Ban asikitishwa na kucheleweshwa kwa uchaguzi Maldives

 

Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema ana wasiwasi mkubwa kutokana na kucheleweshwa kufanyika tena kwa uchaguzi wa rais nchini Maldives baada ya mahakama kuu nchini humo kufuta ule wa kwanza wa tarehe Saba Septemba licha ya jitihada za tume ya uchaguzi. Msemaji wa Umoja wa Mataifa amemkariri Katibu Mkuu akitoa wito kwa pande zote nchini humo kuendeleza utulivu na kutaka viongozi wa kisiasa na taasisi za serikali kutekeleza wajibu wao, kuheshimu mchakato wa kidemokrasia na hatimaye kushiriki kwa amani kwenye uchaguzi jumuishi mapema iwezekanavyo ili Rais mpya aweze kuapishwa tarehe 11 mwezi ujao kwa mujibu wa katiba. Bwana Ban amesema matarajio na utashi wa wananchi wa Maldives yaliwekwa bayana tarehe Saba mwezi uliopita wakati wa uchaguzi na anaamini kwamba utashi wao haupaswi kukiukwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031