Nyumbani » 05/11/2013 Entries posted on “Novemba 5th, 2013”

Mratibu Maalum wa UM-OPCW atoa taarifa kwa Baraza la Usalama

Kusikiliza / Sigrid Kaag

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepata taarifa ya Katibu Mkuu kuhusu Syria ambapo pamoja na mambo mengine inaelezea kazi ya uteketezaji wa mpango wa silaha za kemikali nchini Syria, kazi inayofanywa kwa pamoja na umoja huo na shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya silaha hizo, OPCW. Mara baada ya kupokea taarifa hiyo [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati za kuleta maridhiano Juba, Kusini mwa Somalia zaendelea

Kusikiliza / Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon akihutubia kwenye mkutano huo

Kundi la ngoma za kitamaduni likitumbuiza kwenye kusanyiko la viongozi wa serikali kuu, serikali ya mkoa na viongozi wa kidini na kikabila, mjini Mogadishu, Somalia, kubwa hapa ni mkutano wa maridhiano wa Juba, lengo ni kuongeza wigo wa uongozi wa serikali kuu kwenye eneo hilo na kudhibiti migongano baina ya koo.  Wajumbe wako makini kwenye [...]

05/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Møller wa Denmark mkuu wa ofisi ya UM Geneva

Kusikiliza / Michael Møller

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemteua Michael Møller wa Denmark kuwa kaimu mkuu wa ofisi ya umoja huo mjini Geneva Uswizi. Bwana Møller anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kassym-Jomart Tokayev ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa mchango wake katika kuongoza kazi za Umoja wa Mataifa mjini humo. Mteule huyo Bwana Møller ana [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tumeshindwa kupanga tarehe ya mkutano wa pili wa Geneva: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Matarajio ya kufanyika karibuni kwa mkutano wa pili wa Geneva kuhusu Syria hayakuweza kutimia hata baada ya msururu wa mikutano ya leo, amesema mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi mjini Geneva hii leo alipozungumza na waandishi wa habari. Bwana Brahimi katika mazungumzo ya pande tatu yakihusisha [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yawakwamua watoto waliosafirishwa Uganda

Kusikiliza / watoto

Shirika la Kimataifa la uhamiaji nchini Uganda IOM, limefanikiwa kuwarejesha katika sehemu zao za asili watoto 21 ambao walikumbwa na biashara haramu  ya usafirishaji wa binadamu. Kwa mujibu wa IOM zoezihiloambalo linaendeshwa kwa ushirikiano na serikali yaUgandahususani vyombo vya dola pia linahusisha mafunzo maalum kwa watoto hao kabla ya kuwarejesha nyumbani. Katika mahojiano na Joseoh [...]

05/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

IOM Uganda yafanikiwa kuwarejesha kwenye maeneo ya asili watoto waliorubuniwa

Kusikiliza / Jumbe Omari Jume

  Shirika la Kimataifa la uhamiaji nchini Uganda IOM, likishirikiana na serikali ya Uganda, limefanikiwa kuwarejesha katika sehemu zao za asili watoto 21 ambao walikumbwa na biashara ya usafirishaji watu. Idadi kubwa ya watoto hao wamekuwa wakisafirishwa kutoka eneo la Karamoja lililoko kaskazini mashariki mwa Uganda hadi mji mkuu wa Kampala na kutumikishwa kwenye shughuli [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wa kimataifa muhimu kukabili changamoto za Sahel: Ban

Kusikiliza / Mzozo wa Mali ulisababisha wengi kuhamia ukimbizini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wanaoambatana naye kwenye ziara huko ukanda wa Sahel akiwemo Rais wa Benki ya dunia, kamishina wa muungano wa afrika, kamishina wa maendeleo wa Muungano wa Ulaya na mwakilishi wa Katibu Mkuu kwa ushirikiano wa jumuiya ya nchi za Kiarabu [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wanaohitaji misaada nchini Syria yapanda hadi milioni 9.3: OCHA

