Nyumbani » 29/11/2013 Entries posted on “Novemba, 2013”

Ban akaribisha tamko la baraza la usalama kuhusu Yemen

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tamko la baraza la usalama la tarehe 27 November ambalo limeahidi kusaidia katika mchakato wa amani wa mpito nchiniYemen ikiwamo kongamano la mjadala wa kitaifa. Katibu Mkuu amesema baraza hilo linaendelea kusikitishwa na kuingiliwa au kucheleweshwa machakato wa mpito na kwamba baraza hilo liko tayari kuzingatia [...]

29/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umuhimu wa televisheni ni zaidi ya kuhabarisha nchini Burundi

Kusikiliza / Televisheni

Televisheni au kwingineko ikijulikana kama Runinga imeleta mabadiliko makubwa katika mtazamo wa vipindi hususan kwenye nchi ambazo awali radio ilikuwa imeshika kasi. Televisheni ina umuhimu wake katika kuhabarisha, kuelimisha na hata kuburudisha na ndio maana tarehe 21 ya mwezi Novemba imetengwa kuwa siku ya televisheni duniani. Hata hivyo maadhimisho ya nyakati hizo yanakuja na mengi [...]

29/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

MINUSMA yalaani ghasia huko Kidal nchini Mali

Kusikiliza / Moja ya vituo vya ukaguzi huko Kidal nchini Mali

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchiniMali, MINUSMA umeshutumu vikali ghasia za karibuni huko Kidal kaskazini mwa nchi hiyo na kutaka pande zote husika kujizuia. Ghasia hizo za Alhamisi zimetokea licha ya mpango wa ulinzi wa ujulikanao kama Serval ambao unaratibiwa kwa pamoja na serikali ya Mali na MINUSMA kwa  usaidizi wa Ufaransa. [...]

29/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama bado ni tete CAR; Mia Farrow ashuhudia

Kusikiliza / Mia Farrow akizungumza na wakazi wa CAR wakiwemo watoto

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, hali ya usalama inazorota lakini juhudi za Umoja wa Mataifa zinaendelea ili kusaidia waathirika wa mgogoro unaondelea nchini humo. Juhudi za hivi karibuni zaidi ni ziara ya balozi mwema wa shirika la Umoja UNICEF Mia Farrow aliyefika CAR kuanagalia athari za mgogoro. Ungana Na Joseph Msami katika makala [...]

29/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban aziomba nchi wanachama kuunga mkono watu wa Palestina

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameziomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono juhudi za utafutaji suluhu la mataifa mawili ili kuutokomeza mgogoro kati ya Israel na Palestina. Bwana Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa Siku ya Kimataifa ya kusimama bega kwa bega na watu wa Palestina, ambayo ni [...]

29/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Yemen yakiuka mkataba unaopiga marafuku silaha za ardhini

Kusikiliza / Utafiti wa silaha ardhini

Yemen imekiri kuwa imekwenda kinyume na mkataba wa kimataifa unaopiga marafuku matumizi, kuhifadhi na kuzalisha kwa silaha za ardhini. Kampeni ya kimataifa inayopiga marafuku silaha za ardhini imesema kuwa iliitaka serikali ya Yemen kuondosha maelfu ya silaha mwaka 2011 katika baadhi ya sehemu mbili. Kujitokeza kwa machafuko ya kiraia katika miaka ya hivi karibuni ni [...]

29/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM kuchunguza hali ya watu wenye asili ya Afrika Brazil

Kusikiliza / Watu wenye asili ya Afrika Brazil

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye asili ya Afrika litafanya ziara ya siku kumi nchini Brazil, kuanzia Disema 3 hadi 13 2013, ili kuchunguza masuala kadhaa yanayohusu haki za binadamu za watu wenye asili ya Afrika nchini humo. Mmoja wa wataalamu hao, Mireille Fanon-Mendes-France amesema kuwa Brazil imepiga hatua nyingi katika [...]

29/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yazindua ushirika wa kulinda haki za watoto

Kusikiliza / Watoto wakiwa darasani kwenye shule moja huko Juba, Sudan Kusini

Shirika la Kuhudumia watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeipongeza serikali ya Sudan Kusini kwa kuanzisha shirikisho la wadau wa kulinda haki za watoto walio hatarini, ambalo ni la kwanza la aina yake nchini humo. Mwakilishi wa UNICEF nchini humo, Iyorlumun Uhaa, amesema kuwa watoto maskini zaidi na walio wanyonge zaidi katika nchi yoyote ile huwa [...]

29/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Virusi vya MERS Corona vyabainika kwa ngamia Qatar:WHO

Kusikiliza / Ngamia waripotiwa kuwa na virusi vya MERS Corona huko Qatar

Shirika la afya duniani WHO litatoa ripoti ya uchunguzi kutoka Qatar inayoashiria kuwepo kwa virusi vya MERS Corona miongoni mwa ngamia. Shirika hilo linasema hii ni mara ya kwanza ngamia kuambukizwa virusi vya corona nchini humo lakini njia ya kuambukizwa kwao bado ni kitendawili. Matokeo ya utafiti huo kwa mujibu wa WHO yanatoa mwangaza wa [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wakimbizi kutoka Syria wanabiliwa na wakati mgumu siku za baadaye: UNHCR

Kusikiliza / Watoto wa Syria

Watoto wa wakimbizi walio nchini Lebanon na Jordan wanakabiliwa na wakati mgumu siku za baadaye huku wakiwa wanalazimika kufanya kazi kutafutia familia zao au wakiwa wanalazimishwa kujiunga na makundi yaliyojihami kwa mujibu wa  shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa. Utafiti uliofanywa kwa watoto wa wakimbizi wa Syria kwenye nchi za Lebanon na Jordan [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yazidi kutekeleza hukumu ya kifo hata baada ya kutia sahihi makubaliano ya UM

Kusikiliza / Hukumu ya kifo bado inatekelezwa Sudan Kusini

Ofisi ya haki za bindamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa watu wanne wamenyongwa nchini Sudan Kusini huku wengine 200 wakiwa kwenye  orodha ya kusubiri kunyongwa. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Kulingana na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ni kuwa idara ya mahakama nchini Sudan Kusini inakabiliwa [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya walioathirika na kimbunga Haiyan sasa ni zaidi ya milioni 14:OCHA

Kusikiliza / Athari za Kimbunga Haiyan, Ufilipino

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA linasema kuwa idadi ya watu walioathirika na kimbuka Haiyan nchini Ufilipino imezidi kupindukia. Kwa mujibu wa OCHA, zaidi ya watu milioni 14.4 wameathiriwa na kimbunga hicho ambapo kati yao, milioni 3.62 wamekosa makazi, milioni 1.1 nyumba zao zimebomolewa na vifo vilivyoripotiwa hadi sasa vimefikia [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizi mapya ya Ukimwi yapungua: UNAIDS

Kusikiliza / Moja kliniki za kutoa huduma dhidi ya Ukimwi kwa mama na mtoto nchini Lesotho

Wakati dunia inaelekea kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani tarehe Mosi Disemba, habari njema ni kwamba idadi ya maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha Ukimwi imepungua. Taarifa hizo zimo kwenye ujumbe wa siku hiyo uliotolewa na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na vita dhidi ya Ukimwi, UNAIDS Michel Sidibé. Katika ujumbe huo wa [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifo vya raia wa Haiti katika pwani ya Bahamas vitupe funzo:IOM

Kusikiliza / Nembo ya IOM

Vifo vya wazamiaji 30 wa Haiti waliokumbwa na umauti wakati wakiwa safarini katika ufukwe wa Bahama mapema wiki hii kumezidi kuongeza hali ya wasiwasi kuhusiana na wimbi la wahamiaji haramu wanaokwenda katika nchi za mbali huku wakitumia mashua zisizo na usalama. Kwa mujibu wa shirika la kimataifa linalohusika na wahamiaji IOM, kuna hali ya kutia [...]

29/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP inaendelea kuongeza misaada CAR:

Kusikiliza / Chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaendelea kuongeza operesheni za kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati licha ya hali kuzidi kuwa mbaya.  Shirika hilo limeshasambaza msaada wa chakula kwa maelfu ya watu mjini Basonga lakini limesema watu takribani milioni 2.9 wanahitaji msaada wa kibinadamu nchini humo. Hivi karibuni tani 358 za chakula [...]

29/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba dola milioni 10 kuwarejesha Wasouth Sudan kwao

Kusikiliza / WaSudan Kusini warejeshwa nyumbani na IOM

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM linaomba dola milioni 10.5 ili liweze kutoa msaada wa dharura wa kuwarejesha watu wasiojiweza wa Sudan Kusini kwao. Watu hao wamekwama mjini Khartoum Sudan kwa muda sasa. IOM inasema watu hao hawana uwezo na njia yoyote ya kuwarejesha nyumbani Sudan Kusini. Shirika hilo limeongeza kuwa watu hao wamekuwa wakiishi [...]

29/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lalaani vikali shambulio dhidi ya ubalozi wa Urusi Damascus:

Kusikiliza / Baraza la usalama

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamesikitishwa na kulaani vikali shambulio la magruneti dhidi ya ubalozi wa Urusi mjini Damascus Syria siku ya Alhamisi. Shambulio hilo limekatili maisha ya mtu mmoja na kujeruhi wengine 9 wakiwemo walinzi wa ubalozi huo. Wajumbe hao wametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio [...]

29/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike wamulikwa Tanzania

Kusikiliza / Manusura wa ukatili, mjini Adama, Ethiopia

Kama sehemu ya maadhimisho ya siku kumi na sita za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike tunaangazia swala hili ambalo linahusisha vitendo kama vile vipigo majumbani, unyanyasaji sehemu za umma, shambulio la mwili, ukeketaji, mauaji na hata vitendo vinavyosababisha msongo wa mawazo. Basi ambatana na Tamimu Adamu na Enesi Mwaisakila wa Radio Washirika Jogoo FM [...]

28/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Twaunga mkono mchakato wa kisiasa Yemen, pande ziharakishe ukamilike: Baraza

Kusikiliza / Balozi Liu Jieyi

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wametoa ujumbe wa pamoja na ulio dhahiri ambao unaunga mkono mchakato wa kisiasa unaoendelea nchini Yemen pamoja na jitihada za serikali ya nchi hiyo za kujenga upya uchumi, kuimarisha usalama ikiwemo mjadala wa kitaifa. Msimamo huo umeelezwa kwa waandishi wa habari na Rais wa Baraza hilo [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na kusambaa kwa ghasia Misri

Kusikiliza / Ramana ya Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anasikitishwa na hatua ya kuwekwa vizuizini, na kusambaa kwa ghasia za waandamanaji nchini Misri ikiwamo taarifa za mashambulio ya kijinsia. Katika taarifa yake iliyotolewa mjini New York Bwana Ban amesisitiza umuhimu wa kuheshimu maaandamano ya amani na uhuru wa kukusanyika ikiwa ni pamoja na mazungumzo na [...]

27/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Masaibu ya wakimbizi wa Syria walioko Lebanon yaangaziwa

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria walioko Lebanon

Siku chache baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza tarehe 22 January mwakani ya kufanyika kwa mkutano wa pili wa amani kuhusu Syria huko Geneva, wakimbizi wa nchi hiyo walioko katika kambi nchini Lebanon wanaelezea madhila wanayokutana nayo. Hapa katika mji wa Arsal nchiniLebanonkuna foleni kubwa ya watu nje ya kituo cha usajili. Zaidi ya familia [...]

27/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban na Kim wazungumzia nishati endelevu

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim

Ilikufanikisha malengo ya nishati endelevu kwa wote ni muhimu kukuza uwekezaji mkuu na wa ziada amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Akiwa ameambatana na rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York kufuatia kikao cha ngazi ya juu cha bodi ya mpango wa nishati [...]

27/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wataka hatua zichukuliwe haraka baada ya ripoti za mauaji ya watoto Kinshasa :

Kusikiliza / Mama na mwanawe waliyefurushwa asimama katika kambi ya Mugunga picha ya MONUSCO

Umoja wa Mataifa leo umetoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchukua hatua haraka kufuatia ripoti za kusikitisha  za kupotea na kuuawa kwa watoto na vijana yaliyokwenda sanjari na operesheni ya serikali ya kukabiliana na uhalifu mjini Kinshasa. Kwa mujibu wa ripoti ambazo kwa sasa zinathibitishwa na watu 20 wakiwemo watoto 12 [...]

27/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM Yemen azuru Sa'ada:

Kusikiliza / Wakimbizi wa Yemen

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed, amezuru mji wa Sa'ada Kaskazini mwa Yemen na kukutana na gava, tume ya rais, tume ya bunge, viongozi wa eneo hilo na  wadau wengine wa misaada ya kibinadamu. Ziara yake imekuja wakati ambapo machafuko kwaskazini mwaYemenhususan Dammaj na Kitaf yameingia [...]

27/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serikali ziweke mipango ya maendeleo ya kupunguza majanga:ESCAP

Kusikiliza / Kimbunga Haiyan Ufilipino, mfano wa janga

Kujenga uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga katika eneo la Asia-Pacifiki ndio ajenda kuu kwenye mkutano wa siku tatu ulioanza Jumatano katika tume ya Umoja wa Mataifa ya kiuchumi na kijamii kwa nchi zaAsiana Pacific ESCAP.Taarifa ya Flora Nducha inaarifu  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)  Mkutano huo unaofanyika mjini Bangkok Thailand umewaleta pamoja maafisa wa serikali [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya jitihada China yahiizwa kuhifadhi mazingira:UNEP

Kusikiliza / Mazingira China

Licha ya juhudi za China za kukuza uchumi unaolinda na kuhifadhi mazingira taifa hilo bado linakabiliwa na changamoto za kimazingira na kijamii ambazo lazima zishughulikiwe iwapo nchi hiyo inalenga kwa dhati kutimiza malengo endelevu ya maendeleo. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa wiki hii na wizara ya uhifadhi wa mazingira nchini China, [...]

27/11/2013 | Jamii: Rio+20, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Global Fund yapigwa jeki kwa dola milioni 46 kupitia uuzaji wa mnada

Kusikiliza / Nembo ya Global Fund

Mfuko wa Global Fund kwa ajili ya kupambana na malaria, kifua kikuu na HIV umepigwa jeki kwa mchango wa dola milioni 46, zilizotokana na zoezi la uuzaji wa mnada lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Renew, Energize and Donate (RED), pamoja na michango mingine. Joshua Mmali na taarifa kamili.   (TAARIFA YA JOSHUA) Zoezi [...]

27/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yapitisha idadi ya wakimbizi wa Ivory Coast iliowarudisha nyumbani kutoka Liberia

Kusikiliza / Wakimbizi wa Ivory Coast wakielekea nyumbani kutoka Liberia

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR  Iemepitisha idadi ya wakimbizi  wa Ivory Coast lililowarudisha nyumbani kwa hiari kutoka  nchini Liberia ikiwa pia na mipango ya kuwarudisha  nyumbani wakimbizi zaidi kabla ya mwisho wa mwaka huu. Jason Nyakundi na ripoti kamili.(Taarifa ya Jason) Hadi mwishoni mwa juma lililopita UNHCR ilikuwa imewasaidai wakimbizi 16,232 [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa haraka wahitajika kwa wakulima Ufilipino: FAO

Kusikiliza / Moja ya shamba la kuku ambalo limesambaratishwa na kimbunga Haiyan

Kimbunga Haiyan kimesababisha madhara makubwa nchini Ufilipino lakini madhara hayo yanaweza kuwa maradufu zaidi kwa wakulima iwapo hatua hazitachukuliwa kuwapatia usaidizi wa kuwawezesha kuendelea na kilimo kwa ajili ya kujipatia kipato. Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO ambalo linatoa wito kwa mashirika ya utoaji misaada kuchukua hatua za haraka [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpatanishi wa Darfur akutana na rais wa Chad

Kusikiliza / Mohammed Ibn Chambas

Kiongozi wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa mzozo wa Darfur nchini Sudan Mohamed Ibn Chambas amekutana na Rais wa Chad Idriss Derby katika kile kinachoelezwa kwamba ni jaribio la kidiplomasia la kufanikisha mazungumzo ya amani ya Darfur. Msuluhishi huyo wa kimataifa anayeongoza UNAMID ametoa picha halisi ya usalama [...]

27/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mwongozo mpya wa kutibu watoto wenye unyafuzi

Kusikiliza / Mtoto akipimwa mzunguko wa mkono kufahamu iwapo na utapiamlo

Shirika la afya duniani, WHO leo limetoa mwongozo mpya wa tiba kwa watoto wenye unyafuzi au utapiamlo uliokithiri unaoripotiwa kuwa tatizo kubwa kwa watoto Milioni 20 duniani kote wenye umri wa chini  ya miaka mitano. George Njogopa na ripoti kamili. (Ripoti ya George) WHO inasema kuwa hali mbaya ya utapiamlo inajitokeza wakati ambapo mtoto anakuwa [...]

27/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lapitisha maazimio ya kuunga mkono Palestina na suala la Golan

Kusikiliza / Palestine

Wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo wamepiga kura kuhusu maazimio matano tofauti yanayounga mkono Palestina, pamoja na jingine kuhusu suala la eneo la Golan nchini Syria. Matukio hayo katika ukumbi wa Baraza Kuu yametokea siku chache kabla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kusimama bega kwa bega na watu wa Palestina, ambayo [...]

26/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lapongeza kazi ya kundi la kimataifa la usaidizi kwa Lebanon

Kusikiliza / Balozi Liu Jieyi

Baraza la usalama linapongeza jitihada za kundi la ngazi ya juu la kimataifa kwa usaidizi wa Lebanon lililozinduliwa tarehe 25 mwezi Septemba mwaka huu, ndivyo ilivyoanza kauli ya Rais wa Baraza hilo Balozi Liu Jieyi alipokutana na waandishi wa habari baada ya mashauriano ya baraza hilo leo mjini New York. Kundi analozungumzia linajumuisha Umoja wa [...]

26/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ICC yatengua uamuzi wake kuhusu Kenyatta kufika mahakamani

Kusikiliza / Uhuru Kenyatta

Majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague wanaohusika na kesi dhidi ya Rais waKenya, Uhuru Kenyatta leo wamebadili uamuzi wao ruhusa ya mshtakiwa kutokuwepo mahakamani mfululizo wakati kesi yake inaposikilizwa. Awali walikuwa wamemruhusu lakini baada ya rufani iliyowasilishwa na kutolewa ufafanuzi wa kisheria, hii leo, Jaji Eboe- Osuji amesema mshtakiwa atapaswa [...]

