Kifo cha mlinda amani kutoka Zambia huko Darfur, Ban atuma rambirambi

Kusikiliza /

Walinda amani wa UNAMID (Picha kutoka maktaba)

Katika jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, shambulio lililofanywa Ijumaa na watu waliojihami na silaha huko El Fasher dhidi ya askari wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa Darfur, UNAMID limesababisha kifo cha mlinda amani kutoka Zambia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza kusikitishwa na kifo hicho na ametuma salamu za rambirambi kwa familia za askari huyo, serikali za Zambia na UNAMID. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Bwana Ban akishutumu shambulio hilo na kusema kuwa ni matarajio yake serikali ya Sudan itachukua hatua za haraka kuwasaka wahusika na kuwafikisha mbele ya sharia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2016
T N T K J M P
« nov    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031