Yaya Touré balozi mpya wa UNEP

Kusikiliza /

Yaya Touré

Mchezaji wa kimataifa wa Côte d’Ivoire na klabu ya Manchester City ya Uingereza Yaya Touré ametangazwa rasmi kuwa balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP na kuahidi kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu barani Afrika.

Touré ambaye alilazimika kusafiri hadi Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya kutangazwa kuwa balozi wa UNEP, anaungana na mwanamitindo wa Brazil Gisele Bündchen, mcheza filamu wa Marekani Don Cheadle, muigizaji wa kike kutoka China Li Bingbing, mpiga picha raia wa Ufaransa Yann Arthus Bertrand pamoja na mchumi wa India Pavan Sukhdev katika kutoa elimu kwa uma kuhusu athari za uharibifu wa mazingira.

Akiongea baada ya kutawazwa rasmi Touré amesema anasikitika kwamba timu yake ya taifa inaitwa tembo, lakini wanyama hawa wakubwa na wenye neema wamesalia takribani 800 pekee nchini mwake na kuongeza kuwa ujangili ni tishio kubwa kwa Afrika na lazima kuchukua hatua sasa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031