Mamilioni ya watoto kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio nchini Syria

Kusikiliza /

Huku Syria ikisubiri kuthibitishwa kwa kesi za ugonjwa wa polio mashariki mwa nchi shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limejiunga na Shirika la afya duniani WHO na washirika wengine katika kuongoza zoezi kubwa la utoaji wa chanjo kwa lengo la kuwakinga watoto nchini humo na eneo lote dhidi ya ugonjwa wa polio. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

Ndani mwa Syria kampeni inayoongozwa na wizara ya afya ilianza tarehe 24 mwezi Oktoba ikiwalenga watoto milioni 2.4 kwa lengo la kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa polio, surua na mengineyo. Karibu watoto 500,000 nchini Syria hawajapata chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio kwa kipindi cha miezi miwili iliyiopita kutokana na ukosefu wa usalama. Mzozo nchini Syria umesabaisha kuhama kwa watu wengi huku mamilioni ya watoto wakiwa miongoni mwa wale wanaoahama ndani mwa Syria au wakiwa wanavuka mipaka na kuingia mataifa mengine. Kwa sasa UNICEF inapanga oparesheni zake kuhakikisha kuwa chanjo hziko tayari kuweza kuwafikia washirika wao na kutoa hamazisho kuhusu umuhimu wa kuwachanja watoto.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031