Hali nchini Syria na mataifa jirani yatia wasi wasi

Kusikiliza /

 

wakimbizi wa Syria

Shrika la mpango wa chakula duniani WFP limeelezea wasi wasi uliopo kutokana na hali ilivyo nchiniSyriana mataifa jirani kutokana kuongezeka kwa idadi ya watu wanaohama makwao walioathiriwa na kuzorota kwa  uchumi .

Watu waliohama makwao hawana uwezo wa kununua kutokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa. Mavuno duni mwaka huu . Ikiwa inawafikia watu milioni tatu mwezi huu  Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linapanga kuwafikia watu milioni nne. mwezi ujao.

Kuna watu wengi nchiniSyriaambao misaada ya kibinadadamu haijawafikia. Hali inazidi kuwa mbaya kila siku huku suluhu la kisiasa likihitaji kuafikiwa.

WFP inasambaza chakula kilicho tayari kuliwa kwa watu huku ikigawa vocha ambazo zitatumiwa na wakimbizi kununua chakula . Hata hivyo kuna sehemu zingine kwenye maeneo yaHomsambapo WFP haijafika tangu kuanza kwa mzozo .

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2016
T N T K J M P
« ago    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930