Tutafungua ofisi Misri kusaidia mchakato wa katiba: Pillay

Kusikiliza /

Navi Pillay

Umoja wa Mataifa unatarajia kufungua ofisi ya kanda nchini Misri kwa ajili ya kusaidia nchi hiyo katika machakato wa kuandika katiba. Katika mahojiano maalum na Dob Bob wa idhaa ya Kingereza ya radio ya Umoja wa Mataifa mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navy Pillay amesema bado hali ya usalama ni tete nchini Misri na amekuwa akipokea taarifa za vifo na majeruhi na kusisitiza uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini humo utasadia keleta suluhisho kwa nchi hiyo iliyoko Kaskazini mwa Afrika

 Naendelea kupokea ripoti ya vifo na kujeruhiwa kwa waandamanaji  lakini natarajia kupokea kwa ukunjufu mwaliko wa serikali wa kufungua ofisi ya kikanda yenye mamalaka ya kusimamia ili tuweze kuisadia serikali katika mchakato wake wa kuandika katiba. “

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031