Tuwekeze kwa elimu ya watoto wa kike ili waendelee na kutusaidia: Ban

Kusikiliza /

Elimu kwwa mtoto wa kike

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amesema kuwapa watoto wa kike uwezo, kuhakikisha haki zao za binadamu na kukabiliana na ubaguzi na ukatili wanaokumbana nao ni muhimu kwa maendeleo ya familia ya ubinadamu. Grace Kaneiya na taarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Katika taarifa yake ya kuadhimisha siku ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema kuwapa watoto wa kike elimu inayowafaa ndiyo njia bora ya kufikia malengo ya kulinda haki zao, na kuwalinda kutokana na ubaguzi na ukatili.

Bwana Ban amesema watoto wengi wa kike katika nchi nyingi huzuiwa kwa ajili ya jinsia yao tu, na wengi wao wametoka familia ambazo mama zao pia walinyimwa nafasi ya kwenda shule, huku wale wanaopata fursa hiyo wakikumbana na ubaguzi na ukatili.

Angel Benedict ni mkurugenzi wa taasisi iitwayo Haki sawa nchini Tanzania, na anaeleza namna watoto wa kike wanavyokwama kwenda shule na harakati za kuwakwamua

ANGELA

Katibu Mkuu amesema aliuzindua mkakati wa Kimataifa wa Elimu Kwanza ili kuongeza kasi ya kumpeleka kila mtoto shule, hususan watoto wa kike, akiongeza kuwa ili kupata ufanisi, tunahitaji suluhu mpya kwa changamoto zilizopo kwa elimu ya watoto wa kike

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930