WHO yazindua kampeni ya kutokomeza matumizi ya zebaki kwenye vifaa vya utabibu

Kusikiliza /

Kifaa cha kupima joto kilicho na zebaki

Shirika la afya duniani, WHO limezindua kampeni ya kutokomeza matumizi ya zebaki katika vifaa vya utabibu. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

(Ripoti ya Alice)

Kampeni hiyo iitwayo Sekta ya afya bila zebaki ifikapo mwaka 2020 inalenga kuondosha matumizi ya vipimajoto na vipima shinikizo la damu vyenye madini hayo hatarishi. WHO inasema kampeni hiyo itatokomeza utengenezaji, uagizaji au uuzaje nje ya nchi ya vifaa hivyo huku ikisaidia usambazaji wa vifaa mbadala na vya bei nafuu ya kupima joto na shinikizo la damu visivyotumia zebaki. 

Kampeni imezinduliwa kufuatia kutiwa saini wiki hii kwa mkataba wa kimataifa wa MINAMATA ambao unataka kila nchi kutokomeza matumizi ya aina yoyote ile ya madini ya zebaki kutokana na madhara yake kiafya na kimazingira. WHO na wadau wake wanalenga pia kufanya kampeni ya kutokomeza matumizi ya zebaki kwenye bidhaa za urembo na sekta ya wachimbaji wadogo wa madini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31