Wanawake wanajukumu kubwa kwa usalama wa chakula:Cousin

Kusikiliza /

Wanawake wa dunia

Kuwawezesha wanawake ni suala muhimusanakatika kukabiliana na njaa na utapia mlo amesema Ertharin Cousin, mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Bi Cousin ameyasema hayo mjini Roma wakati wa hafla ya siku ya chakula duniani inayoadhimishwa kila mwaka Oktoba 16, na mwaka huu kauli mbiu ni "mifumo endelevu ya chakula kwa ajili ua usalama wa chakula na lishe."

Ameongeza kuwa hatua yoyote ya kuimarisha na kufanyia mabadiliko mifumo lazima zitambue pia jukumu kubwa na muhimu linalobebwa na wanawake kwani wanajukumu kubwa saana katika mifumo ya chakula.

Bi Cousin amesema mwaka jana WFP imewasaidia watu karibu milioni 100 walioathirika na migogoro,majanga na kushindwa kwa mifumo ya chakula katika mataifa na nchi zaidi ya 80.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031