Umoja wa Mataifa wamkumbuka Hayati Mwalimu Nyerere

Kusikiliza /

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo, shughuli maalum inafanyika kumkumbuka Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tukio linaloenda pamoja na uzinduzi wa kitabu kuhusu jabali huyo wa Afrika, Ripoti ya Assumpta Massoi inaeleza zaidi.

(Ripoti ya Assumpta)

Miaka 14 tangu kifo chake Hayati Mwalimu Nyerere bado anakumbukwa kwa mchango wake katika medani za kimataifa na kitaifa na hapa New York, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ataongoza shughuli hiyo iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa. Wawakilishi wa kudumu kutoka Muungano wa Afrika, China, Kenya, Jamaica, India, Fiji na Afrika Kusini watatoa hotuba kuhusu vile walivyomfahamu Mwalimu. Hotuba ya mwisho ya Baba wa Taifa akiwa Rais alitoa shukrani kwa Watanzania….

(Sauti ya Nyerere)

Profesa Ali Mazrui na Profesa Lindah Mhando kwa pamoja wameandika "Julius Nyerere, jabali la Afrika katika medani za kimataifa" kitakachozinduliwa hii leo na hapa Profesa Lindah anasema:

(Sauti ya Profesa Lindah)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031