26/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maziwa na bidhaa za maziwa ni muhimu kwa lishe ya watu masikini:FAO

Kusikiliza / Maziwa

Shirika la mpango wa chakula duniani FAO linazitaka serikali kuhakikisha maziwa na bidhaa zake zinapatikana kwa familia za watu masikini kabisa duniani. Kwa mujibu wa ripoti yake ya karibuni maziwa na bidhaa za maziwa sio tuu zinaweza kuboresha lishe ya watu masikini bali pia zinaweza kuinua uchumi wa familia za wafugaji na wazalishaji wa bidhaa [...]

26/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA kuhifadhi kidigital kumbukumbu za wakimbizi wa Kipalestina

Kusikiliza / Mama na mtoto, UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limezindua sehemu ya kwanza ya mfumo mpya wa kumbukumbu kwa njia ya digital ambao unajumuisha zaidi ya nusu ya negative za picha, machapisho, slides, filamu na kaseti za video ambazo zinakumbukumbu za Nyanja zote za maisha na historia ya wakimbizi wa Kipalestina tangu [...]

26/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya chanjo kwa watoto yaanza huko Tacloban: WHO

Kusikiliza / Mtoto apewa chanjo

Nchini Ufilipino kampeni ya chanjo dhidi ya polio na surua imeanza kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano kwenye mji wa Tacloban ambao ulipigwa zaidi na kimbunga Haiyan . Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Kampeni hiyo inalenga kufikia zaidi ya watoto Elfu Thelathini na itahusisha pia utoaji wa matone [...]

26/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yafanya kampeni dhidi ya ukatili wa kingono kambi za wakimbizi Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi walioko Hoima, Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huko Hoima nchini Uganda limeanza kampeni ya siku kumi na sita za kupinga unyanyashaji wa kingono na mizozo ya kijinsia kwenye kambi za wakimbizi ya Kyangwali na Kiryandongo. John Kibego wa redio washirika ya Spice FM ana ripoti kamili kutoka Uganda.   (Tarifa ya John Kibego) Kampeni [...]

26/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za dharura zichukuliwe dhidi ya uhaba wa kawi Gaza:UM

Kusikiliza / Ukanda wa Gaza

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Richard Falk ametaka kuchukuliwa kwa hatua za dharura kukabilina na uhaba wa kawi kwenye utawala wa Palestina hali ambayo imewaacha watu milioni 1.7 kwenye  ukanda wa Gaza kwenye hali ya kutatanisha. Kwa kipindi cha majuma matatu sasa tangu kituo cha kuzalisha kawi kufungwa kutokana na uhaba wa mafuta masaa [...]

26/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sheria mpya ya maandamano Misri inahitaji mabadiliko: UM

Kusikiliza / Rupert Colville

Sheria mpya iliyobuniwa nchini Misri kwa lengo la kudhibiti maanadamno huenda ikawa yenye ukiukaji mkubwa wa haki  ya  kukusanyika kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Taaarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Sheria hiyo inazipa idara za usalama  uwezo wa kupiga marufuku mikutano  na kuwazuia waandamanaji  kutoka kwa  [...]

26/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yapatiwa Euro milioni 1.1 kutekeleza miradi Puntland

Kusikiliza / Biashara ya watu

Shirika la Kimataifa linalohisika na wahamiaji IOM, limepokea kiasi cha Euro milioni 1.1 kwa ajili ya kutekeleza mradi wake wa kukabiliana na wimbi la usafirishaji haramu watoto na unyanyasaji wa kijinsia huko Puntland, Somalia. Mpango huo ambao unaratibiwa kwa pamoja baina ya IOM na washirika  wake unalengo la kutoa elimu kwa wananchi na kuvijengea uwezo [...]

26/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waomba hifadhi kisiwa cha Pacific wanakabiliwa na mateso:UNHCR

Kusikiliza / Kituo cha kupumzika Nauru, cha waomba hifahdi, kulingana  na UNHCR hali sio nzuri(UNHCR)

Ripoti mbili zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR zimebaini kuwa mamia ya watu walioomba hifadhi nchini Australia na kisha kuhamishia katika visiwa vya Nauru na Manus vilivyoko huko Papua New Guinea wanaishi  katika maisha ya mateso na hali ya kukatisha tamaaa. Taarifa zadi na George Njogopa. (TAARIFA YA GEORGE) [...]

26/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kenya: Urejeshwaji wakimbizi wa Somalia utafanywa kwa hiari

Kusikiliza / Kambi ya Dadaab, nchini Kenya

Pande zilizohusika na makubaliano juu ya wakimbizi wa Somalia walioko nchini Kenya zimesisitiza hatua ya kuwarejesha wakimbizi hao katika maeneo yao ya asili itafanywa kwa kuzingatia hiari ya mtu. Katika taarifa yao ya pamoja, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR na serikali ya Kenya imeeleza kuwa hakuna mkimbizi atayelazimishwa kurejea nyumbani. UNHCR [...]

26/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Visa 17 vya polio vyabainika Syria:WHO/UNICEF

Kusikiliza / Maandalizi ya siku kutoa chanjo dhidi ya polio

Jumla ya visa 17 vya polio type 1 vimethibitishwa nchini Syria. Visa 15 vimebainika katika jimbo la Deir Al Zour na viwili  kimoja nje ya Damascus na kingine Aleppo, na hivyo kudhihirisha kwamba virusi hivyo vimesambaa. Hatua za kukabiliana na mlipuko huo katika kanda nzima zinaendelea kuchukuliwa limesema shirika la afya duniani WHO na lile [...]

26/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laanza harakati za kukabiliana na hali CAR

Kusikiliza / Jan Eliasson

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamefanya maziungumzo leo Jumatatu jioni na kukubaliana kuwa kuna haja ya kuanza harakati za kukabiliana na hali ya usalama inayozidi kuzorota katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao hicho ambacho baadaye kilifanywa faraghani, Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson amesema [...]

25/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunataka lengo mahsusi kwa wanawake kwenye ajenda endelevu: UNWomen

Kusikiliza / Phumzile Mlambo-Ngcuka, UN Women

Mkuu wa shirika la linalohusika na masuala ya wanawake kwenye Umoja wa Mataifa Phumzile Mlambo-Ngcuka ametaka kuwepo kwa lengo mahsusi kuhusu wanawake kwenye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 kama njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa masuala ya ulinzi na maendeleo kwa kundi hilo yanapatiwa mkazo.   Ametoa kauli hiyo mjini New York wakati wa [...]

25/11/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Tanzania yatekeleza mkakati maalum wa kupambana na ukatili wa kijinsia.

Kusikiliza /

  Wakati siku kumi na sita za kupinga ukatili dhodi ya wanawake na wasichana zimeanza leo, nchi mbalimbali zinatekeleza mkakati huo ikiwamo Tanzania. Nchi hiyo iliyoko mashariki mwa Afrika imeanzisha dawati maalum katika jeshi la polisi ili kushughulikia vitendo vya ukatili kwa kundi hilo.  Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa  idhaa hii kamanda wa [...]

25/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Athari ya taka ya mafuta yaangaziwa Uganda

Kusikiliza / Wavuvi waanda boti, Ziwa Albert, Uganda

Serikali ya Uganda ilitangaza ugunduzi wa mapipa bilioni 3.5 ya mafuta chini ya bonde la ufa la Ziwa Albert . Utafutaji wa mafuta unaendelea wakati moja na mandalizi ya kwanza kuyazalisha. Wanamazingira wanaonya kuwa uvuvi utaathiriwa kwa sababu wanaona serikali haijajiandaa kukabiliana na athari za mafuta kwa mazingira. (MAKALA YA JOHN KIBEGO RADIO WASHIRIKA SPICE [...]

25/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lalaani shambulio dhidi ya UNAMID

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID wakiwa kwenye doria

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali shambulio la Jumapili dhidi ya walinda amani wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika waliokuwa doria huko Kabkabiya, Darfur, UNAMID, shambulio ambalo limesababisha kifo cha mlinda amani kutokaRwanda. Rais wa baraza hilo Balozi Liu Jieyi amewaambia waandishi wa habari kuwa wajumbe wametuma risala [...]

25/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Syria unachangia kuzorota zaidi hali ya usalama Iraq: Mladenov

Kusikiliza / Baraza la Usalama(picha ya faili)

Wakati wakijitahidi kujenga taifa la kidemokrasia, kwa misingi ya utaratibu wa kisheria na ulinzi wa haki za binadamu, watu wa Iraq wanaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi, amesema Mwakilishi wa Katibu Mkuu, na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNAMI, Nikoali Mladenov, wakati akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.   Bwana [...]

25/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na shambulio lingine Darfur

Kusikiliza / Walinda amani, UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amesikitishwa sana kubaini kulikuwa na shmabulio lingine lililofanywa na mtu mwenye silaha dhidi ya msafara wa vikosi vya pamoja vya kulinda amani Darfur vya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID karibu na Kabkabiya Darfur Kaskazini. Katika shambulio hilo mlinda amani mmoja kutoka Rwanda ameuawa. [...]

25/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya visa 4,000 vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana vyaripotiwa Afghanistan:

Kusikiliza / Wanawake , Afghanistan picha ya UNAMA

Zaidi ya visa 4000 vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana vimeripotiwa katika wizara ya wanawake ya Afghanistan kutoka majimbo 33 kwa mwaka 2010-2012 umesema mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo UNAMA. UNAMA inasema hatua za kutokomeza vitendo hivyo vya kikatili, vitisho na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutawawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato [...]

25/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waitaka Malaysia kuondosha marufuku ya matumizi ya neno 'Allah'

Kusikiliza / Heiner Bielefeldt

Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Malaysia kuheshimu na kuzingatia misingi ya kidini ambayo pia inahimiza uhuru wa kuabudu kwa raia. Wito huo umekuja kufuatana na hatua ya Malaysia kupiga marafuku waumini wa Katoliki kutumia jina la "Allah" wakimaanisha "Mungu " wakati wakiendesha ibada zao. Mjumbe huru wa Umoja wa Mataifa juu ya uhuru wa [...]

25/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bado tunajadili orodha rasmi ya washiriki:Brahimi

Kusikiliza / Jeffrey Feltman, Mkuu wa masuala ya Siasa ndani ya Umoja wa Mataifa akiwa na Lakhdar Brahimi mjini Geneva

Baada ya kutangazwa kuwa tarehe 22 ya mwezi Januari mwakani ni siku ya kufanyika kwa mkutano wa pili wa amani kuhusu Syria huko Geneva, mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu juu ya mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi amesema wanachofanya sasa ni kujadili orodha kamili  ya washiriki. Amewaambia waandishi wa habari [...]

25/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vijana barubaru hawapati huduma wanazohitaji dhidi ya Ukimwi:WHO

Kusikiliza / mozambican-girl

Zaidi ya vijana milioni mbili walio kati ya umri wa miaka 10 na 19 wanaoishi na virusi vya ugonjwa wa ukimwi hawapati usaidizi wanaohitaji kuwawezesha kuwa na afya na katika kuzuia maambukizi mapya kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) WHO inasema kuwa kushindwa kuwapa [...]

25/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lamulika LRA

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama wakinyoosha mkono kupiga kura

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limelaani vikali vitendo vya mashambulizi na uhalifu wa kivita vinavyotekelezwa na waasi wa Lord's Resistance Army, LRA, pamoja na kupitisha azimio la kuongeza muda wa kuhudumu kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kuweka utulivu Abyei. Joshua Mmali na taarifa kamili. (Taarifa ya Joshua) [...]

25/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wanawake ni moja ya ukiukwaji mkubwa wa haki a binadamu: Rais wa Baraza Kuu

Kusikiliza / violence women

Siku kumi na sita za Maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana zianaanza leo, ambapo dunia inahamasishwa kupinga vitendo hivyo. Joseph Msami amefuatilia tukiohilona  hii ni taarifa yake (TAARIFA YA MSAMI) Akitoa ujumbe wake katika kuanza kwa siku Kumi na Sita za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana  Rais wa baraza kuu [...]

25/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji wa haki za binadamu Eritrea wasababisha maelfu kukimbilia uhamishoni

Kusikiliza / eritrea_medio

Kiasi cha raia 3,000 wa Eritrea wanaripotiwa kuondoka nchini mwao kila mwezi ili kujiepusha na mienendo ya uvunjifu wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na serikali pamoja na vyombo vya usalama. Taarifa hiyo imeibuliwa na Wataalamu huru wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. George Njogopa na taarifa kamili. (Taarifa ya George) [...]

25/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Geneva kuhusu Syria kufanyika Januari: Ban

Kusikiliza / KM Ban

Hatimaye tarehe ya mkutano wa pili wa amani kuhusu Syria imewekwa hadhari hii leo mjini New York na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon Ban Ki-Moon akieleza kuwa ni 22 Januari mwakani. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Jumatano ya tarehe 22 Januari 2014 ndio mkutano huo utafanyika mjini Geneva [...]

25/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muafaka wa mipango ya nyuklia ya Iran wakaribishwa na Katibu Mkuu

Kusikiliza / Silaha za nyuklia

Muafaka wa muda kuhusu mipango ya nyuklia ya Iran uliotangazwa Jumapili umekaribishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon. Kwa mujibu wa ripoti wawakilishi wa Marekani, Uingereza, Urusi, Uchina, Ufaransa na Ujerumani ambao hujulikana kama P5+1 wamefikia makubaliano naIranmapema Jumapili. Iran imearifiwa kukubali kusitisha baadhi ya mipango yake ya nyuklia kwa malipo ya [...]

25/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatimaye maafikiano yafikiwa Warsaw kuhusu kupunguza gesi chafuzi

Kusikiliza / Misitu hufyonza gesi chafuzi ya kaboni

Baada ya mijadala iloghubikwa na malumbano, hatimaye mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi mjini Warsaw, Poland umeibua fungu la maafikiano kuhusu jinsi ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi kutokana na uharibifu wa misitu. Muafaka kuhusu kinachotajwa kama REDD+ umeungwa mkono kwa ahadi za yapata dola milioni 280 za ufadhili kutoka Marekani, Uingereza na Norway. Rais wa [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya chanjo kwa watoto Ufilipino kuanza Jumatatu: OCHA

Kusikiliza / Watoto hawa wako hatarini kuambukizwa magonjwa

Hivyo ndivyo Mkuu wa ofisi ya masuala ya usaidizi wa kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Valerie Amos alipoanza mkutano wake na waandishi wa habari mjini New York, akieleza kile alichoshuhudia huko Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan kupiga nchi hiyo na kusababisha vifo na majeruhi pamoja na kupoteza makazi. Bi. Amos ambaye amekwenda Ufilipino mara mbili [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFCCC yazindua ubia mpya na kampuni ya GeSI

Kusikiliza / UNFCCC-LOGO

Makubaliano kati ya taasisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa, UNFCC na kampuni ya kimataifa ya suluhu endelevu mtandaoni, GeSi yanalenga kutafuta na kueneza matumizi ya teknolojia zisizo na madhara kwa mazingira. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya pande mbili hizo ikikariri UNFCCC ikisema [...]

22/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kingono wapigwa vita nchini Kenya

Kusikiliza / Maafisa wa Kenya katika usaidizi

Wakati dunia ikiadhimisha mkataba wa watoto unaolinda haki za kundi hilo muhimu katika jamii, nchini Kenya, kama kwingineko duniani, visa vya ubakaji vinatajwa. Hata hivyo katikati ya wingu hilo la ukatili wa kingono kuna habari njema za kuwanusuru wahanga wa matuko hayo. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo .

22/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

IOM yawakwamua wahamiaji wasio na nyaraka toka Tanzania walio mipakani huko Maziwa makuu

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe, msemaji wa IOM

Taarifa zinasema maelfu ya wahamiaji kutoka Tanzania wamekwama mipakani huku hali ya wasiwasi juu ya majaliwa yao ikiibuka. Hii inafuatia zoezi la serikali ya Tanzania kuwaondoa wahamiaji hao katika zoezi lililotangazwa na kutekelezwa na serikali hiyo. Hivi karibuni. Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limejikita kuwasaidia wakimbizi hao kama msemaji wa shirika la uhamiaji IOM [...]

22/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wigo wa vyanzo vya ajira upanuliwe: Dkt. Kituyi

Kusikiliza / Kijana akijaribu kujipatia kipato

          Wiki hii Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD limetoa ripoti kuhusu nchi zenye maendeleo duniani, LDCs kauli mbiu ikiwa  ustawi na ajira kwa maendeleo jumuishi na endelevu. Nchi hizo ziko 48 na miongoni mwao 34 zinatoka Afrika ikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Tanzania. Je ni mambo [...]

22/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kingono haukubaliki, bila kujali kavalia nini mwanamke: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kaatika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema  kila mmoja anatakiwa kutimiza jukumu lake la kukomesha imani zinazosaidia kuendeleza mazingira ambayo yanafanya ukatili dhidi ya wanawake kuonekana kama jambo la kukubalika, au kwamba wanawake hao wanastahili kufanyiwa ukatili. Amesema ukatili wa kingono hauwezi kukubalika kamwe, bila kujali mwanamke kavalia nini. [...]

22/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IUCN yachukua hatua kudhibiti biashara haramu ya ngozi ya Chatu

Kusikiliza / Nyoka

Hofu juu ya kutoweka kwa aina kuu mbili za chatu Kusini Mashariki mwa Asia kumesababisha kuanzishwa kwa ubia kati ya shirika la kimataifa la uhifadhi, IUCN na kampuni ya KERING inayomiliki nembo ya GUCCI. Ubia huo ulioanzishwa na kituo ha kimataifa cha biashara, ITC unalenga kuhakikisha biashara endelevu ya ngozi ya nyoka huyo aina ya [...]

22/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi wa Syria wakimbilia Lebanon

Kusikiliza / syrian refugees Lebanon

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa zaidi ya familia 500 za Syria zimelazimika kuvuka mpaka siku ya jumatano usiku na kukimbilia eneo la Aarsal kutokana na kuenea kwa mapigano hadi katika maeneo ya Nabek na Yabroad. Shirika hilo linasema kuwa zaidi ya watu 10,000 wamepatiwa msaada wa chakula. Idadi ya wakimbizi walioandikishwa [...]

