Kuboreshwa kwa mifumo ya chakula ndilo suluhisho katika kuangamiza njaa: FAO

Kusikiliza /

Leo ni siku ya chakula dunianai

Mifumo bora  ya chakula ndiyo inahitajika ili kuweza kuangamza njaa na utapiamlo kote duniani . Huu ndio ujumbe mkuu wakati wa maadhimisho ya leo ya siku ya chakula duniani kutokana kwa Shirika la kilimo na mazoa la Umoja wa Mataifa FAO. Siku hii huadhimishwa kwenye mataifa 150 na pia ni sherehe ambazo huadhimishwa na FAO tangu Shirikahilolibuniwe mwaka 1945. Jason Nyakundi na taarifa kamli.

 (RIPOTI  YA JASON)

Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni 842 wana utapiamlo.  Kwenye ujumbe uliosomwa na askofu Luigi Travaglino kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba bado kuna njaa duniani.

Papa Francis amesema kuwa kuna haja ya kufanyiwa mabadiliko mifumo ya chakula kamamoja ya njia ya kuonyesha uzalengo kwa wale walio maskini ambapo pia ametaka suala la kutupwa kwa chakula kuzuiwa suala  ambalo amelitaja kuwa chanzo  cha athari za uzalishaji wa chakula duniani.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki amesema kuwa hatakamamifumo ya chakula uzalisha chakula kingi kwa kila mmoja zaidi ya nusu ya watu wote duniani wanatumia chakula kingi zaidi au hawapati chakula cha kuwatosha.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema kuwa lishe haitaboreshwa ikiwa hakuna usalama wa chakula na ikiwa hakuna mifumo ya chakula iliyo bora.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031