Wakati umefika kuwa na bunge la dunia: Mtaalamu

Kusikiliza /

Alfred de Zayas

Mtalaamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu uendelezaji wa demokrasia na usawa duniani Alfred de Zayas ameunga mkono wito unaotolewa wa kuwa na bunge la dunia, chombo ambacho amesema kitakuwa ni jibu la pengo la kidemokrasia linalojitokeza.

Akizungumza mjini Geneva, Uswisi De Zayas amesema chombo hicho kitatoa fursa ya sauti ya umma kusikika kupitia wawakilishi watakaowachagua.

De Zayas amerejelea ripoti yake kwa Baraza Kuu inayosema kuwa bunge la dunia linaweza kuundwa kwa kuzingatia ibara ya 22 ya katiba ya Umoja wa Mataifa au kwa misingi ya mkataba mpya baina ya serikali ikifuatiwa na makubaliano ya kujumuisha makubaliano hayo ndani ya Umoja wa Mataifa.

Mtaalamu huyo amesema bunge la dunia lenye mamlaka kusongesha ajenda ya kidemokrasia awali linaweza kuwa na wabunge kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na nchi alikwa na hatimaye kuwa na wa bunge wa kuchaguliwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031