ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa Kenya Walter Barasa

Kusikiliza /

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa Kenya, Walter Osapiri Barasa kwa madai kadhaa ikiwemo kuingilia mwenendo kwa kesi zinazowakabili raia waKenyaambazo zinaendelea kwenye mahakama hiyo. Hati hiyo iliyotolewa leo inazingatia maelezo ya msingi yaliyotolewa na upande wa mashtaka ambapo Jaji Cuno Tarfusser amesema yanatosheleza kumkamata mwandishi huyo ili asiendelee kuhatarisha ushahidi au kukwamisha kesi zinazoendelea.

Maelezo ya mwendesha mashtaka ni kwamba Walter anashawishi mashahidi au anajaribu kuwalipa hongo mashahidi ili wajiondoe kwenye kesi hizo na hivyo Jaji Tarfusser ameona ni vyema kumkamata mwandishi huyo na afikishwe mahakamani ili kuhakikisha hakwamishi au ahatarishi uchunguzi au mwenendo wa kesi.

Hii ni kesi ya kwanza ICC ambapo mtuhumiwa anashtakiwa kwa kukwamisha utekelezaji wa haki kwa mujibu wa kifungu namba 70 cha mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama hiyo ya kimataifa ya uhalifu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031