Ban astushwa na kuzama kwa boti nyingine ya wahamiaji:

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amestushwa kusikia taarifa za kupotea kwa maisha ya watu baada ya boti nyingine iliyobeba wahamiaji kuzama Ijumaa katika pwani ya Italia. Amesema hii ni ajali nyingine siku chache tu baada ya watu zaidi ya 300 kufa maji kwenye kisiwa cha Lampedusa wiki iliyopita. Katibu Mkuu ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kwa ujumla kuchukua hatua kuzuia madhila kama haya katika siku za usoni ikiwemo hatua za kushughulikia vyanzo vyake na kutoa kipaumbele kwa kulinda haki za binadamu za wahamiaji wakati wa kupata suluhu ya matatizo haya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031