Baraza la Usalama lapitisha azimio la kuongeza usaidizi wa UM kwa CAR

Kusikiliza /

Charles-Armel Doubane, Mwakilishi wa kudumu wa CAR katika Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongeza nguvu za ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, na usaidizi wa Umoja wa Mataifa kwa taifa hilo. Joshua Mmali na taarifa kamili

(RIPOTI YA JOSHUA MMALI)

Kwa mujibu wa azimio namba 2021 linaidhinisha kuongeza nguvu ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kumwomba Katibu Mkuu Ban Ki-Moon kufanya tathmini ya usaidizi zaidi unaoweza kutolewa na Umoja wa Mataifa kwa vikosi vya Muungano wa Afrika vya kurejesha utulivu na kuleta amani nchini humo.

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye Umoja wa Mataifa, Charles-Armel Doubane ameelezea furaha na shukrani zake kwa kupitishwa azimio hilo, akisema linawapa watu wa jamhuri ya Afrika ya Kati mwanzo mpya.

"Hili kwa wanaume na wanawake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ni mwanzo mpya. Nasema hivi kwa sababu huu ni mwanzo wa mwisho wa mateso yao. Azimio hili linachukua msimamo na kuweka njia ya kufuata."

Baraza hilo pia limepokea ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, MINUSTAH na ripoti kuhusu hali nchini Afghanistan, na athari zake kwa jamii ya kimataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031