Mkuu wa UNAMID awaenzi walinda amani waliouawa

Kusikiliza /

Mlinda amani

Mwakilishi maalumu wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID  Mohamed Ibn Chambas Jumatatu amezuru makao makuu ya UNAMID El Geneina, Magharibi mwa Darfur, kufuatia mauaji ya walinda amani polisi watatu wa UNAMID kutoka Senegal hapo Oktoba 13.

Bwana Chambas amepongeza ujasiri wa wafanyakazi wa UNAMID ambao walipoteza maisha yao wakijaribu kurejesha amani Darfur. Amewaambia wafanyakazi wa UNAMID kuwa amewapelekea ujumbe maalumu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon na mkuu wa operesheni za Umoja wa mataifa la kulinda amani Hervé Ladsous.

Amesema wote wametuma salamu za pole na kuwatia moyo kuendelea kutimiza wajibu wao ambao ndio uliowapeleka Darfur, wa kuwalinda raia na kuhakikisha amani inarejea katika eneo hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031