Wataalamu wa kimataifa kuzuru maeneo yaliyoathiriwa na ajali ya kinu cha nuklia nchini Japan

Kusikiliza /

Nembo ya IAEA

Shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia duniani IAEA litatuma ujumbe wa wataalamu wa kimataifa kwenda nchini Japan baadaye mwezi huu kukadiria shughuli kwenye maeneo yaliyoathiriwa na ajali ya kinu cha nuklia cha Fukushima Daichi na kutoa habari kuhusu changamoto zilizopo. Kupitia kwa mwaliko wa serikali ya Japan shughuli hiyo itafanyika kati ya tarehe 14 hadi 21 mwezi huu ambapo kundi la watalaamu 16 litajumuisha watalaamu wa kimataifa na wafanyikazi wa IAEA.

Wakiwa kwenye shughuli hiyo wataalamu hao watashirikiana na utawala wa Japan ikiwemo wizara ya mazingira. Siku  ya mwisho ya shughuli hiyo matokeo kutoka kwa wataalamu hao yatawasilishwa kwa serikali ya Japan ambayo itatayatangaza kwa umma.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031