22/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yachukua hatua ya kuwalinda manusura kutoka mikononi mwa wasafirishaji haramu wa watu

Kusikiliza / Manusura wa Kimbunga Haiyan

Huku watu zaidi wakijaribu kuhama maeneo yaliyokumbwa na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na serikali ya Ufilipino na washirika wake wamekuwa wakifanya jitiha za kuwazuia wale wanaohama kutoka kwa wasafirishaji haramu wa watu na kutambua mahitaji ya watu hao. IOM inakadiria kuwa hadi watu 5000 wanakimbia maeneo yaliyoathiriwa [...]

22/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wasio na vibali wakwama mipakani huko Maziwa makuu; IOM yatoa usaidizi

Kusikiliza / Burundian refugees

Wakati idadi kubwa ya wahamiaji wasiokuwa na vibali ambao hivi karibuni walifukuzwa nchini Tanzania wakiendelea kukwama katika maeneo ya mipakani, kumezuka hali ya wasiwasi juu ya majaliwa hayo.  Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limesema wahamiaji hao kutoka nchi za Rwanda, Uganda na Burundi wapo katika hali mbaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa DRC waanza kurejea nyumbani kutoka Uganda

Kusikiliza / DRC refugees

Takriban wakimbizi elfu saba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliotorokea nchi jirani ya Uganda kufuatia makabiliano kati ya jeshi la serikali ya DRC na waasi wa M23, wamerejea makwao baada ya utulivu kurejea. John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, ana ripoti kamili kutoka Uganda. (Tarifa ya John Kibego) Wakimbizi 3,275 pekee ndio [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto 6000 vitani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati: UNICEF

Kusikiliza / car-violence

Kundi moja lililojihami nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limewaingiza karibu watoto 6000 kwa jeshi lao kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. (Taarifa ya Jason) Karibu nusu ya watoto hao wameingizwa jeshini mwaka huu kufuatia kupinduliwa kwa serikali na waasi mwezi nMachi. UNICEF inasema [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Polio waanza kudhibitiwa eneo la Pembe ya Afrika

Kusikiliza / Polio-Horn-Africa-1Web

Kumekuwa na mafanikio ya kukabiliana na ugonjwa wa kupooza uliolipuka katika eneo la pembe ya Afrika miezi sita iliyopita ambao uliathiri watoto kiasi cha 2000 na watu wazima kadhaa. Maeneo yaliyopigwa na ugonjwa huo ni pamoja na Somalia, Kenya na Ethiopia. Ripoti zinaonyesha kuywa maeneo mengi yaliyokumbwa na tatizo hilo sasa yameanza kupata afuani kutokana [...]

22/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa OCHA ahitimisha tathmini ya janga la kimbunga huko Ufilipino

Kusikiliza / Valerie Amos ziarani Ufilipino

Mkuu wa Ofisi ya masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa, OCHA, Bi. Valerie Amos amehitimisha tathmini yake ya usaidizi wa kibinadamu huko Ufilipino kufuatia janga la kimbunga Haiyan lililopiga nchi hiyo takribani wiki mbili zilizopita. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Baada ya ziara ya wiki hii kwenye maeneo ya Tacloban, [...]

22/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wananchi wafundishwa namna ya kulinda mifugo Sudan Kusini

Kusikiliza / Mafunzo ya kulinda mifugo

  Mambo sasa ni shwari nchini Sudan Kusini. Hii ni baada ya matukio ya muda mrefu ya uwizi wa mifugo hatua iliyosababisha mamalaka ya polisi nchini humo kuingilia kati na kutoa mafunzo maalum kwa raia juu ya namna ya kukabiliana na uwizi huo. Asumpta Massoi anamulika mafunzo hayo katika makala ifuatayo.    

21/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi, maafikiano yacheleweshwa na malumbano

Kusikiliza / Dk Richard Muyungi

Wakati kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia kikielekea mwisho taarifa zinasema hali ni tete katika mijadala ambapo mabishano yameibuka kati ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea . Malumbano hayo yamesababisha vikao kufanyika hadi usiku wa manane na wakati mwingine baadhi ya wawakilishi kutoka nje [...]

21/11/2013 | Jamii: Mahojiano, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Kasi ya mageuzi inahitajika Sudan Kusini: UM

Kusikiliza / Hilde Johson

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini Hilde Johnson amesema ili Sudan Kusini ipige hatua za kimaendeleoa hususani kuimarisha taasisi za kitaifa lazima isukume kasi ya mageuzi muhimu. Katika mahojiano maalum na mwandishi wa idhaa ya Kingereza ya radio ya Umoja wa Mataifa Don Bob, Bi Johnson amesema msingi wa [...]

21/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa ya televisheni yaenziwa

Kusikiliza / TV children

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya televisheni inayoangazia umuhimu wa chombo hicho katika upashanaji habari. Siku hii ni matokeo ya azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwaka1946.Mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadahani Kibuga ametuandalia taarifa ifuatayo:

21/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Elimu ndio muarubaini wa kutokomeza ugaidi: Blair

Kusikiliza / Tony Blair

Kamati ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi imekutana leo ambapo mwasisi wa Tony Blair Faith Foundation, Tony Blair amehutubia kamati hiyo kwa niaba ya tasisi yake kuhusu namna ya kupambana na watekelezaji wa ugaidi kupitia elimu Akihutubuia mkutano huo Tony Balir ambaye ni waziri mkuu mstaafu wa Uingereza amesema [...]

21/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa MONUSCO ajibu maswali ya raia wa DRC

Kusikiliza / Mkuu wa MONUSCO Martin Kolber

Leo asubuhi, katika siku zake za kwanza kama Mkuu Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo, MONUSCO Martin Kobler amewasiliana na watumiaji wa Intaneti na mitandao habari ya kijamii kama vile twitter, faceboook na mtandao wa Radio Okapi kujibu masuali yao kuhusu kazi anayofanya DRC. Alice Kariuki na taarifa kamili: (RIPOTI YA ALICE KARIUK) [...]

21/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtandao maalum wa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi wazinduliwa

Kusikiliza / ctcn

Mwaka mmoja tangu kufanyika kongamano la 18 la mabadiliko ya tabia nchi, ambalo liliagiza kuundwa kwa chombo maalumu kitachomulika masuala ya teknolijia kuhusiana na mazingira, hatimaye mtandao maalumu umezinduliwa rasmi. Taarifa zaidi na George Njogopa: (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA) Mtandao huo ambao unanguvu za kisheria kulingana na mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi, [...]

21/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi Warsaw watafuta njia baada ya Kyoto

Kusikiliza / Warsaw SG--

Wakati kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kinakaribia ukingoni mjini Warsaw, Poland, bado makubaliano tarajiwa yatakayochukua nafasi ya mkataba wa Kyoto ambao haujaweza kudhibiti uchafuzi wa mazingira duniani hayajafikiwa huku ikielezwa malumbano yametawala mkutano baina ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea. Mwenyekiti wa [...]

21/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ashauriana na viongozi pembeni mwa mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

Kusikiliza / SG POLAND

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amefanya mkutano na washirika kwenye majadiliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mjini Warsaw Poland kwenye mkutano kuhusu mabadilio ya hali ya hewa ambao umekuwa ukindelea wiki hii. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. Taarifa ya Jason Nyakundi Ban alifanya mazungumzo na mawaziri kutoka kwa jumuia ya [...]

21/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamhuri ya Korea yaupiga jeki mfuko wa Global Fund

Kusikiliza / Global Fund

Mfuko wa Kimataifa kwa ajili ya kupanbana na Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria, umekaribisha tangazo la Jamhuri ya Korea kuwa itaongeza maradufu mchango wake kwa mfuko huo wa Global Fund kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kwa kutumia fedha zitakazotokana na ada inazotoza wanunuzi wa tikiti za safari za ndege. Wizara ya Afya ya Jamhuri [...]

21/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afya ya watoto yaangaziwa nchini Tanzania

Kusikiliza / Mama na mtoto

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya mkataba wa watoto ambapo haki za mtoto huangaziwa, idhaa hii inamulika afya za watoto katika nchi za Afrika Mashariki hususani Tanzania. Kutokana na takwimu za vifo vya watoto katika mikoa ya kanda ya ziwa kuwa juu, serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii chini [...]

20/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake kutetewa ili wajitokeza kwenye sayansi ya Nyuklia

Kusikiliza / Janice Dunn Lee

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la nguvu za atomiki la Umoja wa Mataifa anatazamia kuzungumzia nafasi ya mwanamke kwenye masuala ya sayansi, wakati atapohutubia hadhara moja mjini New York mwishoni mwa juma.  Bi Janice Dunn Lee ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo, atagusia umuhimu wa wanake kushiriki kwenye masuala ya sayansi hasa lakini [...]

20/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaharakisha misaada kwa waathirika wa kimbunga

Kusikiliza / Ufilipino

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limeanza kusambaza misaada ya dharura kwa waathirika kwa kimbunga Haiyan baada ya ndege yake ya mizigo kuwasili katika uwanja wa Tacloban . Misaada hiyo imepekekwa katika eneo la San Jose eneo ambalo limeaathiriwa vibaya na kimbunga hicho. Kumekuwa na uharibifu mkubwa katika eneo ka San Jose [...]

20/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa Ajira bado changamoto kwa uchumi wa nchi zinazoendelea:Ripoti

Kusikiliza / UNCTAD

Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendelo, UNCTAD limetoa ripoti ya nchi zinazoendelea ya mwaka 2013 yenye kauli mbiu, ustawi na ajira kwa maendeleo jumuishi na endelevu. Ripoti hiyo inayobainisha kwamba watu millioni 130 wataingia sekta ya ajira katika nchi zinazoendelea kufikia mwaka 2020, imeangalia uchumi wa  nchi zinazoendelea na uhusiano wake na [...]

20/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Krähenbühl wa Geneva kuwa kamishina mkuu wa UNRWA

Kusikiliza / Pierre Kraehenbuel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemteua Pierre Krähenbühl wa Switzerland kuwa kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa kipalestina UNRWA. Uteuzi huo unafautia ushauri wa tume ya ushauri ya UNRWA ambapo mteule huyo anachuku anafasi ya Filippo Grandi. Bwana Krähenbühl ana uzoefu [...]

20/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Poland

Kusikiliza / KM Ban na Waziri Mkuu wa Polanda, Donald Tusk

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Polanda, Donald Tusk, pembezoni mwa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ambayo yanaendelea nchini humo katika mji mkuu, Warsaw. Katika Mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Bwana Ban na Waziri Tusk wamejadili kuhusu jinsi ya kuimarisha zaidi [...]

20/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanakandanda wa kimataifa Falcao kuwa balozi mwema wa UNODC:

Kusikiliza / Radamel Falcao García Zárate

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na madawa na uhalifu UNODC Yury Fedotov, amemteuwa mwanasoka wa kimataifa kutoka Colombia Radamel Falcao García Zárate kuwa balozi mwema wa shirika hilo. Falcao, ni mshambuliaji hatari ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Monaco F.C. baada ya kuondoka Atlético Madrid. Bwana Fedotov amesema Falcao amewika saana [...]

20/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban amewapongeza watu wa Nepal kwa uchaguzi wa bunge:

Kusikiliza / Uchaguzi Nepal

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa Nepal kwa kuendesha uchaguzi wa bunge kwa amani na mafanikio. Amesema Idadi ya watu waliojitokeza inadhihirisha nia yao ya kusukuma mbele mchakato wa amani. Bunge hilo jipya litakuwa na majukumu ya kihistoria ya kukamilisha katiba mpya, kuendeleza mafanikio ya mchakato wa amani yaliyopatikana hadi [...]

20/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lamulika hali CAR na waasi wa LRA

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekutana leo kujadili hali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku masuala ya usalama na uhalifu unaovuka mipaka yakimulikwa, vikiwemo vitendo vya waasi wa LRA. Joshua Mmali na taarifa kamili: (TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Wakati wa Mkutano wake hii leo, Baraza la Usalama limesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu [...]

20/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi yaongezeka: UNAIDS

Kusikiliza / Mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe

Katika kuelekea siku ya Ukimwi duniani tarehe Mosi Mwezi ujao, Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na Ukimwi, UNAIDS limesema lina hofu juu ya ongezeko la maambukizi mapya ya Ukimwi Ulaya Mashariki, Asia ya Kati, Mashariki ya Kati na Afrika kaskazini. Ripoti kamili na George Njogopa. (Taarifa ya George)

20/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya watoto duniani yaadhimishwa leo wakati suala la kiweka wazi dhuluma dhidi ya watoto likipewa kipaumbele

Kusikiliza / unicef violence

Wakati siku ya watoto inapoadhimishwa ambapo haki za watoto zinakumbukwa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linataka maslahi ya watoto kuangaziwa zaidi na kila nchi hasa wale wanaokumbwa na dhuluma na mateso yasiyotambuliwa . Taarifa ya Flora Nducha inafafanua zaidi. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Mkurugenzi mkuu wa shirika la kuhudumia watoto la [...]

20/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fedha ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi: Ban

Kusikiliza / climate-change-adaptation

Mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea huko Warsaw Poland umeingia siku ya pili ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya harakati za kupambana na mabadiliko hayo ni suala muhimu. Akizungumza kwenye kikao cha mawaziri, Ban amesema jambo muhimu kwanza ni sera bora za uwekezaji usioharibu mazingira lakini [...]

20/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani vikali shambulio la Beledweyne Somalia:

Kusikiliza / Mashambulio Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio lililokatili maisha ya watu dhidi ya kituo cha polisi huko Beledweyne, Somalia,. Shambulio hilo limefuatia mashambulio mengine kadhaa kama hayo katika wiki za hivi karibuni. Ban amesema vitendo hivyo vya kigaidi dhidi ya serikali na watu wa Somalia vimesababisha machungu makubwa. Katibu Mkuu ametuma [...]

20/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani vikali shambulizi la bomu Lebanon

Kusikiliza / Rais wa Baraza la Usalama Balozi Liu Jieyi wa Uchina

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamelaani vikali shambulio la bomu lililotekelezwa dhidi ya ubalozi wa Iran mjini Beirut, Lebanon, ambalo limewaua watu wapatao 23 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 140 karibu na ubalozi huo. Kundi moja linajihusisha na kundi la kigaidi la Al-Qaeda limedai kutekeleza shambulizi hilo. Wanachama wa Baraza la [...]

19/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa vyoo wahatarisha afya za wananchi nchini Kenya

Kusikiliza / MKURU KWA NJENGA

Dunia ikiadhimisha siku ya choo duniani leo Nov 19, 2013 baadhi ya nyumba bado hazina vyoo. Takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 kote duniani hawana vyoo hatua inayoweza kusababisha matatizo ya afya kwao. Mwandishi wetu Jasson Nyakundi anamulika hali ilivyo nchini Kenya ambapo anazungumza na Samwel Waweru akiwa Mukuru Kwa njenga anayemiliki choo cha [...]

19/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulizi huko Lebanon

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu vikali shambulio la kigaidi lililotokea leo karibu na ubalozi wa Iran uliopo mji mkuu wa Lebanon, Beirut na kusababisha vifo vya raia 23 akiwemo mwanadiplomasia mmoja wa Iran na majeruhi zaidi ya mia moja. Ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za waliokufa pamoja na serikali [...]

19/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Afrika hatarini kuingia kwenye gharama kubwa –UNEP

Kusikiliza / Gharama ni kubwa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi:UNEP

 Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP imesema kuwa gharama ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika itaongezeka kwa kiasi kikubwa iwapo hatua mahsusi hazitachukuliwa hivi sasa. Yakadiriwa kwamba Afrika inaweza ikaingia gharama ya dola Bilioni 350 kila mwaka ifikapo mwaka 2070 iwapo wakati huu itashindwa kutekeleza mipango [...]

19/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya watu wahama mapigano nchini Syria na kuingia nchini Lebanon

Kusikiliza / Wasyria wanokimbia kuelekea Lebanon (UNHCR)

Takriban watu 6000 wamekimbia makwao eneo la Qarah  nchini Syria  ambapo wamevuka mpaka na kuingia mashariki mwa Lebanon. Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu yamekuwa nchini Lebanon tangu juma lililopita yakifanya kazi na wizara inayohusika na masuala ya kijamii kukabiliana na hali hii. Kuhama huku kumetokana na  kuongezeka kwa ghasia eneo la Qarah na vijiji [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji zaidi ya milioni tano wanaishi Italy: IOM

Kusikiliza / Wahamiaji wanaotumia boti kusafiri hadi Italia

Ripoti ya kuhusu uhamiaji iliyozinduliwa na ofisi ya taifa ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Italia na taasisi ifahamikayo kwa jina la IDOS inaonyesha kuwa nchi hiyo ina wahamiaji zaidi ya milioni tano ambayo ni asilimia 7.4 ya idadi ya watu. Ripoti hiyo kadhalika inabainisha kuwa wahamiaji nchini Italia wanachangia asilimia 12 ya pato la [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OHCRM yatilia shaka baada ya kuzuka upya machafuko Libya

Kusikiliza / Ofisi ya haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani na kuelezea masikitiko yake kutokana na kujirudia upya machafuko nchini Libya ambayo yamesababisha zaidi ya watu 40 kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa tangu yaliyozuka ijumaa iliyopita. Grace Kaneiya na maelezo kamili  (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Kumekuwa na ongezeko kubwa la umwagaji damu katika mji [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi waendelea na kuhama wakitafuta misaada nchini Ufilipino

Kusikiliza / Waathirika wa Kimbunga Haiyan wahama kutafuta misaada

Maelfu ya  watu walionusurika kimbunga Haiyan kutoka maeneo ya Tacloban nchini Ufilipino wameripotiwa kuhama makwao wakitafuta wenzao na misaada kwenye maeneo yaliyo karibu na pia ya mabli kama Cebu naManilakwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. UNHCR inasema kuwa muda mfupi baada ya kimbunga kuikumba Ufilipino watu walianza kuondoka kwa [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa COP19 wafunguliwa, viongozi watakiwa kufikiria kwa mapana zaidi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akihutubia mkutano wa COP19 huko Warsaw, Poland

Mkutano wa ngazi ya juu wa mabadiliko ya tabia nchi, umefunguliwa rasmi huko Poland ambapo Umoja wa Mataifa umetaka viongozi kutokuwa wabinafsi katika fikra za mabadiliko ya tabianchi, huku shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa likitoa ripoti inayosema kuwa gharama za kukabili mabadiliko ya tabianchi Afrika itaongezeka iwapo hatua hazitachukuliwa. Assumpta Massoi na ripoti [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya choo duniani:UM

Kusikiliza / Choo

Leo ni siku ya choo duniani inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa huku kukitolewa wito wa kuboresha mazingira na kuzingatia usafi wa vyoo vyenyewe. George Njogopa na taarifa zaidi (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Siku hii ya choo duniani inakumbusha ulimwengu kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 duniani kote wanakabiliwa na matatizo yanayoambatana na ukosefu wa vyoo [...]

