Harakati za kutokomeza umaskini Tanzania zamulikwa

Kusikiliza /

Soko la nguo za mitumba

Wiki hii Mataifa mbali mbali duniani yaliadhimisha siku ya kutokomeza umaskini ambapo ilielezwa kuwa idadi ya watu maskini inapungua lakini bado watu Bilioni Moja nukta mbili ni mafukara. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alieleza bayana kuwa kupungua kwa idadi hiyo kusipofushe watu macho na kuacha harakati za kuweka mazingira sawia kwa kila mtu kuweza kufanya kazi yenye hadhi na kuweza hatimaye kufikai lengo namba moja la milenia la kukomeza umaskini duniani ifikapo mwaka 2015. Nchini Tanzania harakati za kutokomeza umaskini zinaendelea ambapo vijana wake kwa waume wanahaha kila uchao kuhakikisha mkono unakwenda kinywani. Serikali nayo inasonga mbele. Je nini kinafanyika? Mwenzetu George Njogopa kutoka Dar es salaam alivinjari katika baadhi ya maeneo kuweza kufahamu kile kinachofanyika na alianzia maeneo ya mjini..

(MAKALA YA GEORGE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930