Nyumbani » 06/11/2013 Entries posted on “Novemba 6th, 2013”

Muswada wa haki ya faragha kuwasilishwa UM

Kusikiliza / INTERNET

Kutoheshimiwa kwa haki ya faragha ndiko kumetusukuma kupeleka muswada wa azimio hili, amesema Christian Doktor ambaye ni msemaji wa ubalozi wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa. Katika mahojiano na Monica Graylay wa idhaa ya Kireno ya Umoja wa Mataifa Bwana Christaian amesisistiza imani yake juu ya uungwaji mkono kwa azimio hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ujerumani [...]

06/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Majanga ya wahamiaji yanamulika haja kubadili sera: ILO

Kusikiliza / Walionusurika kifo mkasa wa Lampedusa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Ajira, ILO, Guy Ryder, ametoa wito wa kufanywa mabadiliko ya kina katika sera za uhamiaji ili kuepukana na majanga kama yale ambayo huwaua mamia ya wahamiaji wanapjaribu kufika ulaya, wengi wao wakitoka Afrika. Akizungumza wakati wa kongamano la siku tano la kujadili uhamiaji, likiwemo suala la haja ya [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutumie fursa ya yaliyojiri DR Congo kuleta amani ya kudumu: Baraza la Usalama

Kusikiliza / Balozi Atoki Ileka

Habari ni njema kutoka DR Congo ambako yathibitishwa kuwa waasi wa M23 wametangaza rasmi kusitisha uasi wao, na hizo ni miongoni mwa taarifa ambazo wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamepatiwa hii leo na Martin Kobler ambaye ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO na mjumbe maalum wa [...]

06/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Migogoro lazima itafutiwe ufumbuzi ukanda wa Sahel: Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa BanKi-moon ambaye yuko ziarani katika ukanda wa Sahel, hii leo amehutubia katika bunge nchini Niger na kulitaka taifa hilo kuungana na nchi nyingine za ukanda huo kutafuta suluhu za migogoro huku akipendekeza kile alichokiita ni muarubaini wa migogoro. Halikadhalika katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameliambia bunge la [...]

06/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Adha za mapigano zaendelea kuwatesa raia Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Wakimbizi CAR

Taarifa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaeleza kutoimarika kwa utulivu nchini humo ambapo hivi karibuni mapigano hayo yaliiubuka tena na kuzua hofu na mtafaruku kwa raia wa nchi hiyo ambao wamejikuta wakipoteza makazi. Ungana na Joseph Msami katika mkala ifuatayo inayoangazia adha wanazokumbana nazo wakimbizi wa ndani nchini humo.

06/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mijeledi na ukatili dhidi ya wanawake ikomeshwe: UM

Kusikiliza / Frances Raday, mtaalamu

Wataalamu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa wametaka kukomeshwa kwa ukatili dhidi ya wanawake hususani ni kuchapwa mijeledi, ikiwamo kwa tuhuma zinazoitwa za kimaadili na kutaka kuheshimwa kwa sheria za kimataifa. Onyo hili linakuja wakati huu ambapo mwanamke Amira Osman Hamed, ambaye ni mwanaharakati wa haki za wanawake na mhandisi amefikishwa mahakani nchini [...]

06/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuwawezesha wanawake kutunza maliasili ni muhimu katika amani endelevu:Ripoti UN

Kusikiliza / Mwanamke

Ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa njia bora ya kuziwezesha nchi zilizokumbwa na mizozo ya kivita kurejea kwenye amani na kusonga mbele kimaendeleo ni kwanza kuwawezesha wanawake kupata fursa ya kumilika rasilimali ikiwemo ardhi, maji,misitu na madini. Ripoti hiyo imebainisha nchi ambazo zimetumbukia kwenye mizozo ya kivita wanawake ndiyo wanaochukua jukumu la [...]

06/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika yatakiwa kuimarisha mifumo ya kuwalinda watoto:UNICEF

Kusikiliza / Watoto, Afrika

Mashirika kumi na tatu yakiwamo ya  Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi barani Afrika yametoa wito kwa serikali barani humo kuimarisha mifumo ya ulinzi kwa watoto ili kuwalinda dhidi ya ukatili, unyanyasaji, kutelekezwa na unyonyaji katika mazingira ya dharura na yasiyo ya dharura.  (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Taarifa ya mashirika hayo ikiwamo lile la kuhudumia watoto [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchina yachangia dola milioni 2 kufadhili huduma za WFP Syria

Kusikiliza / Mfanyakazi wa WFP, Syria

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetoa mchango wa dola milioni mbili kwa ajili ya huduma za dharura za Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, ambalo sasa linawasaidia watu wapatao milioni nne ndani ya Syria waloathiriwa na mzozo. Mchango huo utaisaidia WFP kununua tani 2,000 za ngano, mafuta ya kupikia, na mchele, ambavyo [...]

06/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viwango vya gesi chavuzi angani vyavunja rekodi: WMO

Kusikiliza / Gesi chafuzi

Viwango vya gesi zinazochafua mazingira angani vilifikia rekodi mpya mwaka 2012 huku vikizidi kupanda hali ambayo imesababisha kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya hali ya hewa na kuibadilisha sayari ya dunia kwa maelfu ya miaka inayokuja. Alice Kariuki anaripoti. (Taarifa ya Alice) Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kupitia kwa makala yake ya [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Niger patieni kipaumbele maslahi ya wanawake na watoto wa kike: Ban

Kusikiliza / Wanawake, Nigeria

Ujumbe wa ngazi ya juu unaoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon huko Sahel umekuwepo Niger ambapo pamoja na mambo mengine umeangazia suala la kuwawezesha wanawake huku Benki ya dunia ikiongeza dau la usaidizi. Taarifa kamili na Joshua Mmali. (Ripoti ya Joshua) Siku ya tatu ziarani huko Ukanda wa Sahel, Bwana Ban [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhalifu wa kimazingira unaathiri usalama na maendeleo:UNEP/INTERPOL

Kusikiliza / Uwindaji haramu wa wanyama pori

Uhalifu dhidi ya mazingira unaoanzia biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori na mbao , biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la ozoni na uvuvi ulio haramu ni changamoto la kimataifa ambalo athari zake ni kubwa. Haya yote yamejadiliwa  kwenye mkutano uliondaliwa mjini Nairobi Kenya kati ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Virusi vingine vipya vya AH7N9 vyazuka Uchina:WHO

Kusikiliza / Vipimo vya H7N9

Kamishna ya afya ya uzazi wa mpango nchini China imeliarifu shirika la afya ulimwenguni WHO juu ya kubainika kwa watu wawili wapya ambao wamegundulika kukumbwa na virusi vya AH7N9 kufuatia uchunguzi wa kimaabara uliofanywa dhidi yao. George Njogopa na taarifa kamili  (TAARIFA YA GEOERGE NJOGOPA) Mgonjwa wa kwanza kugundulika kukumbwa na virusi hivyo ni mtoto [...]

06/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tuimarishe usimamizi wa maliasili kwenye maeneo ya mizozo: Ban

Kusikiliza / Mizozo Sierra Leone imeathiri maliasili,UNEP

Ulimwenguni kwa kiasi kikubwa kumesheheni taarifa juu ya umuhimu wa mazingira kwa maendeleo endelevu lakini wakati huo huo kiwango cha utumiaji hovyo wa maliasili kama vile misitu, wanyamapori, vyanzo vya maji na hata ardhi ya kilimo kinazidi kuongezeka. Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwenye salamu zake maalum kwa siku [...]

06/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031