19/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaendelea kuratibu misaada ya madawa Ufilipino:

Kusikiliza / Hospitali ya muda Ufilipino

Ikiwa ni zaidi ya siku kumi tangu kuzuka kwa kimbunga Haiyan nchini Ufilipino, shirika la afya duniani WHO linaendelea kuleta wataalamu wa kitabibu kutoka sehemu mbalimbali wanaokwenda Ufilipino . Hivi sasa kwa mujibu wa shirika hilo wanajikita zaidi kwa majeruhi na wale walioathirika kisaikolojia na kimbunga hicho huku wakitilia maanani mahitaji ya muda mrefu ya [...]

19/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Familia nyingi Tacloban zimepoteza kila kitu:UNICEF.

Kusikiliza / Waathirika wa kimbunga Haiyan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema uharibifu uliosababishwa na kimbunga Haiyan mjini Tacloban na voinga vyake ni mkubwa saana. Linasema familia nyingi zimepoteza kila kitu na msaada ndio unaanza kuwafikia huku serikali na mashirika ya makanisa yakiendelea kuwasaidia. Kwa mujibu wa UNICEF msaada wa haraka unahitajika ili kuzuia kusambaa kwa magonjwa [...]

19/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Filamu ya Mary na Martha yatanabaisha athari za malaria

Kusikiliza / Mbu wasabibishao Malaria

Mpango wa kimataifa wa kudhibiti malaria,The Roll Back Malaria umeshirikiana na Richard Curtis ambaye ametengeneza filamu iitwayo Mary and Martha inayojikita katika kutanabaisha mkasa wa gonjwa la malaria. Mada kuu ya filamu hiyo ni safari ya mama hao wawili mmoja toka Marekani na mwingine uingereza na kila mmoja wao ameathirika na malaria na maisha yao [...]

19/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 13 wameathirika na kimbunga Haiyan:OCHA

Kusikiliza / Waathirika wa kimbunga Haiyan

Idara ya ustawi wa jamii na maendeleo ya Ufilipino inakadiria kwamba watu milioni 13 wameathirika na kimbunga Haiyan na wengine milioni 4 wametawanywa , limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. OCHA imeongeza kwamba watu zaidi ya 392,000 wanaishi katika vituo vya muda 1,587 ambavyo vingi [...]

19/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ayapongeza mataifa ya Baltic kwa kuwawezesha wanawake:

Kusikiliza / Ban Lithuania

Mataifa ya Baltic yamepongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa hatua waliyopiga katika kutumia teknolojia kwa ajili ya maendeleo na kuwawezesha wanawake. Ban Ki-moon ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari Vilnius, mji mkuu wa Lithuania, wakati akihitimisha ziara yake ya mataifa ya Baltic Jumatatu. Amesema amehamasishwa saana na ari ya mataifa [...]

18/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Chinua Achebe aenziwa hapa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Wakati wa tamasha ya Chinua Achebe

Hapa Umoja wa Mataifa, mwishoni mwa wiki iliopita katika kumbu kumbu ya kumuenzi na kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanariwaya nguli Chinua Achebe. (Makala ya Chinua)

18/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Spika Makinda asema mabadiliko ya sheria ya ndoa yana mlolongo mrefu

Kusikiliza / Sika Anna Makinda

Mkutano wa nane uliwaokutanisha maspika wanawake duniani umemalizika mwishoni mwa juma mjini New York huku mjadala mkubwa ukiwa ni mkakati wa usawa wa kijinsia kuwa sehemu ya malengo endelevu ya milenia baada ya 2015. Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami amekutana na kufanya mahojiano na miongoni mwa waliotoa [...]

18/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNAMID kuwezesha majadiliano baina ya Misseriya na Salamat Darfur:

Kusikiliza / UNAMID

Kufuatia mapigano baina ya Salamat na Misseriya katikati mwa Darfur yaliyokatili maisha ya watu zaidi ya 10 juma lililopita , mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur (UNAMID) iliwezesha kusafiri kwa Wali gavana wa Darfur Kati na kamati ya taifa ya usalama. Watu hao wanaambatana na timu [...]

18/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Licha ya matumaini ya maendeleo, kuna walakin Sudan Kusini: UM

Kusikiliza / Hilde Johnson, UNMISS

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS, Hilde Johnson, ameliambia Baraza la La Usalama kuwa licha ya dalili za matumaini ya kujikwamua na kujiimarisha, taifa la Sudan Kusini bado lipo kwenye barabara ya misukosuko.   Bi Johnson amesema taifa hilo limekabiliwa na changamoto kubwa tangu lijipatie [...]

18/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Moshi wa chuki dhidi ya binadamu bado unafuka, tusikubali: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu,UM Ban Ki-moon na mkewe Yoo Soon-taek katika kumbukumbu ya wayahudi waliopoteza maisha chini ya uongozi wa Hitler

Auschwitz-Birkenau siyo tu eneo lenye orodha ya waliokumbwa na mauaji ya kimbari dhidi ya wayahudi, bali pia ni eneo ambapo wahanga walihifadhi ujasiri wao na matumaini. Ni kauli ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyotoa Jumatatu baada ya kutembelea kambi hiyo iliyokoPoland ambayo ilitumika kwa mauji ya halaiki. Bwana Ban ametumia fursa [...]

18/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwafikia wakimbizi wa kipalestina huko Yarmouk bado ni taabu: UNRWA

Kusikiliza / wakimbizi, kambini

  Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na usimamizi na huduma kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA linazidi kupata hofu juu ya hatma ya wakimbizi hao hususan walioko kambi ya Yarmanouk kwa kuwa hivi sasa hawawezi kufikiwa ili kupatiwa huduma muhimu. Taarifa ya UNRWA inasema wakimbizi hao wanahitaji misaada ya kibinadamu lakini kutokana na hofu ya [...]

18/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaleta matumani kwa manusura wa kimbunga Haiyan

Kusikiliza / Manusura wa kimbunga Haiyan

Manusura wa kimbunga Hayan Evelyn Quisaba ameelezea namna alivyonusurika kifo ikiwa siku chache tu baada ya kuokolewa katika hatari ambayo imeangamiza mamia ya raia. Evelyn mwenye umri wa miaka 53 ambaye aliokolewa kwa kupatiwa kifaa maalumu amesema kuwa hakuamini macho yake wakati aliporejeshwa nyumbani kwake San Roque na kukuta kila kitu kimekwenda na maji. Lakini [...]

18/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mpatanishi wa mzozo wa Darfur akutana na viongozi wa Sudan Kusini

Kusikiliza / Ibn Chambas

Mjumbe wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa ambaye ni mpatanishi wa pamoja kwa mzozo wa Darfur Mohamed Ibn Chambas, amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Sudan Kusini ikiwa ni sehemu ya kuleta suluhu ya kidiplomasia. Katika ziara yake nchini humo, mjumbe huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa rais James Wani Igga, [...]

18/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya viwanda barani Afrika kuadhimishwa tarehe 22 mwezi huu

Kusikiliza / manufacturing Africa

Siku ya viwanda barani Afrika yenye kauli mbiu ubunifu wa ajira na maendeleo ya kibiashara ikiwa ni njia ya kuchochea maendeleo barani Afrika itaadhimishwa mjini New York tarehe 22 mwezi huu. Siku hii iliyobuniwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1989 inatoa hamasisho kuhusu wajibu wa viwanda kwenye maendeleo ya bara la Afrika [...]

18/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nchi wanachama watakiwa kushirikiana na Somalia kupambana na uharamia:

Kusikiliza / pirates of somalia

Nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamechagizwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Somalia kuhakikisha wanatokomeza tatizo la uharamia. Joshua Mmali na taarifa kamili: (TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Ni rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Novemba, Balozi Liu Jieyi wa Uchina, akitangaza matokeo ya kura kuhusu kupambana na uharamia [...]

18/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma ya maji yarejea huko Tacloban

Kusikiliza / tacloban-damage-300x257

Bado twaangazia kimbunga Haiyan ambapo hatimaye huduma kamili ya maji safi na salama imerejea kwa takribani watu laki mbili walioathriwa na kimbunga hicho kwenye mji wa Tacloban nchini Ufilipino na wilaya nyingine sita zinazozunguka mji huo. Kurejea kwa huduma hiyo kunafuatia kukamilika Jumapili usiku kwa ukarabati wa mtambo wa kutakasa maji. George njogopa na ripoti [...]

18/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia wapigiwa chepuo na maspika wanawake duniani

Kusikiliza / Spika anna Makinda

  Mkutano wa muungano wa wabunge duniani uliohusisha maspika wanawake umemalizika mwishoni mwa juma mjini New York ambapo Tanzania iliwakilishwa na Spika Anna Makinda. Joseph Msami alifanya mahojiano na Spika Makinda na hii hapa ni taarifa yake. (TAARIFA YA JOSEPH) Akizungumza katika mahojiano maalum baada ya kuhudhuria mkutano huo, spika Makinda amesema miongoni mwa mambo [...]

18/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahudumu wa Afya wametia nanga Ufilipino: WHO

Kusikiliza / unicefphilippines

Nchini Ufilipino zaidi ya wiki moja baada ya kimbunga Haiyan kupiga eneo hilo, Shirika la afya duniani WHO linasema timu ya wataalamu wa afya inayofuatilia magonjwa iko nchini humo ijapokuwa hakuna mlipuko wa magonjwa uliokwisharipotiwa. Jason Nyakundi na Ripoti kamili. (Ripoti ya Jason) Mengi ya makao 1500 kwenye maeneo yaliyokumbwa na kimbuga yana misongamano ya [...]

18/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwepo na ushirika wa kiuchumi kuongeza uwekezaji OIC:UNCTAD

Kusikiliza / unctad_logo_copy1-300x257

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo na biashara UNCTAD kuhusu muundo wa uwekezaji wa kimataifa inasema uwekezaji wa moja kwa moja wa nje FDI kwenda kwa shirika la jumuiya ya ushirikiano wa n hi za Kiislam OIC umejikita katika baadhi ya nchi tuu. UNCTAD inasema kwa kufanya hivyo umesalia kuwa mdogo katika [...]

18/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kimbunga Haiyan ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa ziarani nchini Lithuania amekutana na kuzungumza na wasomi na viongozi wa kijamii katika chuo kikuu La Vytutas Magnus nchini humo ambapo amesema changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ni tishio kubwa la mustakabali wa dunia. Akitolea mfano wa kimbunga  Haiyan kilichoikumba Ufilipino hivi karibuni na kusababisha [...]

17/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa WFP akutana na manusura wa kimbunga Hyan mjini Tacloban

Kusikiliza / ertharin-cousin

  Ingawa changamoto ya utaratibu wa ugavi inaendelea lakini chakula kingi kinaendelea  kuwasili Ufilipino nchi ambayo ilikumbwa na kimbunga Haiyan, kwa mujibu wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP. Shirika hilolinasema chakula kwa watu zaidi ya laki saba kimepelekwa katika jamii zilizoathirika ikiwemo vifurushi vya chakulakamamchele na biskuti zenye kiwango cha juu cha nguvu [...]

17/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha hitimisho la uchaguzi wa rais nchini Maldives

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban

Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidi mchakato wa kidemokrasia na mafanikio nchini Maldives , amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Kin Moon wakati akipokea hitimisho la kurudiwa kwa uchaguzi wa rais nchini humo.  Katika taarifa uiliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu Jumapili, Bwana Ban amesema  kwa mara nyingine idadi kubwa ya watu waMaldiveswamejitokeza [...]

17/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutumie hatua rahisi kuepusha vifo vya watoto njiti: Balozi Kasese-Bota

Kusikiliza / Mama akiwa amembeba mwanae kwa njia ya Kangaroo ili kumpatia joto.

Mtoto mmoja kati ya watoto Kumi huzaliwa kabla ya muda yaani njiti na katika matukio mengi hufariki dunia. Ni takwimu zilizotolewa wakati wa kongamano tangulizi kuhusu siku ya kimataifa ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu watoto njiti na hatua za kuchukua kuboresha afya zao ili waepuke magonjwa nyemelezi kama vile numonia na kuhara. Siku hiyo [...]

17/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa choo ni jambo la kudhalilisha: Eliasson

Kusikiliza / Jan Eliasson

Ni jambo la kudhalilisha na lisilokubalika ya kwamba watu bilioni Mbili na Nusu duniani hawana huduma bora za vyoo na huishia kujisaida hovyo na kuhatarisha afya zao na za jamii zao. Ni kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson katika kuelekea kuadhimisha siku ya choo duniani tarehe 19 Novemba. (Sauti ya [...]

17/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwanariwaya nguli Chinua Achebe aenziwa Umoja wa Mataifa:

Kusikiliza / Tumbuizo wakati wa siku ya kumuenzi Chinua Achebe

Hapa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa kumefanyika kumbukumbu maalum ya kumuenzi jabali wa fasihi na mwanariwaya nguli Chinua Achebe. Chinua Achebe aliyezaliwa tarehe 16 Novemba mwaka 1930 nchini Nigeria ni mashuhuri kwa kazi zake za fasihi ikiwemo riwaya kama ile ya "Things Fall Aparty" na mashairi. Vitabu vya Achebe vimevuka mipaka ya Nigeria, na [...]

16/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Urejeshaji wa wakimbizi wa Burundi walioko Uganda wamulikwa

Kusikiliza / Wakimbizi wa Burundi walioko Uganda

Burundi,Ugandana Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR wamefikia makubaliano ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Burundi waliochukua hifadhi  nchiniUganda. Hii ni baada ya kikao cha pande hizo tatu kilichofanyika hivi karibuni mjini Bujumbura Burundi.Uganda imewapa hifadhi zaidi ya wakimbizi elfu 10 kutoka Burundi, sehemu kubwa walikimbia machafuko ya mwaka wa 1993. Shughuli hiyo [...]

15/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Huu ni ushindi kwa Afrika, haturudi nyuma -Balozi Macharia

Kusikiliza / Macharia Kamau

Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa balozi Macharia Kamau amesema kile kinachoonekana kama kushindwa kwa ombi la Umoja wa Afrika kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya yaliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC ni ushindi mkubwa kwa Afrika. [...]

15/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNECE yataka hatua kuchukukuliwa ulimwengu unapoadhimisha siku ya choo duniani

Kusikiliza / world_toilet_day

Huku watu watu bilioni sita kati ya watu bilioni saba duniani kwa sasa wakiwa wanamiliki simu za mkononi ni watu bilioni 4.5 tu walio na choo, watu bilioni 2.5 wakiwa hana choo za kisasa huku watu wengine bilioni moja wakiwa hawa choo kabisa kwa mjibu wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya [...]

15/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Suala la kuahirisha kesi ya viongozi wa Kenya ICC halijaenda kombo: Balozi Macharia

Kusikiliza / Balazi Macharia Kamau

Mwakilishi wa kudumu wa KenyaKwenye Umoja wa Mataifa Balozi Macharia Kamau akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi tu baada ya Baraza la Usalama kukataa rasimu ya azimio la kuahirisha hadi wakati muafaka kesi zinazokabili viongozi waandamizi wa Kenyakwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague. Balozi Kamau amesema kilichojiri kwenye upigaji kura [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yawasaidia wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu kutoka Ulaya:

Kusikiliza / iom logo

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Ufaransa limezindua mradi wa kuwarejesha katika maisha ya kawaida wahanga 130 wa usafirishaji haramu wa binadamu ambao wameamua wanataka kurejea kwa hiyari katika nchi walizotoka barani Afrika, Asia na Amerika ya Kusini wakitoka katika nchi za muungano wa Ulaya. Mradi huo wa pamoja walioouita CARE una lengo la [...]

15/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuwalinda wakimbizi wa ndani Sudan Kusini kupewe kipaumbele:Beyani

Kusikiliza / Chaloka Beyani

Hatua za kibinadamu, kujumuishwa katika katiba, maendeleo na hatua za kuleta amani ni viungo muhimu kwa suluhu ya wakimbizi wa ndani na wale wanaorejea nyumbani. Hayo yamesemwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani ambaye ameongeza kuwa maendeleo na amani haviwezi kupatikana wakati maelfu ya [...]

15/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO na washirika wake wameanza kuwafikia wanaohitaji msaada katika visiwa vingi Ufilipino:

Kusikiliza / typhoon_philippines_20131113

Shirika la afya duniani WHO linafanya kazi kwa karibu na serikali ya Ufilipino na wadau wengine wa kimataifa kuwafikia manusura wa kimbunga Haiyan ambao wanahitaji huduma za afya. Hali halisi ya athari za kimbunga hicho inaanza kubainika sasa huku maeneo mengi yakihitaji msaada. Takribani majimbo saba yameathirika na kimbunga hicho ambayo ni Samar, Leyte, Cebu, [...]

15/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yalaani ubaguzi dhidi ya waziri wa sheria wa Ufaransa:

Kusikiliza / Waziri Christiane Taubira

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira. Kwa mujibu wa ofisi hiyo mashambulizi hayo ya wiki chache zilizopita yanajumuisha habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la kila wiki lililotoka Jumatano likiambatanisha picha yake na kichwa cha habari "hila [...]