Kusikiliza / Syria displaced

Idadi ya watu wanaohitaji misaada nchini Syria imeripotiwa kupanda hadi kufikia milioni 9.3 . Kulingana na takwimu mpya kati yao hao watu milioni 6.5 wamekosa makazi lakini bado wako nchini humo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Kiwango hicho ni tofauti na makadirio yaliyowekwa mwezi wa Juni, ambayo yalionyesha kuwa kingekuwa watu [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali inazidi kuwa mbaya Syria kila uchao: Mkuu wa OCHA

Kusikiliza / Raia wa Syria wakiandaa mlo ukimbizini

Naona hali inazidi kuwa mbaya kwa wananchi wa Syria iwapo suluhu la kisiasa halitapatikana, ni kauli ya Valerie Amos Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu aliyotoa wakati wa kikao kati yake na watendaji wa ofisi hiyo kutoka sehemu mbali mbali duniani. Kikao hicho kilifanyika New York na kuunganishwa na ofisi [...]

05/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baada ya boti kuzama huko Myanmar, makumi ya watu hawajulikani waliko: UNHCR

Kusikiliza / Kituo hiki cha Sittwe kinakisiwa kua ni maboti haramu yana ng'oa nanga

Huko Pwani ya Myanmar, majanga ya vifo vitokanavyo na safari za mashua yameendelea kuchukua kasi ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linataja Jumapili kuwa ni siku mbaya zaidi kwani makumi ya watu wakiwemo watoto na wanawake wanahofiwa kufariki dunia  baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kusaka maisha bora kuzama. Msemaji wa UNHCR [...]

05/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahofia hatma ya mkimbizi wa Rwanda Joel Mutabazi

Kusikiliza / Nembo ya UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR latiwa wasiwasi na hali ya Joel Mutabazi, mkimbizi wa Rwanda aliyekamatwa na kukabidhiwa kwa serikali ya nchi yake na polisi wa Uganda bila ridhaa yake mnamo Jumamosi ya oktoba 26 mwaka huu. Waziri wa Uganda anayehusika na masuala ya wakimbizi amethibitishwa kukamatwa na kukabidhiwa kwa mkimbizi huyo [...]

05/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tunalaani vikali shambulizi kwa msafara wa harusi Nigeria: UN OHCHR

Kusikiliza / Cécile Pouilly,msemaji wa OHCHR

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali shambulizi  dhidi ya msafara wa harusi lilitokea kwenye jimbo la Borno nchini Nigeria mwishoni mwa wiki. Mnamo tarehe 2 mwezi huu watu 30 waliokuwa wakihudhuria harusi walitekwa na kuawa kwenye barabara ya Bama-Mubi-Banki  jimbo la Borno. Barabara hiyo iko karibu na mapaka na Cameroon [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malefu ya raia wa DRC waingia Uganda wakikimbia oparesheni dhidi ya kundi la M23

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka DRC waendelea kumiminika Uganda

Zaidi  ya watu 10,000 wamekimbia maeneo yaliyo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DCR kwenda nchini Uganda kufuatia mapigano  kati ya wanajeshi wa serikali na wanachama wa kundi la M23 kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.  (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Wanaohama makwao wanaingia [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yahaidi kuwapiga jeki wakulima waliokumbwa na mafuriko Benin

Kusikiliza / José Graziano da Silva

Shirika la chakula na kilimo FAO limewapiga jeki wakulima waliopoteza mazao yao kaskazini mwa Benin wakati mto kingo cha mto Niger zilipopasuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa mashamba na mifugo. Hali hiyo iliyojitokeza mwezi Agust mwaka huu ilikuwa kama vile kutonesha kidonda kwa wakulima hao ambao walikuwa wakianza kupata afuheni kutokana na mafuriko yaliyowakumba msimu [...]

05/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa umejizatiti kusaidia Mali: Ban

Kusikiliza / Watoto wa Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wanaoambatana naye kwenye ziara huko ukanda wa Sahel wamekuwa na mazungumzo na Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali mjini Bamako kando ya mwa mkutano wa kikanda wa mawaziri unaofanyika mjini humo. Katika mazungumzo yao Bwana Ban amerejelea mshikamano wake [...]

05/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031