Ban ashutushwa na kutekwa nyara kwa waziri mkuu wa Libya

Kusikiliza /

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon ameelezea kustushwa kwake na taarifa za hapo awali kwamba Waziri Mkuu wa Libya , Ali Zeidan, ametekwa nyara na watu watu wenye silaha mjini Tripoli.Akizungumza na waandishi wa habari nchini Brunei Bwana Ban amesema amefanya mawasiliano na mwakilishi wake maalum nchini Libya , Tarek Mitri,ambaye amekuwa katika juhudi za kuwasiliana na mamlaka nchini humo kuhakikisha usalama wa Waziri Mkuu huyo pamoja na kuvuka salama kwa kipindi cha mpito nchini Libya.

(Sauti Ban)

Nilishtushwa kusikia kwamba Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeuidan, alitekwa nyara asubuhi ya leo, natumaini kwamba taarifa kutoka Libya kwamba ameachiwa ni kweli japo hazijathibitishwa.

Hata hivyo taarifa za kuachiwa kwa Waziri Mkuu wa Libya zimethibitishwa hivi punde.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031