Rekodi ya haki za binadamu Uchina yamulikwa

Kusikiliza /

Ramana ya Uchina

Uchina imetetea rekodi yake ya haki za binadamu, wakati wa ukaguaji wake wa pili wa kimataifa katika Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi. Ukaguzi wa rekodi za haki za binadamu za nchi wanachama hufanyika mara moja kila katika miaka mine.

Ujumbe wa Uchina wenye watu 43 uliongozwa na Balozi Wu Hailong kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya China, ambaye amesema serikali ya Uchina ina utashi thabiti wa kulinda haki za binadamu na huuzingatia ukaguzi huu wa mara kwa mara na shughuli nyingine za haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa kama ipasavyo.

Amesema mapendekezo yote 42 ambayo Uchina ilikubali wakati wa ukaguzi wa kwanza ama yametekelezwa, au yanapangwa kutekelezwa.

Miongoni mwa hatua katika haki za binadamu ambazo ujumbe wa Uchina umewasilisha kwenye ukaguzi huo ni juhudi za serikali kukabiliana na umaskini vijijini na kuhakikisha haki ya upatikanaji elimu kwa umma, pamoja na kuzindua mfumo wa bima ya afya kote nchini.

Wajumbe kwenye Baraza la Haki za Binadamu wamependekeza mambo kadhaa, yakiwemo kukomesha matumizi ya utesaji, vifungo na kuwakamata watu ovyo, pamoja na kulinda haki za watu wa asili kama vile jamii za wa Tibet, Uyghur na Mongolia, na kuufanyia marekebisho mfumo wa sheria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031