Nyumbani » 08/11/2013 Entries posted on “Novemba 8th, 2013”

Usafirishaji wa fedha Somalia wahofiwa kuwezesha uharamia

Kusikiliza / Mogadishu

Taifa la Somalia likiwa linapiga hatua za kukuza uchumi wake baada ya takribani miongo miwili ya vita, uharamia nao ni changamoto kubwa inayoikabili nchi hiyo. Joseph Msami anaangazia utumaji wa fedha na athari zake katika uharamia nchini humo. Ungana naye katika makala ifuatayo.

08/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Botswana na Rwanda zatoa msukumo wa kufanyia marekebisho Baraza la Usalama

Kusikiliza / Charles Thembani Ntwaagae, Mwakilishi wa kudumu Botswana

Mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Baraza la Usalama umeingia siku yake ya pili, hukuRwanda na Botswana zikiongeza sauti zao kwa wito wa kutaka Baraza la Usalama lifanyiwe marekebisho. Akiongea wakati wa mjadala huo, Mwakilishi wa Kudumu wa Botswanakwenye Umoja wa Mataifa, Charles Thembani Ntwaagae amesema ujumbe waBotswanaunaazizia mno suala la kulifanyia [...]

08/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wa Utalii wataka uboreshaji wa sera kati ya utalii na usafiri wa angani

Kusikiliza / Utalii

Mawaziri wa Utalii kutoka kote duniani wametaka uboreshwe utandawazi wa angani kwa kuweka uratibu mzuri wa sera za utalii na usafiri wa angani ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa sekta hizo za utalii na usafiri wa angani. Hayo yamejitokeza katika mkutano wa kila mwaka wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, WTO na Shirika [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wasikatishwe tamaa; washirikisheni kwenye utunzi wa sera: Birungi

Kusikiliza / vijana wajasiriamali

Baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa na kamati ya fedha na uchumi ya Baraza Kuu la umoja huo kwa pamoja wameendesha mkutano kuhusu hatma ya ajira duniani na fursa mwaka 2030 ambapo miongoni mwa mambo yaliyomulikwa ni mustakhabali wa ajira kwa vijana wakati huu ambapo kuna kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia. [...]

08/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bi Ameerah Haqm azuru jimbo la Unity Sudan Kusini

Kusikiliza / Ameerah Haqm

Mkuu wa idara inayohusika na maslahi ya walinzi wa amani na wahudumu wa kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Ameerah Haqm amefanya ziara kwenye jimbo la Unity, Sudan Kusini kufanya tathmini ya ujumla ya hali ya mambo. Akiwa katika jimbo hilo, Bi Haqm amekutana na kupewa maelezo na wawakilishi wa serikali kuhusu marekebisho ya katiba, upokonyaji [...]

08/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Suala la vyoo bora lasalia utata duniani, huko Ruvuma Tanzania baadhi wachukua hatua

Kusikiliza / world_toilet_day

Tarehe 17 Novemba imetengwa kuanzia mwaka huu kuwa siku ya choo duniani. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha uamuzi huo mwezi Julai mwaka huu. Sababu hasa ni kuhakikisha suala la usafi wa vyoo na mazingira linapatiwa kipaumbele kwenye ajenda ya maendeleo endelevu. Umoja wa Mataifa unasema cha kustaajabisha ni kwamba dunia ina watu zaidi [...]

08/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watoto Mashariki ya Kati kupewa chanjo dhidi ya polio

Kusikiliza / mtoto apokea chanjo

Zaidi ya watoto milioni 20 katika nchi saba na maeneo ya Mashariki ya Kati wanapewa chanjo dhidi ya polio, kufuatia kulipuka kwa ugonjwa huo wa kupooza nchini Syria. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Shirika la Afya Duniani, WHO na lile la Kuhudumia Watoto, UNICEF yanaongoza kampeni hiyo ya utoaji wa chanjo. [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufisadi upigwe vita mitaani hadi vyumba vya mikutano: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon ataka ufisadi ukomeshwe

Transparency International, taasisi ya kimataifa inayotetea uwazi imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameitumia pongezi akisema kupitia ubia wake na taasisi nyingine ukiwemo Umoja huo limesaidia kusongesha vita dhidi ya ufisadi kwenye nchi tajiri na maskini. Salamu za Ban zimesema ufisadi hauipaswi kugharimu biashara, bali ni [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ghasia nchini Jamhuri ya Afika ya kati huenda zikafikia hali isiyoweza kudhibitika:PILLAY

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameonya kuwa uvamizi na ghasia zinazoendelea kushuhudiwa kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati huenda ikalitumbukiza taifa hilo kwenye mzozo mpya . Jason Nyakundi na taarifa kamili. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)  Mnamo tarehe 26 mwezi Oktoba wanamgambo wanaofahamika kama anti-Balaka walivamia na kuteka mji [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati wa kuchukua hatua ni sasa asema Ban akihitimisha ziara Sahel:

Kusikiliza / Katibu Mkuu zairani Ukanda wa Sahel, akiondoka Mali

Umewadia wakati wa kuachana na maneno na kuanza kutekeleza kwa vitendo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaambia maafisa wa serikali ya Chad mjini N’Djamena alipokuwa akihitimisha ziara yake katika ukanda wa Sahel kwa mujibu wa André-Michel Essoungou, afisa wa Umoja wa mataifa anayesafiri pamoja na Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Bwana Ban amepokea ushirikiano mkubwa [...]

08/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wafanyika Hoima, Uganda kuweka mazingira bora kwa wakimbizi: UNHCR

Kusikiliza / Wakati wa mkutano uliofanyika Hoima, Uganada

Hatimaye Shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia wakimbizi la (UNHCR) eneo la magharibi ya kati mwa Uganda, limefanikisha mkutano wa wa wakimbizi wapya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) uliokuwa na lengo la kuleta mshikamano zaidi kati ya serikali ya Uganda, shirika hilo na mashirika mengine ili wakimbizi wapate huduma bora licha ya idadi [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mvua kubwa zilizoikumba Cambodia zaanza kumalizika

Kusikiliza / Mfanayakazi wa IOM, Cambodia

Wakati maji yaliyojaa katika majimbo mengi yameaanza kutoweka na msimu wa mvua kuelekea kumalizika, mafuriko mabaya kabisa yaliyoathiri Cambodia tangu mwezi septemba yanaonekana kumalizika limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Kwa mujibu wa shirika hilo mvua kubwa zilisababisha mto Mekong kufurika na kuwaathiri watu zaidi ya milioni 1.7, vikiwemo vifo 188 katika majimbo 20 [...]

08/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kimbunga Haiya chapiga Ufilipino UM wasaidia:WMO/OCHA

Kusikiliza / Kimbunga

Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO linasema kimbunga Haiyan kimepiga Ufilipino na kuelezwa kuwa  ni kikubwa na cha kasi sana, na tayari kimeshasababisha uharibifu mkubwa. Assumpta Massoi na ripoti kamili. Kimbunga hicho kinavuma kwa kasi ya kilometa 215 kwa saa na kimeambatana na mvua kubwa. Umoja wa Mataifa unaisaidia serikali ya Ufilipino [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu imekaribisha kupiga mweleka kwa kundi la M23 DR Congo:

Kusikiliza / Kundi la waasi M23

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa Ijumaa imekaribisha kitendo cha kushindwa kwa kundi la waasi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa mujibu wa ofisi hiyo kiongozi wa kundi hilo Sultani Makenga ambaye alijisalimisha nchini Uganda ametajwa kuwa ni mmoja wa wakiukaji wakubwa wa haki za binadamu. Na ofisi hiyo [...]

08/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031