/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Kisukari umebadili maisha yangu: Mkazi wa Tanga, Tanzania

Kusikiliza / Mkoani Morogoro Daktari akimpima Kisukari mmoja wa wakazi

Mtu anapopatiwa taarifa ya kwamba ana ugonjwa wa Kisukari, punde maisha yake hubadilika! Hulazimika kuchukua hatua kadhaa ikiwemo matibabu ya kila siku, kubadili mlo na hata mfumo wa maisha. Kama mtu alizowea mtindo fulani wa maisha hulazimika kubadili iwapo anataka kupata ahueni au kudhibiti ugonjwa huo. Shirika la afya duniani linasema hivi sasa kuna wagonjwa [...]

14/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

ICC yaitaka Libya imkabidhi Saif al Gaddafi kwa mahakama hiyo

Kusikiliza / Fatou Bensouda, Mwendesha mashtaka wa ICC(Picha ya faili)

Serikali ya Libya imeombwa imkabidhi Saif al Gaddafi kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, ili afunguliwe mashtaka. Wito huo umetolewa na Mwendesha Mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, wakati akilihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchiniLibya. Joshua Mmali na taarifa kamili TAARIFA YA JOSHUA Bi Bensouda amesemaLibyaimepiga hatua kadhaa kisheria, ikiwemo kuridhia mkataba wa Rome, [...]

14/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Chanjo ya Malaria sasa majaliwa 2030: WHO

Kusikiliza / Watoto, kizazi kijacho

Shirika la Afya duniani, WHO limetangaza lengo la kuwa na leseni ya chanjo dhidi ya Malaria ifikapo mwaka 2030. Imesema chanjo hiyo itakuwa na uwezo wa kupunguza wagonjwa wa Malaria kwa asilimia 75 na kutokomeza kabisa ugonjwa huo.  Taarifa zaidi na Flora Nducha.  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Mkurugenzi anayehusika na  mpango wa ugonjwa wa Malaria [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wametelekezwa: Mia Farrow

Kusikiliza / Watoto CAR

Jamhuri ya Afrika ya Kati  balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Mia Farrow ametaka hatua za haraka kumaliza ghasia nchini humo kwani raia ndio wanaoteseka na yaonekana wametelekezwa. Jason Nyakundi na ripoti kamili. (Ripoti ya Jason) Akizungumza baada ya ziara ya juma moja nchini humo Bi Farrow amelitaja taifa [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa tushikamane kuwasaidia waathirika wa kimbunga Ufilipino:Amos

Kusikiliza / Valerie Amos, OCHA azuru jamii zilizoathirika na kimbunga Haiyan, Ufilipino

Mratibu wa Umoja wa mataifa wa misaada ya dharura Bi Valarie Amos Alhamisi amezungumzia haja ya mshikamano wa jumuiya ya kimataifa kuwasaidia waathirika wa kimbunga Haiyan nchini Ufilipino. Bi amos Jumatano alikwenda Tacloban moja ya maeneo yaliyoathirika vibaya sana na kimbunga hicho ambako amezungumza na manusura wasio na malazi , wakisubiri wa hamu msaada kuwafikia. [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makampuni yalitumia fedha nyingi zaidi kwa kujitangaza:WIPO

Kusikiliza / Francis Gurry, Mkurugenzai Mkuu, WIPO

Makampuni kote duniani yanatumia hadi dola nusu trillion kila mwaka kwa kutangaza majina yao zaid ya fedha zinazotumika kwenye utafiti na hata zaidi ya uwekezaji mzima wa kampununi . Alice Kariuki na maelezo kamili. (RIPOTI YA ALICE KARIUKI) Hayo yameelezwa kwenye ripoti ya shirika la kimataifa linalohusika na kulinda mali WIPO , ambalo limefanya uchambuzi [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Kisukari wakwangua mifuko ya wagonjwa

Kusikiliza / Vipimo vya kiwango cha sukari

Ikiwa siku ya Kisukari duniani hii leo ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio kila uchao na sasa inaelezwa kuwa watu Milioni 350 duniani, sawa na asilimia Tano ya wakazi wote wana ugonjwa wa kisukari na idadi inatarajiwa kuongezeka. Ujumbe wa siku hii ni eneza ufahamu kuhusu Kisukari na kinga dhdi yake. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mipango kukabiliana na athari zisizoepukika za mabadiliko ya hali ya hewa inafanywa:UNFCCC

Kusikiliza / Kimbunga

Wakati wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wanakutana Warsaw, Poland kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa, nchi masikini kabisa duniani zinakamilisha mipango ya kukabiliana na athari zisizoepukika za mabadiliko ya hali ya hewa . Mikakati hiyo inasaidiwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC, kitengo cha kimataifa [...]

14/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mchezo wa baiskeli ni mtaji wa mshikamano Rwanda

Kusikiliza / Rising-from-Ashes

Rwanda, taifa ambalo lilitatizika kwa mauaji ya halaiki takribani miaka 20 iliyopita, sasa liko katika mchakato wa utangamano. Hatua hii jumuishi inahitaji sekta zote kuwajibika, na hii ndio sababu ya kuanzisha mchezo wa basikeli wenye lengo la kuwaweka vijana  na kamundi mbalimbali pamoja bila kujali tofauti zao.  Ungana na Joseph msami katika makala inayomulika filamu [...]

14/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Tuchukue hatua mapema kudhibiti ugonjwa wa Kisukari: Ban

Kusikiliza / Moja ya Kliniki ya Kisukari nchini Tanzania

Novemba 14 kila mwaka ni siku ya Kisukari duniani ambapo katika salamu zake kwa mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon  amehadharisha juu ya ongezeko la idadi ya wagonjwa hususan watoto, vijana na watu maskini. Amesema takribani watu Milioni 350 duniani waugua Kisukari na licha ya kwamba watu wako hatarini kurithi ugonjwa [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031