Wataalamu wapendekeza kupigwa marufuku kwa aina mbili za kemikali zitumikazo kuhifadhi mbao na kuua wadudu

Kusikiliza /

Unyunyuziaji wa dawa shamabani

Kamati ya mkataba wa kimataifa wa Stockholm unaofuatilia kemikali chafuzi imependekeza kupigwa marufuku kwa matengenezo, matumizi na usambazaji wa aina mbili za kemikali zitumikazo katika kuhifadhi mbao, kwenye rangi na kuua wadudu.

Taarifa iliyotolewa leo imetaja kemikali hizo aina ya PCN na HCBD kuwa zimekuwa zikitumika viwandani kwa miaka kadhaa sasa lakini zimeripotiwa kuwa na madhara kwa afya ya binadamu.

Kemikali chafuzi hubakia muda mrefu kwenye mazingira baada ya kutumiwa na huweza kuleta madhara makubwa ya kiafya kwa binadamu na pia huharibu mazingira.

DDT ni miongoni mwa mifano ya kemikali chafuzi kwa mazingira na afya ya binadamu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930