Nyumbani » 01/11/2013 Entries posted on “Novemba 1st, 2013”

Faraja yatanda DRC kufuatia kujisalimisha kwa M23

Kusikiliza / Martin Kobler akiwa DRC

Taarifa kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC zinasema vikosi vya waasi wa M23 wanaripotiwa kujisalimisha kwa jeshi la serkali linaloendesha mapambano kwa kushirikiana na kikosi cha kuweka utulivu cha Umoja wa Mataifa MONUSCO. Hatua hii imekuwa faraja kubwa kwa wanachi wa eneo hili kama anavyosimulia Joseph Msami katika makala ifuatayo.

01/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Hali Mashariki mwa DRC imedhibitiwa lakini bado kuna makundi ya waasi: MONUSCO

Kusikiliza / Walinda amani wa MONUSCO wapiga doria,DRC

Hali katika Kivu ya Kaskazini imedhibitiwa sasa, ingawa kundi la waasi wa M23 bado lina himaya katika miji miwili midogo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Hayo yamesemwa na Jenerali Santos Cruz, kamanda wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuweka utulivu katika DRC, MONUSCO. Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa, Jenerali [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kujiamini na kuchukua hatua stahili mapema siri ya mafanikio: Samson Gachia

Kusikiliza / expo

Hatimaye maonyesho ya wiki moja ya miradi bunifu isiyo na madhara kwa mazingifa yamefikia ukingoni  hukoNairobiKenyaambapo imeelezwa kuwa miradi yenye thamani ya dola Miliono 450 za kimarekani imewekewa ahadi kati ya wawekezaji na serikali, vikundi mbali mbali, miradi ambayo ikitekelezwa italeta fursa ya ajira, itainua uchumi huku ikijali mazingira. Maonyesho hayo yalishuhudia utoaji tuzo kwa [...]

01/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mimba za utotoni zaangaziwa Tanzania

Kusikiliza / Mama na mwanawe (picha ya UNFPA)

Mapema wiki hii shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA lilitoa ripoti yake kuhusu idadi ya watu ikiangazia zaidi mimba za utotoni. La kustaajabisha ni kwamba takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka, watoto milioni 7.3 wa kike chini ya umri wa miaka 18 hupata ujauzito na kwamba Milioni Mbili katiyaowana umri usozidi miaka 14. Nchini Tanzania [...]

01/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Maonyesho ya nchi za Kusini yakamilika Nairobi

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu John Ashe na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Achim Steiner, Nairobi Kenya

Maonyesho ya wiki moja ya miradi na mbinu za maendeleo zinazojali mazingira yaliokuwa yakifanyika mjini Nairobi, Kenya yakihusisha nchi zinazoendelea yamefungwa hii leo . Maonyesho hayo yaliandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia ushirikiano wa nchi zinazoendelea, SOUTH-SOUTH. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Maonyesho hayo yaliwaleta pamoja zaidi ya wajumbe 800 [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutumie fursa iliyopo kutatua mzozo huko Sahel: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon akizungumza kwenye mkutano ambao Rais wa Benki ya dunia alihutubia kwa njia ya video

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Rais wa Benki ya dunia, Jim Yong Kim wiki ijayo wataanza ziara kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika ambapo watafanya ziara huko Mali, Niger, Burkina Faso na Chad.  Akitangaza ziara hiyo kwa waandishi wa habari mjiniNew York siku ya Ijumaa, Ban amesema ziara hiyo kwenye eneo [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS yaonya kuhusu mzigo wa HIV uzeeni

Kusikiliza / Dokta Stephen Watiti ambaye ana umri wa miaka 60 amekuwa akiishi na virusi vya HIV kwa miaka 25

Visa vya HIV na UKIMWI miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 50 na zaidi vinazidi kuongezeka kote duniani, kulingana na utafiti mpya ulofanywa na Shirika linalohusika na HIV na UKIMWI katika Umoja wa Mataifa, UNAIDS. Taarifa kamili na Alice Kariuki (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Utafiti huo umebinisha kuwa, watu milioni 3.6 wenye umri zaidi [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshikamano wa kimataifa uwe kitovu cha ajenda ya baada ya 2015: Mtaalamu

Kusikiliza / Virginia Dandan, mtaalamu huru

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na mshikamano wa kimataifa Virginia Dandan, ametaka nchi wanachama wa Umoja huo kuweka mbele mshikamano wa kimataifa kama msingi wa mafanikio ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Katika ripoti yake kwa Baraza la Kuu mjini New York, Dandan amesema kupitia mshikamano wa kimataifa [...]

01/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nuru yaonekana kuelekea mkutano wa pili wa Geneva kuhusu Syria: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Nchini Syria matumaini ya kupatia suluhu ya amani mzozo unaoendelea yanaanza kuonekana kufuatia ziara ya mjumbe wa pamoja wa Umoja wa mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi kwenye ukanda huo. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Ripoti ya Assumpta) Ziara ya Brahimi huko Mashariki ya Kati ilianza mwishoni mwa wiki ambapo nchi alizopita [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali bado ni tete Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Ghasia zaendelea kushuhudiwa CAR (picha ya UNHCR)

Kiasi cha raia milioni 1.1 katika Jamhuri ya Kati ikiwemo asilimia 50 ya raia waliokosa makazi kutokana na machafuko yanayoendelea wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula. Wengi waliokimbia makazi yaowanadaiwa kujificha msituni kwa hofu ya kushambuliwa. Mahitaji ya misaada ya kibinadamu yameongezeka katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni kutokana na kuzuka upya kwa [...]

01/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Angola waliokuwa Botswana warejea makwao

Kusikiliza / Wakimbizi wa Angola wakiwasili eneo la Katwitwi Angola kusini kutoka Botswana

Kundi la mwisho la wakimbizi wa Angola nchini Botswana limeondoka jana hii ikiashiria kufungwa rasmi kwa kambi hiyo kongwe barani Afrika.Kundi la wakimbizi hao ambao walikuwa wakiishi katika kambi ya Dukwi waliwasili jana mchana katika eneo la Mashariki mwa Angola wakiwa na mafurushi yao. Taarifa na George Njogopa (Taarifa ya George) Shirika la Umoja wa [...]

01/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yaendesha tathimini kuwasaidia wakimbizi wa DRC

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe mseamaji wa IOM

Wakati kukiwa na taarifa ya waasi wa kundi la M23 wanaopambana na jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kwa usaidizi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kuweka utulivu nchini humo MONUSCO kujisalimisha, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linafanya tathimini ya namna ya kuwasaidia wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msimu wa safari za mashua huko pwani ya Bengali zatia hofu UNHCR

Kusikiliza / Mashua hizi za uvuvi hutumika kwa safari

Katika siku za karibuni shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepokea taarifa za kutia hofu kwamba watu zaidi wanaondoka kwa kusafirishwa katika boti haramu kwenye Pwani ya Bengali, hali ambayo inaashiria kuanza kwa msimu wa kila mwaka wa safari za meli wakati ambao maelfu ya watu kutoka jimbo la Rakhine huko Myanmar wanahatarisha [...]

01/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031