Tokomeza ukatili na vurugu dhidi ya watoto: UNICEF

Kusikiliza /

Mtoto huyu alikumbwa na Ukatili

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF katika siku ya kimataifa ya kupinga vurugu na ukatili, limetaka watoto walindwe ili waweze kuishi kwenye mazingira yanayowawezesha kufikia ndoto zao.

Taarifa ya UNICEF imesema duniani kote kutwa kucha mamilioni ya watoto wanakumbwa na ghasia iwe shuleni, nyumbani kwenye jamii na mara nyingi vitendo hivyo vinafanyika kwenye vificho na mara nyingi hufanywa na mtu ambaye mtoto anamfahamu au anamwamini.

Imesema hatimaye afya ya mtoto kimwili na kiakili inaathirika na anashindwa kutangamana na jamii na hata kukwamisha mwendelezo wa makuzi yake kufikia utu uzima.

Kwa mantiki hiyo imetaja hatua za kuchukua kulinda watoto kama vile kufahamu aina ya ukatili na vurugu wanazofanyiwa watoto na kutoa ripoti mara moja kwa mamlaka husika ili mtuhumiwa wa vitendo hivyo aweze kuchukuliwa hatua.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29