Wahamiaji hawapatiwi stahili yao, usalama wao mashakani: Rais Baraza Kuu

Kusikiliza /

Kikao cha Baraza Kuu kuhusu uhamiaji na maendeleo

Wakati likiripotiwa janga hilo la boti, mjadala mkuu kuhusu uhamiaji wa kimtaifa na maendeleo umeanza leo mjiniNew York. Assumpta Massoi ana taarifa kuuhusu.

 TAARIFA YA ASSUMPTA

 Mjadala huo unajikita katika kutafuta njia mwafaka za kuimarisha utaratibu na ushirikiano kwenye ngazi zote kwa ajili ya kuendeleza faida za uhamiaji wa kimataifa kwa wahamiaji na nchi husika, pamoja na mchango wake kwa maendeleo, huku yakipunguzwa madhara yatokanayo na uhamiaji.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, rais wa Baraza Kuu, John William Ashe, amesema suala la uhamiaji linaigusa kila nchi na watu binafsi

"Mkasa wa hivi majuzi kwenye pwani ya Sicily ni baa linalotukumbusha kwa nini mazungumzo yetu kuhusu uhamiaji, hususan kuhusu usalama na maslahi ya wahamiaji, ni muhimu na ya dharura. Uhamiaji unafaa na unahitaji kuzingatiwa nasi sote, na juhudi za pamoja. Kila mmoja anaweza kunufaika, ikiwa uhamiaji utadhibitiwa vyema."

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, Laura Thompson amezungumzia umuhimu wa ulinzi wa haki za binadamu kwa kundihiloambalo amesema mchango wake wa maendeleo kwa nchi wanazohamia hauthaminiki.

"Ni muhuimu, huwezi kuzungumzia athari chanya za uhamiaji katika maendeleo kama huna mfumo unaolinda haki za wahamiaji. Wahamiaji wanachangamana na jamii katika mazingira wanaoishi na kule wanakotoka. Wahamiaji wenye afya nzuri, haki zao zinagheshimiwa, wanapata malipo stahiki na kazi yenye hadhi mchango wao ni rahisi na mkubwa zaidi."

Mkutano huo wa siku mbili utahusisha pia mashirika mbalimbali ya UM yanayojihusisha na wahamiji pamoja na mashirika mengine ambapo mjadala utagusia pia kuwekwakamaaagenda aya nmaendeleoa baada katika mkakati wa maendeelo wa Umoja wa Mataifa baada 2015.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930