USAID yatoa msaada wa chakula Zimbabwe

Kusikiliza /

Mama amebeba chakula

Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani USAID limechangia dola milioni 25 kusaidia familia zinazoteseka kufuatia ukame na mavuno hafifu nchini Zimbabwe.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limepanga kutumia msaada huo pamoja na ile mingine iliyotolewa kuwasambazia watu milioni 1.8 walioko kwenye maeneo ambayo yako hatarini kukosa chakula cha kutosha.

Operesheni ya usambazaji wa misaada hiyo imepangwa kufanyika katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi March mwakani, ikiwa ni hatua ya kwanza iliyopewa jina la " hatua ya kujifunza"

Kwa kawaida msimu wa mavuno nchiniZimbabweunaanza kuanzia mwezi March hivyo kufanyika kwa mpango huo unalenga kukabiliana na kitisho chochote cha ukosefu wa chakula kinachoweza kujitokeza.

Kiwango cha ukosefu wa chakula nchiniZimbabwekinatajwa kuwa cha hali ya juu huku kukielezwa kwamba hali hiyo imesababishwa na mambo mengi ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, ongezeko la gharama kwa pembe jeo .

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2017
T N T K J M P
« mei    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930