Ivory Coast yajiunga na mkataba wa kutokuwa na utaifa:UNHCR

Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema Ivory Coast imejiunga na mikataba ya kimataifa inayohusu kutokuwa na utaifa. Hii ni moja ya hatua muhimu zinazochukuliwa na serikali hiyo kupunguza idadi ya watu wasio kuwa na utaifa nchini humo.

UNHCR inakadiria kuwa watu 700,000 nchini Ivory Coast kwa sasa hawana utaifa au hawana nyaraka za kuthibitisha utaifa wao na matokeo yake hawawezi kupata huduma muhimu kama elimu na afya. Wengi wa watu hao wasio na utaifa ni watoto ambao vyeti vyao vya kuzaliwa havikusajiliwa na mara nyingi hawawezi kuandikishwa shuleni.

UNHCR imekaribisha hatua ya Ivory Coast ya kujiunga na mikataba ya kutokuwa na utaifa na nia yake ya kulinda haki ya utaifa.Kwa miongo kadhaa uthibitisho wa uraia wa Ivory Coast umekuwa na utata wa kisiasa na kijamii, huku suala la hati za umiliki wa ardhi lilizusha hadi ghasia za kijamii.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930