UNHCR yajikita kurejesha vitambulisho kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza /

Mfanyakazi wa UNHCR akichambua vitambulisho kwenye kituo Raba’a al-Sarhan

Nchini Jordan, wafanyakazi wapatao 50 wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR wanafanya kazi kutwa kucha ili kukamilisha kazi ya kurejesha vitambulisho kwa wakimbizi wa Syria ambao walivisalimisha wakati kabla ya kuingia kambi ya Za'atari nchini Jordan. Kazi hiyo inayofanyika kituo cha Raba’a al-Sarhan kilicho mpakani mwa nchi mbili hizo, inafuatia makubaliano ya mwezi Julai mwaka huu kati ya serikali yaJordanna UNHCR ya kutaka vitambulisho hivyo virejeshwe kwa wahusika kwa kuwa wanavitaka kwa sababu moja hadi nyingine. Hata hivyo kazi hiyo imekuwa ngumu kutokana na mlundikano wa nyaraka hizo baada ya wakimbizi wengi kukimbia machafuko nchiniSyriana kusababisha mfumo wa kupokea nyaraka na kuhifadhi kuzidiwa uwezo. Mkuu wa operesheni za UNHCR nchini Jordan Andrew Harper amesema pamoja na kwamba kazi hiyo ni ngumu, wanapata faraja na furaha kubwa pindi wanapoweza kuwarejeshea wakimbizi hao nyaraka zao na furaha hujidhihirisha usoni. UNHCR inasema wigo wa urejeshaji utahusisha pia wakimbizi walio kambini na pia ina mpango wa kuanzisha kazi ya kusajili upya wakimbizi ili kupata idadi kamili na hivyo kurahisisha kazi ya utoaji misaada na huduma kwa wakimbizi hao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29