Watoto 7 kati ya 10 CAR hawajarejea shuleni:UNICEF

Kusikiliza /

Watoto nchini CAR

Watoto saba kati ya watoto 10 walio na umri  wa kwenda shuleni kwenye Jamhuri yaAfricaya kati hawajarejea shuleni tangu kuanza kwa mzozo mwezi Disemba mwaka 2012. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

 (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 Karibu asilimia 65 ya shule zilizokaguliwa zimeporwa au zimeharibiwa na risasi au mabomu. Wanne kati ya watu watano wanasema kuwa hofu ya kutokea ghasia ndiyo sababu ya wanafunzi kukosa kurudi shuleni. Karibu nusu ya shule zimesalia kufungwa huku watoto wakiwa wamepoteza takriban miezi sita ya masomo. Wakati huohuo wakurugenzi wa  masuala ya dharura ya Umoja wa Mataifa yakiwemo OCHA, UNICEF , WFP , IOM , UNHCR, WHO, IMC , Mercy Corps na waakilishi wa FAO wanatarajiwa kutembelea Jamhuri ya Afrika ya kati kuanzia tarehe 17 hadi 19 mwezi huu. Jens Laerke ni mseaji wa OCHA.

 (SAUTI YA YENS LAERKE)

Ujumbe huo unatarajiwa kujadili masuala kuhusu njia za kuimarisha misaada ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati na jinsi ya kuusaidia utawala wa nchi hiyo na washirika wengine katika masuala ya kibinadamu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930