UNMISS imelaani vikali mashambulizi jimboni Jonglei

Kusikiliza /

UNMISS

Mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini (UNMISS) umelaani vikali mashambulio dhidi ya raia siku ya Jumapili kwenye eneo la Twic Mashariki jimboni Jonglei. Mashambulio hayo yamesababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi.

Moja ya mashambulio hayo yamefanyika katika kambi za ng'ombe moja Paliau , huko Ajong Payam na lingine Maar huko Pakeer Payam, na mashambulio kadhaa katika maeneo mbalimbali. Baada ya mapigano kusita Jumapili humama za usafiri wa anga za Umoja wa Mataifa UNHAS iliwasafirisha wahudumu wa afya kwenye maeneo ya mashambulizi ili kuwaokoa manusura.

Hadi mwisho wa siku UNHAS imesafirisha watu 31 waliojeruhiwa vibaya sana kuwapeleka Bor na Juba na kuarifu kwamba majeruhi wengine zaidi ambao ni raia bado wapo kwenye eneo hilo na UNHAS imetuma helkopta kuendelea kuwahamisha.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930