Licha ya changamoto tumeimarisha ushirikiano wa kimaendeleo: Afrika

Kusikiliza /

Tete Antonio akihojiwa na Joseph Msami wa Radio ya UM

Mwangalizi wa kudumu wa Ujumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa Tete Antonio amesema wakati maadhimisho ya wiki ya Afrika katika Umoja wa Mataifa  yakianza leo bara hilo linajivunia mabadiliko yanayotokea hususani katika mashirikiano ya kimaendeleo na jumuiya ya kimataifa.

Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahii ya radio ya Umoja wa Mataifa Bwana Antonio amesema licha ya mafanikio hayo ziko  changamoto za usimamizi wa uchumi wa kimataifa

 (Sauti Antonio)

Kuna mabadiliko mengi barani Afrika,ukiangalia katika maeneo yaubora wa  majadiliano na ushirikiano ambao msingi wake ni wa manufaa kwa pande zote, Kuna changamoto kuhusu namna ya kusimamia uchumi wa kimataifa kwani taasisi za kimataifa ziliundwa zamani lakini zipo juhudi za mabadiliko na mabadiliko lazima yaanzie kwetu.”

Maadhimisho ya wiki ya Muungano wa Afika katika Umoja wa Mataifa yanayoangazia  mpango wa Afrika kujitathmini masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanaratibiwa na mpango wa ushirikiano kwa  programu ya ubia mpya kwa ajili ya maendeleo ya Afrika, NEPAD.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031