Kamishna ya fidia ya UM yakamilisha kulipa dola milioni 1.24 kwa Kuwait

Kusikiliza /

Ramana ya Kuwait

Kamishna ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya utoaji fidia leo imetangaza kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 1.24 kwa serikali ya Kuwait ikiwa na sehemu iliyosalia baada ya kufanyika malipo ya awali katika siku za nyuma.

Kamishna hiyo ya utoaji fidia ilianzishwa mwaka 1991 kwa kufuata azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nambari 687 la mwaka 1991 kwa ajili ya kutathmini na kisha kutoa fidia kwa walalamikaji waliokumbwa na madhira mbalimbali.

Fidia hiyo inaweza kutolewa kwa serikali, mtu binafsi ama taasisi kwa kuzingatia madai ya mlalamikaji.

Kuwait imelipwa fidia hiyo kutokana na uvamizi uliofanywa na Iraq katika kipindi cha August 2 1990 hadi March 2, mwaka 1991 ilipoondolewa kwa nguvu katika ardhi hiyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031