Nyumbani » 12/11/2013 Entries posted on “Novemba 12th, 2013”

Maji utapiamlo vyapata suluhu Ethiopia

Kusikiliza / Maji Ethiopia

Maji yamekuwa ni kitendawili ambacho hakina jibu nchiniEthiopiakwa muda mrefu hususani maeneo ya vijijini. Huduma ya lishe nayo si shwari. Katika jamii yenye changamotokamahizo maisha huwa kizungumkuti. Lakini waswahili alisema nyota njema huonekana asubuhi, na hiki ndicho kilichotokea hukoEthiopia. Kufahamu undani wa hatma ya huduma hizi, ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

12/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Nchi 14 zaungana na wenzao katika ujumbe wa Baraza la Haki za Binadamu

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu John Ashe

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo pamoja na majukumu mengine lilikuwa na kazi ya kuchagua wajumbe 14 wa Baraza la Haki za binadamu watakaohudumu kwa miaka mitatu kuanzia mwezi Januari mwakani. Uchaguzi huo umefanyika ili kuziba nafasi hizo zitakazoachwa wazi pindi nchi 14 zitakapomaliza ujumbe wao mwishoni mwa mwaka huu. Rais wa Baraza Kuu [...]

12/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Usimamizi mzuri unakwenda sambamba na uhamiaji mzuri

Kusikiliza / Msemaji wa IOM, Jumbe Omari Jumbe

Maafisa wa uhamiaji wa kutoka Sudan Kusini walisafiri hadi Tanzani kushiriki katika mafunzo yaliotolewa na Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM . Mafunzo hayo yalilenga kuwafunza kuhusu njia bora za kudhibiti mipaka na pia kuwakutanisha na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania. Assumpta Massoi wa Idhaa hii aliongea na msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe ambaye [...]

12/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya watoto syria yalaaniwa

Kusikiliza / Nembo ya UNICEF

Mauaji ya watoto wasio na hatia yameendelea nchini Syria ambapo tukio la hivi karibuni zaidi ni la vifo vya watoto watano walioripotiwa kuuwawa wakiwa darasani baada ya kombora kushambulia shule iitwayo St. John iliyoko Damascus. Katika tukio hilo watoto kumi na mmoja walijeruhiwa Katika tukio jingine siku hiyo hiyo watoto wanne pamoja na dereva mmoja [...]

12/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa AMISOM nchini Somalia

Kusikiliza / Mwakilishi wa kudumu wa Somalia, UM Balozi Dk. Elmi Ahmed Dual

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na vikao vya wazi na faragha vikimulika hali ilivyo nchini Somalia wakati huu ambapo serikali inajitahidi kuimarisha usalama ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Novemba Balozi Liu Ji Ye [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yafanikiwa kufikisha chakula Al Rastan Syria:

Kusikiliza / WFP yawasilisha chakula eneo la, Al Rastan Syria

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP Ijumaa lilifanikiwa kufikisha msafara uliosheheni msaada wa mashirika mbalimbali wa chakula katika eneo la Al Rastan jimbo la Homs nchini Syria. Msaada huo unagawanywa na chama cha msalaba mwekundu cha nchi hiyo . Msafara huo ulijumuisha malori 9 yaliyokuwa yamebeba vifurishu 5000 vya mgao wa chakula unaotosheleza kulisha [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yatoa ombi la dola milioni 24 kugharamia misaada nchini Ufilipino.

Kusikiliza / Kimbunga Haiyan kimeathiri kilimo

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linakusanya misaada kwa ajili ya waathiriwa wa kimbunga Hayian kilichoikumba Ufilipino na kusababisha uharibifu mkubwa kwa sekta nyingi ikiwemo ya kilimo ambapo pia watu wengi walipoteza maisha. Mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva amesema kuwa shirika hilo limesimama na kuonyesha uzalendo kwa watu [...]

12/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Pneumonia wangoza kwa vifo miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano duniani

Kusikiliza / Mtoto apokea chanjo dhidi ya uginjwa wa Pneumonia,malawi

Ugonjwa wa Pneumonia unaongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano duniani ambapo husababisha zaidi ya vifo milioni moja kila mwaka. Lakini hata hivyo vifo hivyo vinaweza kuzuiwa. Taarifa kamili na Flora Nducha (Taarifa ya Flora Nducha)  Huku nchi zikiadhimisha siku ya ugonjwa wa Pneumonia duniani hii leo muungano [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watoa ombi la dola milioni 300 kuwasaidia waathiriwa wa kimbunga Ufilipino

Kusikiliza / Madhara ya kimbunga Haiyan

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola milioni 301 zinakazotumika kufadhili misaada ya kibinadamu kwenye maeneo yaliyokumbwa na kimbunga nchini Ufilipino. Karibu watu milioni 11 wameathiriwa na kimbunga hicho huku  watu 700,000 wakilazimika kuhama makwao. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya  Grace Kaneiya) Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye maeneo yaliyoathiriwa yanasema kuwa chakula, [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zambia yaingia kipindi muhimu katika vita dhidi ya Ukimwi

Kusikiliza / Ujumbe wa PCB wahudhuria mafunzo ya afya ya uzazi katika shuke ya msingi, Lusaka

Shirika la Umoja wa Mataifa linaohusika na mapambano dhidi ya Ukimwi, UNAIDS limesema Zambia iko katika hatua muhimu zaidi dhidi ya ugonjwa huo ambapo limesema nchi hiyo haipaswi kubweteka na mafanikio ilipata. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Jan Beagle amesema hayo mwishoni mwa ziara ya siku tatu ya ujumbe alioongoza kwenye nchi hiyo ambako takribani [...]

12/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maafisa wa Sudan Kusini wajifunza masuala ya uhamiaji nchini Tanzania:IOM

Kusikiliza / Maafisa wa Uhamiaji kutoka Sudan Kusini wakiwa na wenzao kutoka Tanzania

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha mafunzo ya siku sita yaliyowaleta maafisa wa uhamiaji kutoka Sudan Kusini hadi nchini Tanzania kujifunza kuhusu njia bora za kudhibiti mipaka na pia kukutana na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania. Wawakilishi sita kutoka serikali ya Sudan Kusini idara ya uraia, pasi za kusafiria na uhamiaji (DNPI) akiwemo mkurugenzi [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaonya kuhusu athari na mahitaji ya kiafya Ufilipino

Kusikiliza / Waathirika wa kimbunga Haiyan (picha ya AP) W.Santana

Shirika la Afya Duniani WHO, limesema linapeleka wataalamu wa afya kwenye maeneo yaloathiriwa na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino ili kusaidia kurejesha huduma za afya. WHO imesema vituo vingi vya afya viliharibiwa kabisasa, na vile ambavyo vimesalia vimebanwa kwa mahitaji, huku uhaba wa vifaa vya afya ukishuhudiwa. Tayari matabibu kutoka Ubeljiji, Japan, Israel, na Norway wamepelekwa [...]

12/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Takribani wajawazito 200,000 wahitaji msaada Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan: UNFPA

Kusikiliza / Emily akifarijiwa na mumewe baada ya kujifungua salama

Madhara ya kimbunga Haiyan nchini Ufilipino yanazidi kuwa dhahiri shairi kila uchao ambapo Shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA limemulika afya ya uzazi ikisema wajawazito Laki mbili wanahitaji msaada wa haraka baada ya kuathirika na kimbunga hicho. Taarifa ya shirika hilo limetolea mfano mjamzito mmoja huko Tacloban City ambaye alilazimika kujifungulia [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031