Ban ataka wamisri waandamane kwa amani Jumapili

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Wakati wananchi wa Misri wakijiandaa kwa maandamano siku ya Jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza umuhimu wa maandamano hayo kufanyika kwa amani bila ghasia yoyote na kuzingatia haki ya watu kukusanyika. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Bwana Ban akielezea pia wasiwasi wake kutokana na vurugu kubwa zilizotokea leo kwenye mji mkuu wa Misri,Cairo. Amerejelea kauli yake ya kuhakikisha kuna ushirikishwaji wa mawazo ya kisiasa, kuheshimu haki za binadamu ikiwemo hata za wale wanaoshikiliwa magerezani bila kusahau utawala wa kisheria ambao amesema ni chimbuko la amani na kipindi cha mpito wa demokrasia. Amesema hiyo ni misingi ambayo hata mamlaka za Misri zimeridhia kwenye mpango walioandaa juu ya mustakhbali wa nchi hiyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031