Baraza Kuu lapitisha azimio kuhusu biashara ya utumwa, Mnara maalum kujengwa New York

Kusikiliza /

Majaji wa shindano , na mshindi wa sanamu ya mnara, “safina ya marejeo”, Rodney Leon

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limepitisha rasimu ya azimio kuhusu kumbukumbu ya kudumu ya madhila ya biashara ya utumwa iliyofanyika kupitia Bahari ya Atlantiki zaidi ya miaka 200 iliyopita. Ripoti ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.

 (Ripoti ya Grace)

 Kikao cha 35 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilirejelea azimio la mwaka 2001 kuhusu biashara hiyo ya utumwa lililotaka kuwepo na mnara wa kumbukumbu ya wahanga wa biashara hiyo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Rais wa Baraza Kuu John Ashe akasema picha ya sanamu ya mnara iliyoshinda ni ile iliyobuniwa na Rodney Leon waHaitiikiwa na maudhui "Safina ya marejeo."

 (Sauti ya Ashe)

 ”Kama vile ambavyo minara mingine ya kumbukumbu imejengwa kweney eneo la Umoja wa Mataifa kukumbusha jamii ya kimataifa kutambua thamani ya amani na kutokuwepo ghasia, ni matumaini yangu kuwa mnara wa Safina ya marejeo utakaojengwa karibuni utafanya vivyo hivyo kama mchango wa chombo hiki wa kuendeleza amani, haki za binadamu, haki za kijamii na utu wa binadamu."

Na hatimaye ikawa hatua za kuhakikisha biashara hiyo dhalili hairudiwi tena, Baraza likapitisha azimio ambalo lilitambulishwa na Mwakilishi wa kudumu waJamaicakwenye Umoja wa Mataifa balozi Courtenay Rattray ambaye alisema kamwe biashara hiyo isirejewe tena na hatua zichukuliwe ili kila mmoja afahamu madhila yake kwani binadamu wote ni sawa na wanastahili utu.

 (Sauti ya Balozi Rantrray)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031