Ulinzi wa wanawake vitani ni lazima: Dokta Mukwege

Kusikiliza /

Dokta Dennis Mukwege

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake anayejitolea kutibu wanawake waliokumbwa na ubakaji na ukatili wa kingono huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC, Denis Mukwege amesema jumuiya ya kimatifa lazima iheshimu na kutoa ulinzi kwa wanawake katika migogoro kwani hudhalilishwa kinyume na hadhi yao katik jamii.

Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa hii Dokta Mukwege raia wa DRC ambaye alinusirika kifo mwaka mmoja uliopita kufuatia watu wasiojulikana kuivamia familia yake kwa kuchukizwa na harakati zake za kutetea wanawake amesema azimio la baraza la usalama la kulinda wanawake katika migogoro linazidi kukiukwa.

(Sauti Mukwege)

Kwa undani wa simulizi ya kusisimua juu mwanaharakati huyo usikose kusikiliza kutembelea ukurasa wetu na kusikiliza makala yetu ya wiki.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930