Baraza la Usalama laangazia hali ya Darfur na ujumbe wa UNAMID

Kusikiliza /

Walinda amani wa UNAMID

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali magharibi mwa Sudan na majukumu ya ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika eneo la Darfur, UNAMID. Assumpta Massoi na taarifa kamili:

TAARIFA YA ASSUMPTA

Katika kikao cha leo, Baraza hilo la Usalama limesikiliza ripoti ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa UNAMID, Mohamed Ibn Chambas, ambaye amelihutubia kwa njia ya video kutoka Khartoum, Sudan.

Katika ripoti yake, Bwana Chambas amesema hali ya usalama Darfur na jinsi inavyotishia hata usalama wa walinda amani, imeendelea kuwa ya kutia wasiwasi, huku akiendeleza wito wake kwa serikali ya Sudan kufanya juhudi zaidi ili kuhakikisha wanaoendeleza mashambulizi dhidi ya walinda amani wanakabiliwa na mkono wa sheria.

"Ingawa mikataba kadhaa ya usitishaji mapigano imesainiwa, hali bado ni tete. UNAMID inaendelea kuwezesha ufikishaji wa misaada ya kibinadamu kwa jamii zilizoathiriwa. Visa vya kuzuiwa kuzifikia jamii hizi, kuwepo uhuru mdogo wa kusafiri pamoja na ukiritimba, vyote vimeendelea kuwa changamoto ambayo inaathiri vibaya juhudi zetu hizi za pamoja."

Bwana Chambas amesema licha ya kupigwa hatua chache kuhusu masuala ya umiliki wa ardhi na ujumuishaji wa watu wa Darfur katika huduma za sheria na umma, hakujakuwepo hatua zozote za dhati za kutekeleza vipengee vya usitishaji kabisa mapigano na mikataba yote ya mipango ya amani usalama. Mwingine aliyelihutubia baraza hilo ni Herves Ladsous, Mkuu wa Shughuli za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031