GAVI kuwachanja watoto milioni 250 ifikapo kwaka 2015

Kusikiliza /

Ripoti mpya iliyotolewa inaonyeha kuwa ubia wa chanjo duniani GAVI uko kwenye mkondo kuzisaidia nchi zinazoendelea kuwachanja karibu watoto milioni 250 ifikapo mwaka 2015 ambapo vifo milioni moja vitazuiwa kwenye mpango huo. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Jason)

Kwenye ripoti ya GAVI iliyochapishwa hii leo inasema kuwa watoto wengi zaidi wanafikiwa na chanjo ya kuokoa maisha ikiwa ni miaka miwili tangu kutolewa kwa ahadi ya kati ya mwaka 2011 na 2015. Ripoti hiyo inasema kuwa nchi nyingi zimebuni chanjo mpya hali ambayo imechangia kuzuia vifo vingi na kuimarisha afya na maisha ya mamilioni ya watu. Ripoti hiyo inasema kuwa mwanya uliopo kati ya wanaopata chanjo na wale wanaokosa kati ya nchi tajiri na maskini unazidi kupungua. Kwenye wilaya ya kilifi nchini Kenya kwa mfano idadi ya watoto wanaolazwa wakiugua magonjwa ya njia za hewa ilipungua kutoka 38 hadi sufuri kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu tangu kuanza kutolewa kwa chanjo hiyo. Dr Seth Berkley ni Mtendaji Mkuu wa GAVI.

(Sauti ya Dkt. Seth)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031