15/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa mafuta waathiri jitihada za utoaji misaada Ufilipino:UM

Kusikiliza / typhoon-haiyan3

Nchini Ufilipino ambako wakati mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiendelea na jitihada za kutoa misaada kwenye maeneo yaliyokumbwa na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino uhaba mkubwa wa mafuta umekwamisha jitihada za kuwafikia mamilioni ya watu walioathiriwa na kimbunga hicho. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa hata [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakataa ombi la Kenya la kutaka kesi ziahirishwe

Kusikiliza / Baraza la usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo baada ya kupokea ombi kutoka Umoja wa Afrika la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya iliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC imepiga kura na kupinga ombi hilo. Flora Nducha na ripoti kamili.  (Ripoti ya Flora)  Ijumaa asubuhi wajumbe wa Baraza la [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wanaojaribu kuingia Ulaya wakataliwa na kurejeshwa walikotoka:UNHCR

Kusikiliza / Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema linatiwa hofu na hatua ya baadhi ya nchi za muungano wa Ulaya kuweka vikwazo vya kuingia au kuwarejesha kwa nguvu watu wanaoomba hifadhi wakiwemo wale waliokimbia machafuko nchini Syria. Kwa mujibu wa shirika hilo Bulgaria mwishoni mwa wiki iliwakatalia kuingia wakimbizi 100 na kuweka polisi [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA yakamilisha uchunguzi Australia

Kusikiliza / IAEA LOGO

Timu ya wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu nguvu za atomiki IAEA leo limekamilisha tathimini ya usalama nchini Australia namna taifa hilo linavyochukua hatua za usalama kuhusiana na matumizi ya nukilia. Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wamekuwa nchini humo kwa muda wa wiki mbili ambako pa moja na kufanya ukaguzi wa mitambo [...]

15/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Misaada ya UNHCR kwa waathirika wa kimbunga Philippine yaanza kuwasili

Kusikiliza / philippines12nov

Kumekuwa na ongezeko kubwa la misaada kwa waathirika wa kimbunga Haiyan kilichowakumba raia wa Ufilipino baada ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kusambaza misaada kadhaa kwa njia ya ndege. Ndege mbili za shirika hilo zimekuwa zikidondosha misaada eneo Cebu ambalo limeaathiriwa zaidi na juhudi za kuyafikia maeneo mengine ikiwemo mji wa [...]

15/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni Wakati wa kutoa mchango wa kweli kukabiliana na tabia nchi: Mtaalam wa UM

Kusikiliza / HRC 21

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu na mshikamamo wa pamoja duniani Virginia Dandan, amezitaka nchi kutoa michango ya kweli ili kukabiliana na tatizo la tabia nchi.  George Njogopa na taarifa kamili (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Wito wa Bi Dandan umekuja katika wakati ambapo wataalamu wa majadiliano ya mapatano kutoka mataifa [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Heko Afrika kwa kuchukua hatua kulinda albino: Ofisi ya Haki za binadamu

Kusikiliza / Albinos_Senegal_IRIN-Helen-Blakesley

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imepongeza hatua ya Tume ya Afrika ya kuridhia azimio la kwanza la ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi barani humo au Albino huku ikisema kilichobakia sasa ni utekelezaji na elimu kwa umma juu ya haki za msingi za kundi hilo. Msemaji wa Ofis hiyo Rupert [...]

15/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka udhibiti wa vikosi vya FDLR

Kusikiliza / Kikosi cha MONUSCO kikiwa kwenye doria huko DR Congo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia taarifa ya Rais wa baraza hilo ambayo pamoja na mambo mengine inakaribisha kumalizika kwa uhasama kati ya serikali ya DR Congo na waasi wa M23 na kusema kutaka hitimisho la haraka la mazungumzo ya Kampala yanayotoa fursa ya kupokonywa silaha waasi na kuwajibika kwa waliokiuka haki za [...]

14/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban asifu hatua za maendeleo Latvia

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelipongeza taifa la Latvia kwa kuendeleza haki za binadamu, kuwapa wanawake nguvu na kuendeleza usawa wa jinsia. Bwana Ban amesema hayo katika mkutano na waandishi habari wakati wa ziara yake nchini humo, akiongeza kuwa taifa hilo huchangia mara kwa mara kwa ajenda ya kimataifa ya amani, [...]

14/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Kisukari umebadili maisha yangu: Mkazi wa Tanga, Tanzania

Kusikiliza / Mkoani Morogoro Daktari akimpima Kisukari mmoja wa wakazi

Mtu anapopatiwa taarifa ya kwamba ana ugonjwa wa Kisukari, punde maisha yake hubadilika! Hulazimika kuchukua hatua kadhaa ikiwemo matibabu ya kila siku, kubadili mlo na hata mfumo wa maisha. Kama mtu alizowea mtindo fulani wa maisha hulazimika kubadili iwapo anataka kupata ahueni au kudhibiti ugonjwa huo. Shirika la afya duniani linasema hivi sasa kuna wagonjwa [...]

14/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

ICC yaitaka Libya imkabidhi Saif al Gaddafi kwa mahakama hiyo

Kusikiliza / Fatou Bensouda, Mwendesha mashtaka wa ICC(Picha ya faili)

Serikali ya Libya imeombwa imkabidhi Saif al Gaddafi kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, ili afunguliwe mashtaka. Wito huo umetolewa na Mwendesha Mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, wakati akilihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchiniLibya. Joshua Mmali na taarifa kamili TAARIFA YA JOSHUA Bi Bensouda amesemaLibyaimepiga hatua kadhaa kisheria, ikiwemo kuridhia mkataba wa Rome, [...]

14/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Chanjo ya Malaria sasa majaliwa 2030: WHO

Kusikiliza / Watoto, kizazi kijacho

Shirika la Afya duniani, WHO limetangaza lengo la kuwa na leseni ya chanjo dhidi ya Malaria ifikapo mwaka 2030. Imesema chanjo hiyo itakuwa na uwezo wa kupunguza wagonjwa wa Malaria kwa asilimia 75 na kutokomeza kabisa ugonjwa huo.  Taarifa zaidi na Flora Nducha.  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Mkurugenzi anayehusika na  mpango wa ugonjwa wa Malaria [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wametelekezwa: Mia Farrow

Kusikiliza / Watoto CAR

Jamhuri ya Afrika ya Kati  balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Mia Farrow ametaka hatua za haraka kumaliza ghasia nchini humo kwani raia ndio wanaoteseka na yaonekana wametelekezwa. Jason Nyakundi na ripoti kamili. (Ripoti ya Jason) Akizungumza baada ya ziara ya juma moja nchini humo Bi Farrow amelitaja taifa [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa tushikamane kuwasaidia waathirika wa kimbunga Ufilipino:Amos

Kusikiliza / Valerie Amos, OCHA azuru jamii zilizoathirika na kimbunga Haiyan, Ufilipino

Mratibu wa Umoja wa mataifa wa misaada ya dharura Bi Valarie Amos Alhamisi amezungumzia haja ya mshikamano wa jumuiya ya kimataifa kuwasaidia waathirika wa kimbunga Haiyan nchini Ufilipino. Bi amos Jumatano alikwenda Tacloban moja ya maeneo yaliyoathirika vibaya sana na kimbunga hicho ambako amezungumza na manusura wasio na malazi , wakisubiri wa hamu msaada kuwafikia. [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makampuni yalitumia fedha nyingi zaidi kwa kujitangaza:WIPO

Kusikiliza / Francis Gurry, Mkurugenzai Mkuu, WIPO

Makampuni kote duniani yanatumia hadi dola nusu trillion kila mwaka kwa kutangaza majina yao zaid ya fedha zinazotumika kwenye utafiti na hata zaidi ya uwekezaji mzima wa kampununi . Alice Kariuki na maelezo kamili. (RIPOTI YA ALICE KARIUKI) Hayo yameelezwa kwenye ripoti ya shirika la kimataifa linalohusika na kulinda mali WIPO , ambalo limefanya uchambuzi [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Kisukari wakwangua mifuko ya wagonjwa

Kusikiliza / Vipimo vya kiwango cha sukari

Ikiwa siku ya Kisukari duniani hii leo ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio kila uchao na sasa inaelezwa kuwa watu Milioni 350 duniani, sawa na asilimia Tano ya wakazi wote wana ugonjwa wa kisukari na idadi inatarajiwa kuongezeka. Ujumbe wa siku hii ni eneza ufahamu kuhusu Kisukari na kinga dhdi yake. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mipango kukabiliana na athari zisizoepukika za mabadiliko ya hali ya hewa inafanywa:UNFCCC

Kusikiliza / Kimbunga

Wakati wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wanakutana Warsaw, Poland kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa, nchi masikini kabisa duniani zinakamilisha mipango ya kukabiliana na athari zisizoepukika za mabadiliko ya hali ya hewa . Mikakati hiyo inasaidiwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC, kitengo cha kimataifa [...]

14/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mchezo wa baiskeli ni mtaji wa mshikamano Rwanda

Kusikiliza / Rising-from-Ashes

Rwanda, taifa ambalo lilitatizika kwa mauaji ya halaiki takribani miaka 20 iliyopita, sasa liko katika mchakato wa utangamano. Hatua hii jumuishi inahitaji sekta zote kuwajibika, na hii ndio sababu ya kuanzisha mchezo wa basikeli wenye lengo la kuwaweka vijana  na kamundi mbalimbali pamoja bila kujali tofauti zao.  Ungana na Joseph msami katika makala inayomulika filamu [...]

14/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Tuchukue hatua mapema kudhibiti ugonjwa wa Kisukari: Ban

Kusikiliza / Moja ya Kliniki ya Kisukari nchini Tanzania

Novemba 14 kila mwaka ni siku ya Kisukari duniani ambapo katika salamu zake kwa mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon  amehadharisha juu ya ongezeko la idadi ya wagonjwa hususan watoto, vijana na watu maskini. Amesema takribani watu Milioni 350 duniani waugua Kisukari na licha ya kwamba watu wako hatarini kurithi ugonjwa [...]

14/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tangazo la Israel la ujenzi wa makazi mapya litaweka njia panda suluhu ya amani:Serry

Kusikiliza / Robert Serry

Mratibu wa Umoja wa mataifa kwa masuala ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Bwana Roberty Serry amesema amekuwa akifuatilia kwa hofu matangazo ya Israel ya ujenzi wa makazi mapya yaliyotolewa wiki chache zilizopita , ambayo anasema hayaendi sambamba na lengo la kuwa na hatma ya suluhu ya mataifa mawili. Bwana Serry amesema msimamo [...]

13/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Makosa kwenye mikataba ya awali kuhusu mabadiliko ya tabianchi kuepukwa: Dokta Muyungi

Kusikiliza / Dr. Richard Muyungi

Wataalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi wanaendelea na kikao chao huko Warsaw Poland, matarajio ni kufikiwa makubaliano mapya ifikapo mwaka 2015 kuhusu hali ya hewa kwa mustakhbali endelevu wa dunia, wakati huu ambapo madhara yatokanayo na mabadiliko hayo hayachagui nchi maskini wala tajiri. Dokta Richard Muyungi, ni Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya Kisayansi [...]

13/11/2013 | Jamii: Mahojiano, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

IAEA kujadili ongezeko la asidi baharini katika mkutano wa Warsaw

Kusikiliza / ocean acid2

Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, linaandaa mjadala kuhusu kuongezeka kwa viwango vya asidi baharini mnamo Novemba 18, pembezoni mwa mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ambao unaendelea mjini Warsaw, Poland. Jopo la wataalam litajadili hali hii inayotia hofu kimataifa, na ambayo inahatarisha uhai wa viumbe wote wa baharini, na wote wanaoyategemea [...]

13/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2013 watajwa kuwa kati ya miaka yenye joto jingi zaidi duniani

Kusikiliza / Kimbunga Haiyan

Mwaka 2013 unaelekea kuwa kati ya miaka kumi iliyo na viwango vya juu zaidi vya joto kuwai kuandikishwa tangu kuanza kunakiliwa kwa takwimu hizo mwaka 1850 kwa mujibu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) Kupitia kwa ripoti yake shirika la utabiri wa [...]

13/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Plumbly azuru wakimbizi wa Syria Bekaa Lebanon:

Kusikiliza / Derek Plumbly

Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon Derek Plumbly, leo amezuru maeneo ya Zahleh na Joub Jennin Magharibi mwa bonde la Bekaa nchini Lebanon ili kuangalia hali ya wakimbizi wa Syria na jamii inayowahifadhi. Mratibu huyo pia amekwenda kufuatilia juhudi za shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR na serikali [...]

13/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO na WHO waandaa mkutano kuhusu lishe bora

Kusikiliza / fao nutrition

Tatizo la lishe kwa sasa ni changamoto kwa zaidi ya nusu ya watu duniani ambapo mifumo ya chakula inatakiwa kufanyiwa mabadiliko kwa minajili ya kuboresha lishe pamoja na maisha. Haya ni baadhi ya yaliyozungumziwa wakati wa ufunguzi wa mkutano uliondaliwa na shirila la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO kwa ushirikiano na shirika [...]

13/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muungano wa Afrika wapongeza azimio la Baraza la Usalama la UM

Kusikiliza / Annadif

Mwakilishi maalum wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, Balozi Mahamat Saleh Annadif ameunga mkono azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa MAtaifa la kuongeza muda wa vikosi vya muungano huo nchini Somalia, AMISOM hadi Oktoba mwaka 2014, pamoja na kuongeza usaidizi kwa jeshi la nchi hiyo. Alice Kariuki na taarifa kamili (RIPOTI YA ALICE [...]

13/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara ya hewa ya Ukaa yadorora, kupatiwa msukumo mpya

Kusikiliza / COP 19

Kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi kinaendelea mjini Warsaw, Poland, jitihada ikiwa ni kuibuka na makubaliano mapya yatakayokuwa jumuishi kuliko ya awali kama Kyoto ambayo hayajaweza kudhibiti uchafuzi wa mazingira duniani. Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya Kisayansi na Taaluma ya mkataba huo Dk. [...]

13/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpango mpya kuboresha huduma za uzazi wa kupanga baada ya kujifungua mimba: WHO

Kusikiliza / Unyonyeshaji mtoto baada ya kujifungua ni mojawapo ya njia za uzazi wa mpango- WHO

Shirika la Afya Duniani, WHO, limezindua mpango mpya wa kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa kupanga kwa akina mama katika miezi 12 ya kwanza baada ya kujifungua, ambao unawalenga wahudumu wa afya na watunga sera. Kwa mujibu wa WHO, mimba zinazokaribiana sana au zisizotarajiwa ni tishio la kiafya kwa mama na mtoto, na kwamba [...]

13/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati misaada inaendelea kuwasili Ufilipino kuwafikia walengwa bado ni changamoto:

Kusikiliza / typhoon

Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, kimataifa na wadau wengine wanaendelea kupeleka watu na misaada nchini Ufilipino lakini kuwafikia walengwa bado ni changamoto, kwani miundombinu imeharibika vibaya na mawasiliano ni shida. Flora Nducha na taarifa kamili (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Timu ya shirika la afya duniani WHO na wahudumu wengine wamewekwa tayari kupelekwa kwenye maeneo [...]

13/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uzalishaji wa afyuni Afghanistan wapanda kwa asilimia 36

Kusikiliza / opium_poppy1

Upandaji wa afyuni nchini Afghanistan ulipanda kwa asilimia 36 mwaka huu, ambacho ni kiwango cha juu zaidi, kwa mujibu wa ripoti ya utafiti katika upandaji mmea huo unaotumiwa kutengeneza dawa haramu za kulevya, ambayo imetolewa leo mjini Kabul na wizara ya kukabiliana na dawa za kulevya na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na dawa [...]

13/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yawapatia mafunzo wakimbizi wa DR Congo nchini Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi wa DRC nchini Uganda

Huko nchini Uganda, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeanza kuwapatia wakimbizi wapya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walioko kambi ya kambi ya Kyangwali mafunzo kuhusu haki zao ikiwemo ile ya ulinzi wa kimataifa pamoja na sheria. Hatua hiyo inakuja baada ya shirika hilo kubaini kuwa wakimbizi hao hawafahamu lolote [...]

13/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maji utapiamlo vyapata suluhu Ethiopia

Kusikiliza / Maji Ethiopia

Maji yamekuwa ni kitendawili ambacho hakina jibu nchiniEthiopiakwa muda mrefu hususani maeneo ya vijijini. Huduma ya lishe nayo si shwari. Katika jamii yenye changamotokamahizo maisha huwa kizungumkuti. Lakini waswahili alisema nyota njema huonekana asubuhi, na hiki ndicho kilichotokea hukoEthiopia. Kufahamu undani wa hatma ya huduma hizi, ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

12/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Nchi 14 zaungana na wenzao katika ujumbe wa Baraza la Haki za Binadamu

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu John Ashe

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo pamoja na majukumu mengine lilikuwa na kazi ya kuchagua wajumbe 14 wa Baraza la Haki za binadamu watakaohudumu kwa miaka mitatu kuanzia mwezi Januari mwakani. Uchaguzi huo umefanyika ili kuziba nafasi hizo zitakazoachwa wazi pindi nchi 14 zitakapomaliza ujumbe wao mwishoni mwa mwaka huu. Rais wa Baraza Kuu [...]

12/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Usimamizi mzuri unakwenda sambamba na uhamiaji mzuri

Kusikiliza / Msemaji wa IOM, Jumbe Omari Jumbe

Maafisa wa uhamiaji wa kutoka Sudan Kusini walisafiri hadi Tanzani kushiriki katika mafunzo yaliotolewa na Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM . Mafunzo hayo yalilenga kuwafunza kuhusu njia bora za kudhibiti mipaka na pia kuwakutanisha na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania. Assumpta Massoi wa Idhaa hii aliongea na msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe ambaye [...]

12/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya watoto syria yalaaniwa

Kusikiliza / Nembo ya UNICEF

Mauaji ya watoto wasio na hatia yameendelea nchini Syria ambapo tukio la hivi karibuni zaidi ni la vifo vya watoto watano walioripotiwa kuuwawa wakiwa darasani baada ya kombora kushambulia shule iitwayo St. John iliyoko Damascus. Katika tukio hilo watoto kumi na mmoja walijeruhiwa Katika tukio jingine siku hiyo hiyo watoto wanne pamoja na dereva mmoja [...]

12/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa AMISOM nchini Somalia

Kusikiliza / Mwakilishi wa kudumu wa Somalia, UM Balozi Dk. Elmi Ahmed Dual

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na vikao vya wazi na faragha vikimulika hali ilivyo nchini Somalia wakati huu ambapo serikali inajitahidi kuimarisha usalama ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Novemba Balozi Liu Ji Ye [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yafanikiwa kufikisha chakula Al Rastan Syria:

Kusikiliza / WFP yawasilisha chakula eneo la, Al Rastan Syria

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP Ijumaa lilifanikiwa kufikisha msafara uliosheheni msaada wa mashirika mbalimbali wa chakula katika eneo la Al Rastan jimbo la Homs nchini Syria. Msaada huo unagawanywa na chama cha msalaba mwekundu cha nchi hiyo . Msafara huo ulijumuisha malori 9 yaliyokuwa yamebeba vifurishu 5000 vya mgao wa chakula unaotosheleza kulisha [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yatoa ombi la dola milioni 24 kugharamia misaada nchini Ufilipino.

