Ban ahimiza kujali maslahi ya wazee kwenye Siku ya Afya ya Akili

Kusikiliza /

Mshauri wa afya ya akili akizungumza na wagonjwa DRC

Katika kuadhimisha Siku ya Afya ya Akili Duniani, leo Oktoba 10, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema siku hii inatoa fursa ya kuongeza ufahamu kuhusu matatizo ya afya ya akili wanayokumbana nayo wazee, hususan wenye umri wa miaka zaidi ya 60.

Bwana Ban amesema wakati watu wengi hutazamia kuufikia umri wa uzeeni unaoridhisha, mmoja kati ya wazee watano wenye umri wa zaidi ya miaka 60 hukabiliwa na matatizo ya akili. Amesema wazee pia huwa kwenye hatari ya kutelekezwa na kudhalilishwa, na hivyo, kuibua matatizo ya afya ya akili.

Katibu Mkuu ametoa wito wa kutekelezwa mkakati ulowekwa mna mo Mwezi Mei mwaka huu na Baraza la Afya Duniani, wenye lengo la kuunganisha huduma za kijamii na huduma za afya ili kukabiliana na matatizo ya afya ya akili hadi mwaka 2020.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031