IOM yajadili afya za wasafiri mipakani na nchi za Kusini mwa Afrika

Kusikiliza /

Nchini Tanzania, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM leo limehitimisha mkutano wake wa siku uliowakutanisha wataalamu wa fani mbalimbali kwa ajili ya kujadilia mkakati wa pamoja wa afya kwa wasafiri maeneo ya mipakani pamoja na madereva wa magari makubwa ambao wanakabiliwa na hatari ya kukubwa na magonjwa ya kuambukizwa. Kutoka dsm, George Njogopa na taarifa zaidi.

Mkutano huo ambao umewaleta pamoja wawakilishi kutoa nchi za Burundi, Kenya, Uganda,Zambia, Msumbiji na wenyeji Tanzania unafuatia majadiliano ya pamoja uliofanyika huko Kigali Rwanda, miaka miwili iliyopita.  Wakati akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu Wizarav ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil alisema kuwa, Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi inazopakananazo ili kuhakikusha kwamba sekta ya afya inaimarika. Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa shirika la kimataifa ka uhamiani IOM Damien Thuriax alitaka kuimarishwa kwa ufanisi katika maeneo ya mipakani ili kurahisisha shughuli za usafiri.

" Nangependa kuona kwamba huduma zinaboresha katika maeneo ya mipakani ili watu hawatumia muda mwingi zaidi.”

 Kuhusu maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kwa madereza wanaosafiri mwendo mrefu, Makamu Mwenyekiti wa chama cha madereza nchini Tanzania bwana Mohamed Shariff Abdukadir, alitaja sababu zinazowatumbukiza madereva hao katika janga hilo.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031