Kusikiliza / Kimbunga Haiyan kimeathiri kilimo

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linakusanya misaada kwa ajili ya waathiriwa wa kimbunga Hayian kilichoikumba Ufilipino na kusababisha uharibifu mkubwa kwa sekta nyingi ikiwemo ya kilimo ambapo pia watu wengi walipoteza maisha. Mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva amesema kuwa shirika hilo limesimama na kuonyesha uzalendo kwa watu [...]

12/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Pneumonia wangoza kwa vifo miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano duniani

Kusikiliza / Mtoto apokea chanjo dhidi ya uginjwa wa Pneumonia,malawi

Ugonjwa wa Pneumonia unaongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano duniani ambapo husababisha zaidi ya vifo milioni moja kila mwaka. Lakini hata hivyo vifo hivyo vinaweza kuzuiwa. Taarifa kamili na Flora Nducha (Taarifa ya Flora Nducha)  Huku nchi zikiadhimisha siku ya ugonjwa wa Pneumonia duniani hii leo muungano [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watoa ombi la dola milioni 300 kuwasaidia waathiriwa wa kimbunga Ufilipino

Kusikiliza / Madhara ya kimbunga Haiyan

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola milioni 301 zinakazotumika kufadhili misaada ya kibinadamu kwenye maeneo yaliyokumbwa na kimbunga nchini Ufilipino. Karibu watu milioni 11 wameathiriwa na kimbunga hicho huku  watu 700,000 wakilazimika kuhama makwao. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya  Grace Kaneiya) Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye maeneo yaliyoathiriwa yanasema kuwa chakula, [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zambia yaingia kipindi muhimu katika vita dhidi ya Ukimwi

Kusikiliza / Ujumbe wa PCB wahudhuria mafunzo ya afya ya uzazi katika shuke ya msingi, Lusaka

Shirika la Umoja wa Mataifa linaohusika na mapambano dhidi ya Ukimwi, UNAIDS limesema Zambia iko katika hatua muhimu zaidi dhidi ya ugonjwa huo ambapo limesema nchi hiyo haipaswi kubweteka na mafanikio ilipata. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Jan Beagle amesema hayo mwishoni mwa ziara ya siku tatu ya ujumbe alioongoza kwenye nchi hiyo ambako takribani [...]

12/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maafisa wa Sudan Kusini wajifunza masuala ya uhamiaji nchini Tanzania:IOM

Kusikiliza / Maafisa wa Uhamiaji kutoka Sudan Kusini wakiwa na wenzao kutoka Tanzania

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha mafunzo ya siku sita yaliyowaleta maafisa wa uhamiaji kutoka Sudan Kusini hadi nchini Tanzania kujifunza kuhusu njia bora za kudhibiti mipaka na pia kukutana na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania. Wawakilishi sita kutoka serikali ya Sudan Kusini idara ya uraia, pasi za kusafiria na uhamiaji (DNPI) akiwemo mkurugenzi [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaonya kuhusu athari na mahitaji ya kiafya Ufilipino

Kusikiliza / Waathirika wa kimbunga Haiyan (picha ya AP) W.Santana

Shirika la Afya Duniani WHO, limesema linapeleka wataalamu wa afya kwenye maeneo yaloathiriwa na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino ili kusaidia kurejesha huduma za afya. WHO imesema vituo vingi vya afya viliharibiwa kabisasa, na vile ambavyo vimesalia vimebanwa kwa mahitaji, huku uhaba wa vifaa vya afya ukishuhudiwa. Tayari matabibu kutoka Ubeljiji, Japan, Israel, na Norway wamepelekwa [...]

12/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Takribani wajawazito 200,000 wahitaji msaada Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan: UNFPA

Kusikiliza / Emily akifarijiwa na mumewe baada ya kujifungua salama

Madhara ya kimbunga Haiyan nchini Ufilipino yanazidi kuwa dhahiri shairi kila uchao ambapo Shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA limemulika afya ya uzazi ikisema wajawazito Laki mbili wanahitaji msaada wa haraka baada ya kuathirika na kimbunga hicho. Taarifa ya shirika hilo limetolea mfano mjamzito mmoja huko Tacloban City ambaye alilazimika kujifungulia [...]

12/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alihutubia Baraza Kuu baada ya kuhitimisha ziara yake Sahel

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelihutubia Baraza Kuu leo Jumatatu, baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye ukanda wa Sahel, hotuba hiyo ikianza kwa kutoa risala za rambi rambi na pole kwa serikali na watu wa Ufilipino kufuatia janga la kimbunga Haiyan. Kuhusu eneo la Sahel, Bwana Ban amesema ujumbe wake yeye na [...]

11/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Utashi na uzingativu wa serikali unaweza kukabiliana na ukatili wa kingono DRC: Bangura

Kusikiliza / Hawa Bangura

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono katika maeneo ya vita, Zainab Hawa bangura, amekaribisha tangazo la Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC la hatua mpya za kukabiliana na ukatili wa kingono nchini humo. Ameelezea pia kufurahishwa na tangazo la Rais Kabila la Oktoba 23 kwa wabunge kuwa [...]

11/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa UM wasikitikia mkwamo wa mazungumzo ya Kampala

Kusikiliza / Mary Robinson

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu nchi za Maziwa Makuu, Mary Robinson, Mwakilishi wa Marekani kwenye nchi hizo na DRC, Russ Feingold, Mwakilishi wa Umoja wa Afrika, AU, Boubacar Diarra na Mwakilishi wa Muungano wa Ulaya, EU Koen Vervaeke, pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu katika DRC, Martin Kobler, wametoa taarifa ya kuelezea masikitiko yao [...]

11/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yapigia chapuo afya ya mama na mtoto India

Kusikiliza / Afya India

Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na serikalai ya India linasaidia kuinua sekta ya afya nchini humo hususani kwa kina mama na watoto. UNICEF imewekeza katika raslimali watu na vifaa  na kuleta mabadiliko makubwa. Joseph Msami anafafanua vyema katika makal ifuatayo.

11/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNHCR Kutumia ndege kusaidia waathirika wa kimbunga Typhon nchini Ufilipino

Kusikiliza / Uharibifu uliofanyika baada ya kimbunga typhoon

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetangaza leo kwamba linatoa msaada wa huduma za dharura kwa kutumia ndege nchini Ufilipino ambapo inakadiriwa watu milioni 9.8 wamethiriwa na kimbunga Typhhon kilichoikumba nchi hiyo wiki iliyopita. Taarifa ya shirika hilo imemkariri Kamishana Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres akisema ingawa shirika lake hufanya kazi zihusuzo [...]

11/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Upungufu wa wafanyakazi sekta ya afya ni dhahiri, tumechukua hatua:Tanzania

Kusikiliza / Dk Rashid

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO inasema dunia itakuwa na upungufu wa wafanyakazi milioni 12.9 katika sekta ya afya ifikapo mwaka 2035, huku kwa sasa  upungufu huo ni milioni 7.2, . Serikali yaTanzaniainakiri upungufu huo kuikabili sekta ya afya na kuelezea mikakati iliyopo katika kukabilina na upungufu wa wafanya kazi wa sekta ya [...]

11/11/2013 | Jamii: Mahojiano, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa huduma kwa waathiriwa wa tufani nchini Ufilipino

Kusikiliza / Athari za kimbunga Haiyan, Ufilipino

Shirika la afya duniani WHO limendaa mikakati kwa ushirikono na idara ya afya nchini Ufilipino katika jitihada za kuwasaidia wale walioathiriwa na tufani Haiyan. Tufani inayofahamika miongoni mwa wenyeji kama Yolanda ilikumba eneo la kati la Archipelago siku ya Ijumaa asubuhi ikiwa na upepo uliovuma kwa kasi ya kilomita 250 kwa saa. Watu wanaoishi kwenye [...]

11/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya ICJ yaikabidhi Cambodia hekalu la Preah Vihear

Kusikiliza / Mahakama ya ICJ

Mahakama ya dunia, ICJ, ambayo ndicho kiungo cha sheria cha Umoja wa Mataifa, imetoa uamuzi wake kuhusu kesi iloamuliwa mnamo Juni 15 mwaka1962 kati ya Cambodia na Thailand kuhusu hekalu la Preah Vihear. Ingawa iliamuliwa mnamo mwaka 1962 kuwa hekalu hilo lilikuwa kwenye ardhi ya Cambodia, bado kulikuwa na hali ya kukanganisha kuhusu vipengee fulani [...]

11/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Gesi chafu na majanga vyamulikwa kwenye mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / climate-change1

Kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi umeanza leo mjini Warsaw, Poland, ambako viwango vya gesi ya kaboni angani na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi vimemulikwa. Joshua Mmali na taarifa kamili TAARIFA YA JOSHUA Akiufungua mkutano huo, Katibu Msimamizi wa mkataba wa Umoja wa [...]

11/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya, Somalia, UNHCR, zatia saini makubaliano ya wakimbizi

Kusikiliza / Wakimbizi wa Somalia nchini Kenya

Serikali ya Kenya na Somalia kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR, leo zimesaini makubali noayeney lengo la kuanzisha msaada wa kisheri ana mingineyo kwa wakimbizi wa Somalia walioo nchini Kenya ambao kwa hiari yao watataka kurejea nchini mwao. Makubaliano hayo ambayo hayaweki ukomo wa kurejea makwao yanaeleza wajibu wa pande [...]

11/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sekta ya afya yakabiliwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi: WHO

Kusikiliza / Wahudumu afya

Dunia itakuwa na upungufu wa wafanyakazi milioni 12.9 katika sekta ya afya ifikapo mwaka 2035 huku kwa sasa upungufu huo ukiwa ni milioni 7.2 limesema shirika la afya duniani WHO. WHO inaonya kwamba ikiwa hatua za kuridhisha hazitachukuliwa dhidi ya utafiti huo madahara yake yatakuwa makubwa kwa afaya za mabailioni ya watu duniani kote. Taarifa [...]

11/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yaendelea kupeleka misaada kwa waathirika wa kimbunga Ufilipino:

Kusikiliza / Hurrican Haiyan

Mashirika ya Umoja wa mataifa yanendelea kupeleka misaada ya kibinadamu kwa mamilioni ya watu waklioathirika na kimbunga Haiyan au Yolanda kilichoikumba Ufilipino. Grace Kaneiya na taarifa kamili (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Kwa mujibu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP watu milioni 9.5 wameathirika na kimbunga hicho huku 400,000 wakitawanywa na kimbunga hicho na [...]

11/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA na Iran zatangaza utaratibu wa ushirikiano

Kusikiliza / Yukiya Amano IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, Yukiya Amano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Iran, wametoa tangazo la pamoja la makubaliano ya utaratibu wa ushirikiano kuhusu suala la mpango nyuklia nchini Iran. Tangazo hilo limesema IAEA na Iran zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wao na mazungumzo yenye lengo la kuhakikisha mpango [...]

11/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban aendelewa kutiwa hofu na athari za kimbunga nchini Ufilipino:

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema anaendelea kutiwa hofu na athari za kimbunga Haiyan ambacho ni moja ya vimbunga vikubwa kuwahi kutokea. Kimbunga hicho kimeathiri takriban watu milioni 9.5 nchini Ufilipino , huku kikisababisha uharibifu mkubwa , kutawanya watu na ukatili maisha ya watu wengi wakati idadi ya waliokufa ikitarajiwa kuongezeka. Hivi [...]

11/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani shambulio la kigaidi Somalia

Baraza la Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la bomu lililofanyika Ijumaa kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, shambulio ambalo kundi la kigaidia la Al-Shabaab limedai kuhusika nalo na limesababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi. Taarifa ya baraza hilo imekariri wajumbe wakituma salamu za rambirambi kwa familia na wananchi pamoja [...]

09/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kusaidia serikali y Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan

Watoto nchini Ufilipino wahitaji msaada

Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaimarisha operesheni zake nchini Ufilipino , na kupeleka msaada wa dharura kuisaidia serikali kutoa msaada kwa walioathirika na kimbunga Haiyan au Yolanda kama kinavyojulikana katika nchi hiyo. Maafisa wa WFP wameungana na timu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Ufilipino ili kutathimini [...]

09/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na athari za kimbunga Haiyan Ufilipino:

Waokoaji wakisaidia waathirika wa kimbunga Haiyan huko Ufilipino

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amestushwa na kusikitishwa na athari kubwa zilizosababishwa na kimbunga Haiyan au Yolanda ambapo watu wengi wamepoteza maisha na miundombinu kuharibiwa vibaya. Ban ametuma salamu za rambirambi kwa watu na serikali ya Ufilipino hususani kwa waliopoteza ndugu na jamaa, nyumba zao au kuathirika kwa aina yoyote na [...]

09/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waathirika wa kimbunga Haiyan Ufilipino wasaidiwe :Amos

Mkuu wa OCHA, Bi. ,Valerie Amos

Mratibu mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja waMataifa Bi Valarie Amos amesema amestushwa sana na ripoti za vifo vya watu na uharibifu mkubwa uliosababishwa na kimbunga Haiyan au Yolanda huko Ufilipino. Amesema kuna idadi tofauti ya waliopoteza maisha ikiwemo ile ya chama cha msalaba mwekundu ambayo kwa sasa ni 1200, [...]

09/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usafirishaji wa fedha Somalia wahofiwa kuwezesha uharamia

Kusikiliza / Mogadishu

Taifa la Somalia likiwa linapiga hatua za kukuza uchumi wake baada ya takribani miongo miwili ya vita, uharamia nao ni changamoto kubwa inayoikabili nchi hiyo. Joseph Msami anaangazia utumaji wa fedha na athari zake katika uharamia nchini humo. Ungana naye katika makala ifuatayo.

08/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Botswana na Rwanda zatoa msukumo wa kufanyia marekebisho Baraza la Usalama

Kusikiliza / Charles Thembani Ntwaagae, Mwakilishi wa kudumu Botswana

Mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Baraza la Usalama umeingia siku yake ya pili, hukuRwanda na Botswana zikiongeza sauti zao kwa wito wa kutaka Baraza la Usalama lifanyiwe marekebisho. Akiongea wakati wa mjadala huo, Mwakilishi wa Kudumu wa Botswanakwenye Umoja wa Mataifa, Charles Thembani Ntwaagae amesema ujumbe waBotswanaunaazizia mno suala la kulifanyia [...]

08/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wa Utalii wataka uboreshaji wa sera kati ya utalii na usafiri wa angani

Kusikiliza / Utalii

Mawaziri wa Utalii kutoka kote duniani wametaka uboreshwe utandawazi wa angani kwa kuweka uratibu mzuri wa sera za utalii na usafiri wa angani ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa sekta hizo za utalii na usafiri wa angani. Hayo yamejitokeza katika mkutano wa kila mwaka wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, WTO na Shirika [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wasikatishwe tamaa; washirikisheni kwenye utunzi wa sera: Birungi

Kusikiliza / vijana wajasiriamali

Baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa na kamati ya fedha na uchumi ya Baraza Kuu la umoja huo kwa pamoja wameendesha mkutano kuhusu hatma ya ajira duniani na fursa mwaka 2030 ambapo miongoni mwa mambo yaliyomulikwa ni mustakhabali wa ajira kwa vijana wakati huu ambapo kuna kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia. [...]

08/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bi Ameerah Haqm azuru jimbo la Unity Sudan Kusini

Kusikiliza / Ameerah Haqm

Mkuu wa idara inayohusika na maslahi ya walinzi wa amani na wahudumu wa kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Ameerah Haqm amefanya ziara kwenye jimbo la Unity, Sudan Kusini kufanya tathmini ya ujumla ya hali ya mambo. Akiwa katika jimbo hilo, Bi Haqm amekutana na kupewa maelezo na wawakilishi wa serikali kuhusu marekebisho ya katiba, upokonyaji [...]

08/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Suala la vyoo bora lasalia utata duniani, huko Ruvuma Tanzania baadhi wachukua hatua

Kusikiliza / world_toilet_day

Tarehe 17 Novemba imetengwa kuanzia mwaka huu kuwa siku ya choo duniani. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha uamuzi huo mwezi Julai mwaka huu. Sababu hasa ni kuhakikisha suala la usafi wa vyoo na mazingira linapatiwa kipaumbele kwenye ajenda ya maendeleo endelevu. Umoja wa Mataifa unasema cha kustaajabisha ni kwamba dunia ina watu zaidi [...]

08/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watoto Mashariki ya Kati kupewa chanjo dhidi ya polio

Kusikiliza / mtoto apokea chanjo

Zaidi ya watoto milioni 20 katika nchi saba na maeneo ya Mashariki ya Kati wanapewa chanjo dhidi ya polio, kufuatia kulipuka kwa ugonjwa huo wa kupooza nchini Syria. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Shirika la Afya Duniani, WHO na lile la Kuhudumia Watoto, UNICEF yanaongoza kampeni hiyo ya utoaji wa chanjo. [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufisadi upigwe vita mitaani hadi vyumba vya mikutano: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon ataka ufisadi ukomeshwe

Transparency International, taasisi ya kimataifa inayotetea uwazi imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameitumia pongezi akisema kupitia ubia wake na taasisi nyingine ukiwemo Umoja huo limesaidia kusongesha vita dhidi ya ufisadi kwenye nchi tajiri na maskini. Salamu za Ban zimesema ufisadi hauipaswi kugharimu biashara, bali ni [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ghasia nchini Jamhuri ya Afika ya kati huenda zikafikia hali isiyoweza kudhibitika:PILLAY

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameonya kuwa uvamizi na ghasia zinazoendelea kushuhudiwa kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati huenda ikalitumbukiza taifa hilo kwenye mzozo mpya . Jason Nyakundi na taarifa kamili. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)  Mnamo tarehe 26 mwezi Oktoba wanamgambo wanaofahamika kama anti-Balaka walivamia na kuteka mji [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati wa kuchukua hatua ni sasa asema Ban akihitimisha ziara Sahel:

Kusikiliza / Katibu Mkuu zairani Ukanda wa Sahel, akiondoka Mali

Umewadia wakati wa kuachana na maneno na kuanza kutekeleza kwa vitendo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaambia maafisa wa serikali ya Chad mjini N’Djamena alipokuwa akihitimisha ziara yake katika ukanda wa Sahel kwa mujibu wa André-Michel Essoungou, afisa wa Umoja wa mataifa anayesafiri pamoja na Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Bwana Ban amepokea ushirikiano mkubwa [...]

