Mjumbe wa UM kuhusu haki za wakimbzi wa ndani afanya ziara Serbia na Kosovo

Kusikiliza /

Chaloka Beyani

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani ameishauri serikali ya Serbia na utawala wa Kosovo kufanya mikakati ya kupata suluhu kwa wakimbizi wa ndani nchini Serbia na Kosovo. Akiongea baada ya kukamilisha ziara rasmi nchini humo Beyani amesema kuwa huu ndio wakati mwafaka wa kupata suluhu. Amesema kuwa serikali ya Serbia na utawala wa Kosovo ni lazima wajitahidi kuwatafutia suluhu wakimbizi hao. Kuna karibu wakimbzii wandani 97,000 kutoka Kosovo walio na mahitaji kutokana na makadirio tangu mwaka 2011 yaliyofanywa na Shirika la kuhudumia wakibizi la Umoja wa Mataifa UNHCR . Ziara ya siku nne aliyofanya mjumbe huyo ilimpeleka Belgrade na Pristina ambapo alikutana waakilishi wa serikali , Umoja wa Mataifa na mashirika ya umma.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031