Irina Bokova ateuliwa tena kuwa Mkurugezni Mkuu wa UNESCO

Kusikiliza /

Irina Bokova

Bi Irina Bokova ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, ameteuliwa tena kuendelea kuushikilia wadhafa huo kwa muhula wa pili, katika kura ya mchujo ilowajumuisha wagombea wengine wawili. Wagombea hao walikuwa na Bwana Rachad Farah kutoka Djibouti na Joseph Maïla kutoka Lebanon.

Uteuzi huo utawasilishwa kwenye mkutano mkuu wa nchi 195 wanachama wa UNESCO, ili ufanyiwe idhinisho.

Irina Bokova ambaye ana umri wa miaka 61, ni raia wa Bulgaria na amekuwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO tangu alipoteuliwa kwanza mnamo Oktoba 2009. Aliwahi kuhudumu kama balozi wa Bulgaria nchini Ufaransa, na kama Mwakilishi wake wa Kudumu kwa UNESCO.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2017
T N T K J M P
« mei    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930