08/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wafanyika Hoima, Uganda kuweka mazingira bora kwa wakimbizi: UNHCR

Kusikiliza / Wakati wa mkutano uliofanyika Hoima, Uganada

Hatimaye Shirika la Umoja wa Mataifa kuhudumia wakimbizi la (UNHCR) eneo la magharibi ya kati mwa Uganda, limefanikisha mkutano wa wa wakimbizi wapya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) uliokuwa na lengo la kuleta mshikamano zaidi kati ya serikali ya Uganda, shirika hilo na mashirika mengine ili wakimbizi wapate huduma bora licha ya idadi [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mvua kubwa zilizoikumba Cambodia zaanza kumalizika

Kusikiliza / Mfanayakazi wa IOM, Cambodia

Wakati maji yaliyojaa katika majimbo mengi yameaanza kutoweka na msimu wa mvua kuelekea kumalizika, mafuriko mabaya kabisa yaliyoathiri Cambodia tangu mwezi septemba yanaonekana kumalizika limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Kwa mujibu wa shirika hilo mvua kubwa zilisababisha mto Mekong kufurika na kuwaathiri watu zaidi ya milioni 1.7, vikiwemo vifo 188 katika majimbo 20 [...]

08/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kimbunga Haiya chapiga Ufilipino UM wasaidia:WMO/OCHA

Kusikiliza / Kimbunga

Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO linasema kimbunga Haiyan kimepiga Ufilipino na kuelezwa kuwa  ni kikubwa na cha kasi sana, na tayari kimeshasababisha uharibifu mkubwa. Assumpta Massoi na ripoti kamili. Kimbunga hicho kinavuma kwa kasi ya kilometa 215 kwa saa na kimeambatana na mvua kubwa. Umoja wa Mataifa unaisaidia serikali ya Ufilipino [...]

08/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu imekaribisha kupiga mweleka kwa kundi la M23 DR Congo:

Kusikiliza / Kundi la waasi M23

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa Ijumaa imekaribisha kitendo cha kushindwa kwa kundi la waasi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa mujibu wa ofisi hiyo kiongozi wa kundi hilo Sultani Makenga ambaye alijisalimisha nchini Uganda ametajwa kuwa ni mmoja wa wakiukaji wakubwa wa haki za binadamu. Na ofisi hiyo [...]

08/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Juan Somavia kuwa Mshauri wake kuhusu ushirikiano wa kikanda kuhusu sera

Kusikiliza / Juan Somavia ILO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bwana Juan Somavía wa Chile kuwa Mshauri wake Maalumu kuhusu ushirikiano wa kikanda kuhusu sera. Bwana Somavía ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ajira, ILO, atasaidia kuweka mkakati wa miaka miwili wa ushirikiano wa kisera kuhusu masuala fulani muhimu miongoni mwa tume za kikanda [...]

07/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asifia mazungumzo ya amani Colombia

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amekaribisha tangazo lililofanywa jana na serikali ya Colombia na Kundi lililojihami la mapinduzi la FARC kuwa wamefikia makubaliano kuhusu kushirikishwa kisiasa kwa kundi hilo, katika mazungumzo yanayoendelea mjini Havana, Cuba. Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ametilia mkazo umuhimu wa uaminifu na mbinu [...]

07/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jeshi la DR Congo sasa ladhibiti maeneo yote yaliyokuwa chini ya M23

Kusikiliza / Wanawake na watoto huko Rutshuru, DR Congo wakifurahia baada ya kijiji chao kukombolewa na askari wa serikali kwa usaidizi wa MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo, MONUSCO umethibitisha kuwa jeshi la nchi hiyo hivi sasa linadhibiti maeneo yote ambayo awali yalikuwa chini ya kundi la waasi la M23. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa MONUSCO iliunga mkono hatua za jeshi hilo kwa kutimiza wajibu [...]

07/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM-OPCW wathibitisha eneo lililokuwa bado kukaguliwa Syria

Kusikiliza / Msafara wa wakaguzi wa UM-OPCW huko Syria

Hatimaye ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la kupinga matumizi ya silaha za kemikali, wameweza kuthibitisha eneo moja kati ya mawili nchini Syria ambayo awali wakaguzi hawakuweza kufika kutokana na sababu za kiusalama.  Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari hatua hiyo ya karibuni huko Aleppo [...]

07/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP yakaribisha hatua ya Marekani kuridhia mkataba kuhusu zebaki:

Kusikiliza / Mercury

Marekani imepiga jeki juhudi za kimataifa za kupunguza gesi chafuzi itokanayo na metali nzito baada ya kuridhia mkataba wa Minamata kuhusu zebaki. Mkataba huo uliopitishwa tarehe 10 Oktoba nchini Japan na kupewa jina la mji ambao maelfu ya watu walidhurika na sumu ya zebaki katikati ya karne ya 20 sasa umetiwa saini na nchi 93. [...]

07/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Usafi wa Mazingira waangaziwa Nepal

Kusikiliza / Usafi wa mazingira waangaziwa,Nepal

Muziki unasikika katika sherehe rasmi ilioandaliwa Nepal kwa sababu ya hatua zilizopigwa swala la usafi wa mazingira. Watoto kwa wakubwa wamejumuika pamoja kusherehekea . Hili ni eneo la hivi karibuni zaidi Nepal kutajwa kuzingatia swala la usafi wa mazingira. Hii ni sehemu ya kampeni inayohimiza watu kutumia vyoo na kuzingatia usafi Hapa tunakutana na mwakilishi [...]

07/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNFPA yafanikisha ujenzi wa kituo cha elimu ya uzazi Haiti

Kusikiliza / Haiti unfpa

Kumeanza kujitokeza hatua ya kutia matumaini nchini Haiti iliyokumbwa na mafuriko makubwa mwaka 2010 ambayo yalivuruga miundo mbinu ikiwemo shule na huduma nyingine za kijamii.  Tayari Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu limefanikisha ujenzi wa baadhi ya nyumba ikiwemo hospitali na shule jambo ambalo limetoa matumaini makubwa kwa wananchi wa eneo [...]

07/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

AU yaipongeza Somalia kwa kuanza mazungumzo ya amani

Kusikiliza / Mahamat Saleh Annadif

Mwakilishi wa mwenyekiti wa kamishna ya Umoja wa Afrika kwa Somalia balozi Mahamat Saleh Annadif ametuma salama za pongezi kwa serikali ya nchi hiyo na watu wake kwa kufanikisha mkutano wa maridhiano kuhusiana na eneo la Juba. Balozi Annadif amesema kuwa anamatumaini makubwa kuhusiana na hatua iliyofikiwa na wananchi wa taifa hilo ambao wamedhamiria kupiga [...]

07/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lajadili ufanyiaji Baraza la Usalama Marekebisho

Kusikiliza / Vandi Chidi Minah

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili suala la kulifanyia marekebisho Baraza la Usalama, ambalo limekuwa likizua utata katika mijadala mingi ya Umoja wa Mataifa. Joshua Mmali na taarifa kamili TAARIFA YA JOSHUA Suala la kutaka kufanyia marekebisho Baraza la Usalama limekuwa likiibuka katika vikao vingi vya mijadala mikuu ya Baraza Kuu. Leo [...]

07/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNEP yakaribisha hatua ya Marekani kuridhia mkataba kuhusu zebaki:

Kusikiliza / MERCURY TREATY

Marekani imepiga jeki juhudi za kiamataifa za kupunguza gesi chafuzi itokanayo na metali nzito baada ya kuridhia mkataba wa Minamata kuhusu zebaki. Mkataba huo uliopitishwa tarehe 10 Oktoba mjini Kumamoto Japan na kupewa jina la mji ambao maelfu ya watu walidhurika na sumu ya zebaki katikati ya karne ya 20 sasa umetiwa saini na nchi [...]

07/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yatabiri kuongezeka kwa uzalishaji wa chakual na kushuka kwa bei

Kusikiliza / food-prices

Bei ya vyakula inataraajiwa kushuka ikilinganishwa na miaka iliyopita hali ambayo imechangiwa na kuongezeka kwa uzalishaji hasa wa nafaka kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO. Jason Nyakundi na ripoti kamili., (Ripoti ya Jason) Bei ya vyakula kuu imeshuka miaezi michache iliyopta hali ambayo imetokana na [...]

07/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ITU na INTEL zaingia ubia kuleta mabadiliko kwenye elimu

Kusikiliza / ITU and education

Kampuni mashuhuri ya utengenezaji wa chipu za kompyuta, INTEL imeungana na Shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU katika kupanua wigo wa matumizi ya teknolojia ili kuleta mabadiliko kwenye sekta ya elimu katika nchi zinazoendelea. Katibu Mtendaji wa ITU Hamadoun I. Touré amesema ubia huo wakati wa jukwaa la siku nne la teknolojia ya mawasiliano litakalofanyika [...]

07/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aitaka Burkina Faso kupambana na mabadiliko ya tabia nchi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiwa na Waziri Mkuu wa Bukirna Faso Luc-Adolphe Tiao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon akiwa angali ziarani katika ukanda wa Sahel amekutana na kuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu Luc-Adolphe Tiao na baraza la mawaziri la Burkina Faso ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia mabadiliko ya tabianchi kama miongoni mwa changamoto kuu zinazoikumba nchi hiyo na kutaka nguvu za pamoja katika [...]

07/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muswada wa haki ya faragha kuwasilishwa UM

Kusikiliza / INTERNET

Kutoheshimiwa kwa haki ya faragha ndiko kumetusukuma kupeleka muswada wa azimio hili, amesema Christian Doktor ambaye ni msemaji wa ubalozi wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa. Katika mahojiano na Monica Graylay wa idhaa ya Kireno ya Umoja wa Mataifa Bwana Christaian amesisistiza imani yake juu ya uungwaji mkono kwa azimio hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ujerumani [...]

06/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Majanga ya wahamiaji yanamulika haja kubadili sera: ILO

Kusikiliza / Walionusurika kifo mkasa wa Lampedusa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Ajira, ILO, Guy Ryder, ametoa wito wa kufanywa mabadiliko ya kina katika sera za uhamiaji ili kuepukana na majanga kama yale ambayo huwaua mamia ya wahamiaji wanapjaribu kufika ulaya, wengi wao wakitoka Afrika. Akizungumza wakati wa kongamano la siku tano la kujadili uhamiaji, likiwemo suala la haja ya [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutumie fursa ya yaliyojiri DR Congo kuleta amani ya kudumu: Baraza la Usalama

Kusikiliza / Balozi Atoki Ileka

Habari ni njema kutoka DR Congo ambako yathibitishwa kuwa waasi wa M23 wametangaza rasmi kusitisha uasi wao, na hizo ni miongoni mwa taarifa ambazo wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamepatiwa hii leo na Martin Kobler ambaye ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO na mjumbe maalum wa [...]

06/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Migogoro lazima itafutiwe ufumbuzi ukanda wa Sahel: Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa BanKi-moon ambaye yuko ziarani katika ukanda wa Sahel, hii leo amehutubia katika bunge nchini Niger na kulitaka taifa hilo kuungana na nchi nyingine za ukanda huo kutafuta suluhu za migogoro huku akipendekeza kile alichokiita ni muarubaini wa migogoro. Halikadhalika katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameliambia bunge la [...]

06/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Adha za mapigano zaendelea kuwatesa raia Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Wakimbizi CAR

Taarifa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaeleza kutoimarika kwa utulivu nchini humo ambapo hivi karibuni mapigano hayo yaliiubuka tena na kuzua hofu na mtafaruku kwa raia wa nchi hiyo ambao wamejikuta wakipoteza makazi. Ungana na Joseph Msami katika mkala ifuatayo inayoangazia adha wanazokumbana nazo wakimbizi wa ndani nchini humo.

06/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mijeledi na ukatili dhidi ya wanawake ikomeshwe: UM

Kusikiliza / Frances Raday, mtaalamu

Wataalamu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa wametaka kukomeshwa kwa ukatili dhidi ya wanawake hususani ni kuchapwa mijeledi, ikiwamo kwa tuhuma zinazoitwa za kimaadili na kutaka kuheshimwa kwa sheria za kimataifa. Onyo hili linakuja wakati huu ambapo mwanamke Amira Osman Hamed, ambaye ni mwanaharakati wa haki za wanawake na mhandisi amefikishwa mahakani nchini [...]

06/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuwawezesha wanawake kutunza maliasili ni muhimu katika amani endelevu:Ripoti UN

Kusikiliza / Mwanamke

Ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa njia bora ya kuziwezesha nchi zilizokumbwa na mizozo ya kivita kurejea kwenye amani na kusonga mbele kimaendeleo ni kwanza kuwawezesha wanawake kupata fursa ya kumilika rasilimali ikiwemo ardhi, maji,misitu na madini. Ripoti hiyo imebainisha nchi ambazo zimetumbukia kwenye mizozo ya kivita wanawake ndiyo wanaochukua jukumu la [...]

06/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika yatakiwa kuimarisha mifumo ya kuwalinda watoto:UNICEF

Kusikiliza / Watoto, Afrika

Mashirika kumi na tatu yakiwamo ya  Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi barani Afrika yametoa wito kwa serikali barani humo kuimarisha mifumo ya ulinzi kwa watoto ili kuwalinda dhidi ya ukatili, unyanyasaji, kutelekezwa na unyonyaji katika mazingira ya dharura na yasiyo ya dharura.  (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Taarifa ya mashirika hayo ikiwamo lile la kuhudumia watoto [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchina yachangia dola milioni 2 kufadhili huduma za WFP Syria

Kusikiliza / Mfanyakazi wa WFP, Syria

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetoa mchango wa dola milioni mbili kwa ajili ya huduma za dharura za Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, ambalo sasa linawasaidia watu wapatao milioni nne ndani ya Syria waloathiriwa na mzozo. Mchango huo utaisaidia WFP kununua tani 2,000 za ngano, mafuta ya kupikia, na mchele, ambavyo [...]

06/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viwango vya gesi chavuzi angani vyavunja rekodi: WMO

Kusikiliza / Gesi chafuzi

Viwango vya gesi zinazochafua mazingira angani vilifikia rekodi mpya mwaka 2012 huku vikizidi kupanda hali ambayo imesababisha kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya hali ya hewa na kuibadilisha sayari ya dunia kwa maelfu ya miaka inayokuja. Alice Kariuki anaripoti. (Taarifa ya Alice) Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kupitia kwa makala yake ya [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Niger patieni kipaumbele maslahi ya wanawake na watoto wa kike: Ban

Kusikiliza / Wanawake, Nigeria

Ujumbe wa ngazi ya juu unaoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon huko Sahel umekuwepo Niger ambapo pamoja na mambo mengine umeangazia suala la kuwawezesha wanawake huku Benki ya dunia ikiongeza dau la usaidizi. Taarifa kamili na Joshua Mmali. (Ripoti ya Joshua) Siku ya tatu ziarani huko Ukanda wa Sahel, Bwana Ban [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhalifu wa kimazingira unaathiri usalama na maendeleo:UNEP/INTERPOL

Kusikiliza / Uwindaji haramu wa wanyama pori

Uhalifu dhidi ya mazingira unaoanzia biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori na mbao , biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la ozoni na uvuvi ulio haramu ni changamoto la kimataifa ambalo athari zake ni kubwa. Haya yote yamejadiliwa  kwenye mkutano uliondaliwa mjini Nairobi Kenya kati ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na [...]

06/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Virusi vingine vipya vya AH7N9 vyazuka Uchina:WHO

Kusikiliza / Vipimo vya H7N9

Kamishna ya afya ya uzazi wa mpango nchini China imeliarifu shirika la afya ulimwenguni WHO juu ya kubainika kwa watu wawili wapya ambao wamegundulika kukumbwa na virusi vya AH7N9 kufuatia uchunguzi wa kimaabara uliofanywa dhidi yao. George Njogopa na taarifa kamili  (TAARIFA YA GEOERGE NJOGOPA) Mgonjwa wa kwanza kugundulika kukumbwa na virusi hivyo ni mtoto [...]

06/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tuimarishe usimamizi wa maliasili kwenye maeneo ya mizozo: Ban

Kusikiliza / Mizozo Sierra Leone imeathiri maliasili,UNEP

Ulimwenguni kwa kiasi kikubwa kumesheheni taarifa juu ya umuhimu wa mazingira kwa maendeleo endelevu lakini wakati huo huo kiwango cha utumiaji hovyo wa maliasili kama vile misitu, wanyamapori, vyanzo vya maji na hata ardhi ya kilimo kinazidi kuongezeka. Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwenye salamu zake maalum kwa siku [...]

06/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mratibu Maalum wa UM-OPCW atoa taarifa kwa Baraza la Usalama

Kusikiliza / Sigrid Kaag

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepata taarifa ya Katibu Mkuu kuhusu Syria ambapo pamoja na mambo mengine inaelezea kazi ya uteketezaji wa mpango wa silaha za kemikali nchini Syria, kazi inayofanywa kwa pamoja na umoja huo na shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya silaha hizo, OPCW. Mara baada ya kupokea taarifa hiyo [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati za kuleta maridhiano Juba, Kusini mwa Somalia zaendelea

Kusikiliza / Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon akihutubia kwenye mkutano huo

Kundi la ngoma za kitamaduni likitumbuiza kwenye kusanyiko la viongozi wa serikali kuu, serikali ya mkoa na viongozi wa kidini na kikabila, mjini Mogadishu, Somalia, kubwa hapa ni mkutano wa maridhiano wa Juba, lengo ni kuongeza wigo wa uongozi wa serikali kuu kwenye eneo hilo na kudhibiti migongano baina ya koo.  Wajumbe wako makini kwenye [...]

