Uteketezaji wa silaha za kemikali waanza Syria

Kusikiliza /

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Kupinga Silaha za Kemikali, OPCW, tayari umeanza kuteketeza vifaa na silaha za kemikali nchini Syria baada ya kufanya ukaguzi wa awali mnamo Jumapili na Jumatatu wiki hii, amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la OPCW, Ahmet Üzümcü

Bwana Üzümcü amesema kazi ya ukaguzi inaendelea, na timu ya wataalam wengine kumi na wawili inapelekwa nchini Syria kujiunga na wale walioko huko tayari. Ameongeza kuwa ujumbe huo una muda mfupi wa kutekeleza majukumu yake, kama ilivyoidhinishwa na Baraza la Usimamizi la OPCW.

"Hii ni hali ya kipekee kwa OPCW. Haijawahi kutokea, na tupo mwanzoni mwa harakati ngumu, kwani kuna changamoto kubwa. Hata hivyo, shirika letu lina uwezo wa kutosha, kimaarifa, kitaaluma na uzoefu wa kutekeleza jukumu hili. Wakati Syria ikikaribia kuwa nchi mwanachama nambari 119 wa shirika letu mnamo Oktoba 14 wiki ijayo, tutakaribia hata zaidi kukamilisha umbo la kimataifa la mkataba wetu."

Syria inatakiwa kuwasilisha mpango wa utaratibu wa kuteketeza silaha za kemikali kwa Baraza la Usimamizi la OPCW ifikapo tarehe 27 Oktoba. Viwanda vya kutengeneza silaha za kemikali vinatakiwa vikome kuwa na uwezo wa kutumiwa wakati huo pia. Mpango wa kuteketeza uwezo wote wa silaha za kemikali ifikapo kati ya mwaka ujao, unatakiwa kuridhiwa na Baraza hilo ifikapo tarehe 15 Novemba.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930