Kazi ya kuharibu silaha za kemikali Syria yaanza

Kusikiliza /

Timu ya OPCW ikiondoka kuelekea Syria/picha ya OPCW

Jopo la wataalamu kutoka shirika la kudhibiti silaha za kemikali, OPCW chini ya usaidizi wa Umoja wa Mataifa limesimamia kazi ya kuharibu silaha za kemikali nchini Syria inayofanywa na watendaji wa nchi hiyo. Taarifa ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Alice)

Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa watendaji hao walitumia vifaa maalumu kuharibu na kuvunja aina mbali mbali za silaha ikiwemo vichwa vya makombora, mabomu ya kurushwa kutoka angani na vifaa vya kuchanganyia silaha hizo za kemikali. Mchakato huo wa kuharibu silaha za kemikali nchini Syria ulioanza Jumapili utaendelea siku zijazo ambapo wataalamu hao wa OPCW chini ya usaidizi wa Umoja wa mataifa wanafuatilia, wanathibitisha na kutoa taarifa juu ya mwelekeo wa Syria wa kukidhi masharti ya kimataifa ya kuharibu silaha zake za nyuklia na maeneo ya kuzitengenezea.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031