05/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Møller wa Denmark mkuu wa ofisi ya UM Geneva

Kusikiliza / Michael Møller

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemteua Michael Møller wa Denmark kuwa kaimu mkuu wa ofisi ya umoja huo mjini Geneva Uswizi. Bwana Møller anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kassym-Jomart Tokayev ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa mchango wake katika kuongoza kazi za Umoja wa Mataifa mjini humo. Mteule huyo Bwana Møller ana [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tumeshindwa kupanga tarehe ya mkutano wa pili wa Geneva: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Matarajio ya kufanyika karibuni kwa mkutano wa pili wa Geneva kuhusu Syria hayakuweza kutimia hata baada ya msururu wa mikutano ya leo, amesema mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi mjini Geneva hii leo alipozungumza na waandishi wa habari. Bwana Brahimi katika mazungumzo ya pande tatu yakihusisha [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yawakwamua watoto waliosafirishwa Uganda

Kusikiliza / watoto

Shirika la Kimataifa la uhamiaji nchini Uganda IOM, limefanikiwa kuwarejesha katika sehemu zao za asili watoto 21 ambao walikumbwa na biashara haramu  ya usafirishaji wa binadamu. Kwa mujibu wa IOM zoezihiloambalo linaendeshwa kwa ushirikiano na serikali yaUgandahususani vyombo vya dola pia linahusisha mafunzo maalum kwa watoto hao kabla ya kuwarejesha nyumbani. Katika mahojiano na Joseoh [...]

05/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

IOM Uganda yafanikiwa kuwarejesha kwenye maeneo ya asili watoto waliorubuniwa

Kusikiliza / Jumbe Omari Jume

  Shirika la Kimataifa la uhamiaji nchini Uganda IOM, likishirikiana na serikali ya Uganda, limefanikiwa kuwarejesha katika sehemu zao za asili watoto 21 ambao walikumbwa na biashara ya usafirishaji watu. Idadi kubwa ya watoto hao wamekuwa wakisafirishwa kutoka eneo la Karamoja lililoko kaskazini mashariki mwa Uganda hadi mji mkuu wa Kampala na kutumikishwa kwenye shughuli [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wa kimataifa muhimu kukabili changamoto za Sahel: Ban

Kusikiliza / Mzozo wa Mali ulisababisha wengi kuhamia ukimbizini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wanaoambatana naye kwenye ziara huko ukanda wa Sahel akiwemo Rais wa Benki ya dunia, kamishina wa muungano wa afrika, kamishina wa maendeleo wa Muungano wa Ulaya na mwakilishi wa Katibu Mkuu kwa ushirikiano wa jumuiya ya nchi za Kiarabu [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wanaohitaji misaada nchini Syria yapanda hadi milioni 9.3: OCHA

Kusikiliza / Syria displaced

Idadi ya watu wanaohitaji misaada nchini Syria imeripotiwa kupanda hadi kufikia milioni 9.3 . Kulingana na takwimu mpya kati yao hao watu milioni 6.5 wamekosa makazi lakini bado wako nchini humo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Kiwango hicho ni tofauti na makadirio yaliyowekwa mwezi wa Juni, ambayo yalionyesha kuwa kingekuwa watu [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali inazidi kuwa mbaya Syria kila uchao: Mkuu wa OCHA

Kusikiliza / Raia wa Syria wakiandaa mlo ukimbizini

Naona hali inazidi kuwa mbaya kwa wananchi wa Syria iwapo suluhu la kisiasa halitapatikana, ni kauli ya Valerie Amos Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu aliyotoa wakati wa kikao kati yake na watendaji wa ofisi hiyo kutoka sehemu mbali mbali duniani. Kikao hicho kilifanyika New York na kuunganishwa na ofisi [...]

05/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baada ya boti kuzama huko Myanmar, makumi ya watu hawajulikani waliko: UNHCR

Kusikiliza / Kituo hiki cha Sittwe kinakisiwa kua ni maboti haramu yana ng'oa nanga

Huko Pwani ya Myanmar, majanga ya vifo vitokanavyo na safari za mashua yameendelea kuchukua kasi ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linataja Jumapili kuwa ni siku mbaya zaidi kwani makumi ya watu wakiwemo watoto na wanawake wanahofiwa kufariki dunia  baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kusaka maisha bora kuzama. Msemaji wa UNHCR [...]

05/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahofia hatma ya mkimbizi wa Rwanda Joel Mutabazi

Kusikiliza / Nembo ya UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR latiwa wasiwasi na hali ya Joel Mutabazi, mkimbizi wa Rwanda aliyekamatwa na kukabidhiwa kwa serikali ya nchi yake na polisi wa Uganda bila ridhaa yake mnamo Jumamosi ya oktoba 26 mwaka huu. Waziri wa Uganda anayehusika na masuala ya wakimbizi amethibitishwa kukamatwa na kukabidhiwa kwa mkimbizi huyo [...]

05/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tunalaani vikali shambulizi kwa msafara wa harusi Nigeria: UN OHCHR

Kusikiliza / Cécile Pouilly,msemaji wa OHCHR

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali shambulizi  dhidi ya msafara wa harusi lilitokea kwenye jimbo la Borno nchini Nigeria mwishoni mwa wiki. Mnamo tarehe 2 mwezi huu watu 30 waliokuwa wakihudhuria harusi walitekwa na kuawa kwenye barabara ya Bama-Mubi-Banki  jimbo la Borno. Barabara hiyo iko karibu na mapaka na Cameroon [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malefu ya raia wa DRC waingia Uganda wakikimbia oparesheni dhidi ya kundi la M23

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka DRC waendelea kumiminika Uganda

Zaidi  ya watu 10,000 wamekimbia maeneo yaliyo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DCR kwenda nchini Uganda kufuatia mapigano  kati ya wanajeshi wa serikali na wanachama wa kundi la M23 kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.  (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Wanaohama makwao wanaingia [...]

05/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yahaidi kuwapiga jeki wakulima waliokumbwa na mafuriko Benin

Kusikiliza / José Graziano da Silva

Shirika la chakula na kilimo FAO limewapiga jeki wakulima waliopoteza mazao yao kaskazini mwa Benin wakati mto kingo cha mto Niger zilipopasuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa mashamba na mifugo. Hali hiyo iliyojitokeza mwezi Agust mwaka huu ilikuwa kama vile kutonesha kidonda kwa wakulima hao ambao walikuwa wakianza kupata afuheni kutokana na mafuriko yaliyowakumba msimu [...]

05/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa umejizatiti kusaidia Mali: Ban

Kusikiliza / Watoto wa Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wanaoambatana naye kwenye ziara huko ukanda wa Sahel wamekuwa na mazungumzo na Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali mjini Bamako kando ya mwa mkutano wa kikanda wa mawaziri unaofanyika mjini humo. Katika mazungumzo yao Bwana Ban amerejelea mshikamano wake [...]

05/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Elimu kwa mtoto wa kike Afghanistan bado inakumbwa na changamoto

Kusikiliza / Wanafunzi wakike Afghanistan

Elimu imekuwa changamoto kubwa kwa watoto wa kike nchini Afghanistan ambapo utamaduni wa kutosomesha watoto wa kike na  uwepo wa utawala wa Taliban ni kikwazo kikubwa katika kufanikisha hilo. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo inafafanua kwa kina juu ya changamoto hiyo.

04/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Taarifa za kusitisha uhasama DR Congo zatia matumaini: Wajumbe

Kusikiliza / Martin Kobler na mlinda amani wa MONUSCO

Kundi la wajumbe maalum wakiongozwa na Umoja wa Mataifa Jumatatu wamesema wanazingatia taarifa za kusitisha uhasama kati ya waasi wa M23 na serikali ya DR Congo na kutaka waasi hao kuachana na uasi kama ilivyokubali awali. Taarifa ya pamoja wajumbe hao wakiongozwa na yule wa Maziwa Makuu Mary Robinson wamesema wana hofu juu ya kuibuka [...]

04/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wataka Sheria imara za kudhibiti makampuni binafsi ya ulinzi

Kusikiliza / Nembo ya Umoja wa Mataifa

Serikali kote duniani zimetakiwa kutambua umuhimu wa mkataba wa kisheria wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya makundi binafsi ya majeshi na makampuni ya ulinzi (PMSCs) katika kusaidia mfumo wa sheria wa sasa, amesema mtaalamu huru Anton Katz ambaye anaongoza mkutano wa kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa la wanachama wa kudumu. Bwana Katz [...]

04/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuongeza juhudi kukabili mzozo wa Syria:UNDP

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria kambini

Wakurugenzi na wawakilishi wa mashirika 22 ya Umoja wa mataifa wameafikiana kuzindua mpango wa pamoja wa maendeleo kwa ajili ya kukabili mzozo wa Syria  kwenda sambamba na juhudi za kibinadamu zinazoendelea za kutoa misaada ya kuokoa maisha kwa wakimbizi wa ndani ya Syria na katika nchi jirani. Muafaka huo umepatikana katika mwisho wa mkutano wa [...]

04/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uharamia pembe ya Afrika wakusanya karibu dola Milioni 400: Ripoti

Kusikiliza / Pembe ya Afrika

Utafiti mpya kuhusiana na mwenendo wa vitendo vya uharamia umebaini kuwa takriban dola Milioni 400 zilikusanywa kutokana na vitendo hivyo katika kipindi cha kati ya Aprili 2005 na Disemba 2012. Pia utafiti huo umebainisha kuwa kiasi cha meli 179 zilitekwa katika Pwani ya Somalia na eneo la Pembe ya Afrika katika kipindi hicho hicho. George [...]

04/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awasili Mali katika mwanzo wa ziara yake Sahel

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Bank ya dunia Jim Yong Kim wamewasili Bamako Mali katika mwanzo wa ziara ya pamoja huko Sahel. Grace Kaneiya na maelezo zaidi (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Katika ziara hiyo ya pamoja viongozi hao watazuru pamoja na Mali, Niger, Burkina Faso na Chad. Walipowasili Bamako [...]

04/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yajiandaa kuwarejesha raia 40, 000 wa Sudan Kusini Nyumbani

Kusikiliza / IOM yawarejesha waSudan Kusini nyumbani (picha ya faili)

  Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesema linajitahidi kuweza kuwarejesha nyumbani takriban raia wa Sudan Kusini 40, 000, ambao sasa wamekwama katika kambi za muda mjini Khartoum, Sudan. Taarifa kamili na Alice Kariuki. (Taarifa ya Alice) IOM imesema itahitaji karibu dola milioni 20 ili kuweza kuwasafirisha kwa ndege nusu ya watu hao hadi Sudan [...]

04/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunzeni mazingira ili tuvutie watalii: Rais Museveni

Kusikiliza / Mazingira

Suala la utunzaji wa mazingira likiwa miongoni mwa malengo manane ya mendeleo ya milenia. Raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amekemea unchafuzi wake akisema, kinaathiri sana sekta ya utalii. Hi hapa ni ripoti yake John Kibego wa redio washirika ya Spice FM Uganda. (Tarifa ya John Kibego) Akihutubia umati wa waliokusanyika wilayani Nebi kutazama tukio [...]

04/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabilioni ya dola yaahidiwa kwa ajili ya ukanda wa Sahel

Kusikiliza / Wakaazi wa eneo la Sahel

Benki ya dunia imeahidi dola Bilioni 1.5 ilhali Umoja wa Ulaya umeahidi dola bilioni 6.75 kwa ajili ya kusaidia maendeleo kwenye nchi Sita zilizo Ukanda wa Sahel barani Afrika kwa kipindi cha miaka Saba. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (TAARIFA YA JASON) Tangazo hilo linajiri wakati kunapofanyika ziara ya kihistoria kwenda eneo la Sahel ziara [...]

04/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani mauaji ya waandishi wa habari nchini Mali

Kusikiliza / Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali utekaji nyara na mauaji ya waandishi habari wawili Wafaransa katika eneo la Kidal nchini Mali, mnamo Novemba 2, 2013. Wanachama hao wa Baraza la Usalama wametuma risala za rambi rambi kwa familia za wahanga, pamoja na serikali ya Ufaransa. Wamesema, kwa mujibu wa sheria [...]

03/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Faraja yatanda DRC kufuatia kujisalimisha kwa M23

Kusikiliza / Martin Kobler akiwa DRC

Taarifa kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC zinasema vikosi vya waasi wa M23 wanaripotiwa kujisalimisha kwa jeshi la serkali linaloendesha mapambano kwa kushirikiana na kikosi cha kuweka utulivu cha Umoja wa Mataifa MONUSCO. Hatua hii imekuwa faraja kubwa kwa wanachi wa eneo hili kama anavyosimulia Joseph Msami katika makala ifuatayo.

01/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Hali Mashariki mwa DRC imedhibitiwa lakini bado kuna makundi ya waasi: MONUSCO

Kusikiliza / Walinda amani wa MONUSCO wapiga doria,DRC

Hali katika Kivu ya Kaskazini imedhibitiwa sasa, ingawa kundi la waasi wa M23 bado lina himaya katika miji miwili midogo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Hayo yamesemwa na Jenerali Santos Cruz, kamanda wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuweka utulivu katika DRC, MONUSCO. Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa, Jenerali [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kujiamini na kuchukua hatua stahili mapema siri ya mafanikio: Samson Gachia

Kusikiliza / expo

Hatimaye maonyesho ya wiki moja ya miradi bunifu isiyo na madhara kwa mazingifa yamefikia ukingoni  hukoNairobiKenyaambapo imeelezwa kuwa miradi yenye thamani ya dola Miliono 450 za kimarekani imewekewa ahadi kati ya wawekezaji na serikali, vikundi mbali mbali, miradi ambayo ikitekelezwa italeta fursa ya ajira, itainua uchumi huku ikijali mazingira. Maonyesho hayo yalishuhudia utoaji tuzo kwa [...]

01/11/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mimba za utotoni zaangaziwa Tanzania

Kusikiliza / Mama na mwanawe (picha ya UNFPA)

Mapema wiki hii shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA lilitoa ripoti yake kuhusu idadi ya watu ikiangazia zaidi mimba za utotoni. La kustaajabisha ni kwamba takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka, watoto milioni 7.3 wa kike chini ya umri wa miaka 18 hupata ujauzito na kwamba Milioni Mbili katiyaowana umri usozidi miaka 14. Nchini Tanzania [...]

01/11/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Maonyesho ya nchi za Kusini yakamilika Nairobi

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu John Ashe na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Achim Steiner, Nairobi Kenya

Maonyesho ya wiki moja ya miradi na mbinu za maendeleo zinazojali mazingira yaliokuwa yakifanyika mjini Nairobi, Kenya yakihusisha nchi zinazoendelea yamefungwa hii leo . Maonyesho hayo yaliandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia ushirikiano wa nchi zinazoendelea, SOUTH-SOUTH. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Maonyesho hayo yaliwaleta pamoja zaidi ya wajumbe 800 [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutumie fursa iliyopo kutatua mzozo huko Sahel: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon akizungumza kwenye mkutano ambao Rais wa Benki ya dunia alihutubia kwa njia ya video

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Rais wa Benki ya dunia, Jim Yong Kim wiki ijayo wataanza ziara kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika ambapo watafanya ziara huko Mali, Niger, Burkina Faso na Chad.  Akitangaza ziara hiyo kwa waandishi wa habari mjiniNew York siku ya Ijumaa, Ban amesema ziara hiyo kwenye eneo [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS yaonya kuhusu mzigo wa HIV uzeeni

Kusikiliza / Dokta Stephen Watiti ambaye ana umri wa miaka 60 amekuwa akiishi na virusi vya HIV kwa miaka 25

Visa vya HIV na UKIMWI miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 50 na zaidi vinazidi kuongezeka kote duniani, kulingana na utafiti mpya ulofanywa na Shirika linalohusika na HIV na UKIMWI katika Umoja wa Mataifa, UNAIDS. Taarifa kamili na Alice Kariuki (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Utafiti huo umebinisha kuwa, watu milioni 3.6 wenye umri zaidi [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshikamano wa kimataifa uwe kitovu cha ajenda ya baada ya 2015: Mtaalamu

Kusikiliza / Virginia Dandan, mtaalamu huru

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na mshikamano wa kimataifa Virginia Dandan, ametaka nchi wanachama wa Umoja huo kuweka mbele mshikamano wa kimataifa kama msingi wa mafanikio ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Katika ripoti yake kwa Baraza la Kuu mjini New York, Dandan amesema kupitia mshikamano wa kimataifa [...]

01/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nuru yaonekana kuelekea mkutano wa pili wa Geneva kuhusu Syria: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Nchini Syria matumaini ya kupatia suluhu ya amani mzozo unaoendelea yanaanza kuonekana kufuatia ziara ya mjumbe wa pamoja wa Umoja wa mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi kwenye ukanda huo. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Ripoti ya Assumpta) Ziara ya Brahimi huko Mashariki ya Kati ilianza mwishoni mwa wiki ambapo nchi alizopita [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali bado ni tete Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Ghasia zaendelea kushuhudiwa CAR (picha ya UNHCR)

Kiasi cha raia milioni 1.1 katika Jamhuri ya Kati ikiwemo asilimia 50 ya raia waliokosa makazi kutokana na machafuko yanayoendelea wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula. Wengi waliokimbia makazi yaowanadaiwa kujificha msituni kwa hofu ya kushambuliwa. Mahitaji ya misaada ya kibinadamu yameongezeka katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni kutokana na kuzuka upya kwa [...]

01/11/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Angola waliokuwa Botswana warejea makwao

Kusikiliza / Wakimbizi wa Angola wakiwasili eneo la Katwitwi Angola kusini kutoka Botswana

Kundi la mwisho la wakimbizi wa Angola nchini Botswana limeondoka jana hii ikiashiria kufungwa rasmi kwa kambi hiyo kongwe barani Afrika.Kundi la wakimbizi hao ambao walikuwa wakiishi katika kambi ya Dukwi waliwasili jana mchana katika eneo la Mashariki mwa Angola wakiwa na mafurushi yao. Taarifa na George Njogopa (Taarifa ya George) Shirika la Umoja wa [...]

01/11/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yaendesha tathimini kuwasaidia wakimbizi wa DRC

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe mseamaji wa IOM

Wakati kukiwa na taarifa ya waasi wa kundi la M23 wanaopambana na jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kwa usaidizi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kuweka utulivu nchini humo MONUSCO kujisalimisha, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linafanya tathimini ya namna ya kuwasaidia wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo [...]

01/11/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msimu wa safari za mashua huko pwani ya Bengali zatia hofu UNHCR

Kusikiliza / Mashua hizi za uvuvi hutumika kwa safari

Katika siku za karibuni shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepokea taarifa za kutia hofu kwamba watu zaidi wanaondoka kwa kusafirishwa katika boti haramu kwenye Pwani ya Bengali, hali ambayo inaashiria kuanza kwa msimu wa kila mwaka wa safari za meli wakati ambao maelfu ya watu kutoka jimbo la Rakhine huko Myanmar wanahatarisha [...]

01/11/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031